Itaonekana ni jambo la ajabu kuwashauri kobazi kufuga nguruwe lakini ushauri huo umetolewa na Abubakari Mwaibabile wa msikiti wa Sabasaba katika kitongoji cha Holemela,Mbarali Mbeya,wakati akiyasema hayo aliwasisitiza waislamu kuielewa Quran zaidi na kutokubaliana na mambo ambayo hayako katika Quran,aliendelea kufafanua kuwa Quran haijakataza kufuga nguruwe bali imekataza kula nguruwe,alisema hata yeye amekuwa akifuga nguruwe ambao wamempa manufaa ya kiuchumi ikiwemo uwezo wa kuwalipia karo watoto shuleni,alisisitiza waislamu hawakatazwi kufuga nguruwe kwa ajili ya kujikwamua kutoka katika dimbwi la umasikini