Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 8,870
- 14,258
Kuna hali zikitokea katika nchi au mbali ya miji waislamu humuelekea Allah aliyetukuka ili awape msaada. Na hiyo ina dalili kutoka kwa Mtume swalaLlaahu alayhi wassalam mwenyewe.
Baadhi ya matukio hayo ni pale nchi inapopata ukame mpaka watu wemekata tamaa na uhai wao. Watu hutoka nje ya mji katika hali ya kujidhalilisha kwa kuvaa zile nguo zao mbovu na kubebe vyombo vya maji huku wakiviweka juu chini na kuomba kwa unyonge mwingi ili wahurumiwe wapate maji.
Matukio ya aina hiyo yapo mengi.Hata wakati wa corona miaka 3 iliyopita waislamu wa Tanzania walipotishika na vifo vilivyotajwa kutokana na maradhi hayo misikiti mingi ilikumbuka dua maalum iitwayo kunuti na walikuwa wakiileta kila baada ya kipindi cha swala.
Katika muda huu ambapo jeshi la Israel limejichimbia Gaza na kuzima mawasiliano na kuzuia chakula na maji visiwafikie wote waliopo eneo hilo,ni wakati muwafaka wa kuleta kunuti kila baada ya swala au angalau mara mbili kwa siku kuomba nusra kwa wapalestina.
Ni kweli wale wenye moyo wa kuwasaidia hawawezi kufika huko kwa namna mbali mbali,hata hivyo dua zao zinapenya moja kwa moja bila kizuizi cha mdudu yoyote.
Wako waislamu wengi binafsi tayari wanaomba dua nzito kwa ajili ya ndugu zao wapalestina lakini ipo haja ya kuanza dua za pamoja ili kupata matokeo ya haraka.