Waitara: Wote waliothibitika kuiba fedha za serikali wanyongwe!

Rare Sapphire

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2021
Posts
590
Reaction score
1,648
Msikile Waitara akitema cheche hapa

Your browser is not able to display this video.

Asema watanzania wengi wanaisha maisha ya ufukara sana kiasi cha kushindwa hata kuwalipia ada watoto wao na kwenda kuomba msaada wa kufanikishiwa jambo hilo, akisema watumishi wa umma wote wanasomeshwa na watanzania na wana elimu ya kutosha, na kwamba wanafanya makusudi na kuiba kwa utaalamu.

Your browser is not able to display this video.

Akisema uzembe upo kwa wabunge, kama mtu ameiba ripoti ipo, taarifa zipo, vyombo vipo, lakini mwizi hawajibishwi, je wanafundisha nini vijana wa Tanzania? Kwamba mtu ataiba na kuhamishwa tu wizara bila ya kuwajibika? Ataka wote waliothibitishwa kuhusika na wizi huo wanyongwe.

Asema wasisubiri kuambiwa kuwa wanantakiwa kuchukua hatua, bali wawajibishe sababu wao wabunge ndio wenye dhamana ya kufanya hivyo. Asema kama fedha zinatolewa kwaajili ya ripoti ya CAG kufanya uchunguzi halafu hakuna kinachofanyika zaidi ra ripoti hizo kuwekwa kwenye makabati na mwaka unaofata mambo kuwa yale yale, yeye Waitara ataachana na kuchangia maoni juu ya ripoti hiyo.
 
Hili ndio pendekezo langu lengo ni kufuta kizazi cha aina hii katika Taifa.

Hatuwezi kupiga hatua tukiwa na watu wa aina hii ambao hata Mwalimu alliwasema hadharani kuwa wana tabia za "kimalaya malaya".

Nawasilisha
 
Hili ndio pendekezo langu lengo ni kufuta kuzazi cha aina hii katika Taifa.

Hatuwezi kupiga hatua tukiwa na watu wa aina hii ambao hata Mwalimu alliwasema hadharani kuwa wana tabia za "kimalaya malaya".
Naunga mkono hoja 100%
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…