Nakubali kwamba Tanzania kuna changamoto nyingi tu, niseme haya yafuatayo:
Mosi, Tanzania inaweza kutengeneza Healthiest Dependency Ratio kwasababu, watu wenye uwezo wa kufanya kazi (Working Age Population) ni wengi kuliko wale wasioweza kufanya kazi (Dependents). Hili ni tatizo la kisera ambalo serikali ikiwa makini inaweza kulimaliza kama Uchina walivyofanya. Injecting the youths into the Market, either through employment and self-employment. Tanzania imejaa vijana waliomaliza chuo kikuu wenye utaalamu mwingi ambao wanaweza kufanya kazi endapo watawezeshwa na kusaidiwa.
Pili, FDI ni muhimu na Tanzania ni nchi ambayo ni kivutio kikubwa. Hili mbona halina ubishi. Tatizo ni lilelile la kisera, kwamba tunafanyaje kuhakikisha kwamba watanzania wa kawaida wananufaika na uwekezaji kutoka nje, aidha kwa kupitia kodi, ajira, ujuzi na ushirikishwaji katika uwekezaji. Mpaka sasa faida haionekani kwasababu kuna sehemu panavuja na hatujasimama kidete kuhakikisha tunarekebisha. Mashirika mengi yanapewa Tax Holidays na mikataba ya uwekezaji ina changamoto kama ule wa bandari. Ila binafsi naamini leo hii tukiamua kukusanya kodi kwa mashirika yanayowekeza hapa nchini, hela ipo nyingi mno.
Tatu, kwenye biashara ya kimataifa sisi ni Commodity Based Economy bado hatujawa Industrial Based Economy au Financial Based Economy nadhani tuendelee kujikita huko ambako tuna Comparative Advantage. Soko la dunia ya leo linahitaji sana rasilimali za uzalishaji ambazo Tanzania inazo kwa wingi na zinaiuzwa kwa Benchmark Price. Tunaweza kufanya mambo mengi mno kupitia Bilateral Trade na tukafanikiwa vizuri sana, tatizo ni kwamba watu wanafanya maksudi kwasababu wanataka kupata mafungu ya kumi (Ten Percent).
Nne, viwanda vidogo-vidogo vya kutengeneza Toothpick vinaweza kuanzishwa nchini Tanzania hata kesho endapo tutaamua. Kipindi hiki inawezekana kwasababu watu wengi wana mitaji na ujuzi, na uwepo wa soko la ajira la bei nzuri (Cheap Labour). Tatizo tunarudi palepale, kwamba watu wananufaika wenyewe na hii hali.
Niseme tu, hakuna pesa ambayo inatengenezwa Tanzania isionekane. Pesa zipo lakini zinaingia mifukoni kwa watu ndiyo maana uchumi kweli unakua lakini wewe mtu wa kawaida huuoni kwasababu, watu wachache wanazitafuna na kujimilikisha nchi. Hili ndiyo changamoto yetu Tanzania.