Basi naomba takwimu za Raisi aliyefanya vizuri kuliko wote hapa nchini kwenye suala la uchumi. Nasubiri majibu!
Mkuu kila mmoja alijitahidi kwa namna yake. Kwanza kabisa Julius K. Nyerere aliikuta Tanganyika ina uchumi imara Afrika Mashariki. Akataifisha, akajenga viwanda kadhaa, akaleta ujumaa uchumi ukaanguka mpaka kila kitu kikakwama, akafunga nchi hakukuwepo na demokrasia, hadi Nyerere anang'atuka nchi ilikuwa nchi ya mwisho masikini duniani!
Akaja Mzee ruksa, Ali H. Mwinyi, akafungua mipaka ya nchi. Nchi ikaanza kupumua. Akapambana na uchumi, angalau maisha ya wananchi yakawa na ahueni kiasi ukilinganisha na kipindi cha Mchonga, ila hadi anaondoka serikali ilikuwa hoi bin taaban.
Mzee wa ukweli na uwazi Benjamin W. Mkapa akaingia, akaweka mifumo ya mapato, uongozi, usimamizi na udhibiti serikalini. Akapunguza mzigo wa madeni ya nje, akawezesha ubinafshishaji na kuvutia wawekezaji wa ndani na kutoka nje . Hadi anaondoka demokrasia ilishaanza kushamiri na uchumi ulikuwa umeanza kutengamaa na serikali ilikuwa na hela.
Akaingia Mzee wa mtandao; ari mpya, nguvu mpya na maisha bora kwa kila mtanzania, Jakaya M. Kikwete. Kaanza kwa kupanua wigo wa demokrasia, akajenga miundombino ya barabara nchi nzima kuunganisha mikoa na wilaya, akaongeza viwanda, akapanuwa uwekezaji kwenye viwanda, elimu, afya, benki, ujenzi, utalii, nishati, uchukuzi, mawasiliano, maji na kilimo. Akaimarisha maslahi ya watumishi wa umma, akaongeza ajira kwa vijana kuliko Rais yeyote nchini, Akaimarisha usalama kila kona ya nchi. Akagatua madaraka kwa kuongeza mikoa na wilaya kama sehemu ya kupelekea huduma na maendeleo zaidi kwa wananchi. Mahusiano na diplomasia ya nchi yetu ikafikia viwango vya juu duniani. Volume ya biashara ndani na nje ya nchi ikawa kubwa sana kiasi cha kuifanya kariakoo kuwa hub ya biashara kwa nchi za burundi, Uganda, Rwanda, Comoros, Madagascar, Malawi na Zambia. Aliwekeza kwenye usalama wa majeshi yetu ya ulinzi kiasi cha kutambulika kimataifa. Kama kuna wakati wanainchi wengi waliweza kufanya maendeleo yao binafsi ni kipindi cha awamu ya 4. Hata msingi wa kufikia uchumi wa kati ulitokana na uchumi aliouimarisha Jakaya. Hadi anaondoka wananchi walikuwa na hela na serikali ilikuwa na hela
Akaingia Mzee wa hapa kazi tu John P. Magufuli! Ikawa kazi kweli kweli! Akavuruga wafanyakazi kisa vyeti feki, wafanyabiashara, wawekezaji, wapinzani na majirani. Miaka mitano tu nchi ikawa na deni la nje tirilioni 66 kutoka tirilioni 26, kiwango cha demokrasia kikashuka, mahusiano ya nje yakaporomoka, bidhaa zikapanda bei, ajira ikawa mtihani. Akawa juu ya katiba na mizizi ya utawala wake ikajichimbia zaidi, upendeleo wa maendeleo ukazaliwa na ufisadi wa kihistoria ukatokea Ikulu! Akawaibia machinga kwa kuwa vitambulisho visivyo na maana, mauwaji yakashamiri, vyombo vya habari vikaufyata, viongozi wa dini wakatishiwa kufutiwa uraia wao! Na uporaji wa fedha za maduka ya kubadilisha kutumia jeshi mchana kweupe. Kwa mara ya kwanza fremu Kariakoo zikakosa wateja! Akaturudisha nyuma miaka 30, Mungu akaingilia kati, akaenda zake! Hadi anaenda zake vyuma vilikuwa vimekaza ajabu! Wananchi na serikali ilikuwa hoi! Hawana hela!
Ndio akaingia mama wa Kazi iendelee; mama wa 4R Samia S. Hassan. Kakuta mvurugano zaidi ya mkorogano, nchi ilikuwa imegawanyika, uchumi upo hoi, Kakuta miradi mikubwa isiyo na vyanzo vya hela, kakuta ajira hakuna kwa miaka 6, kukuta demokrasia iko taaban, mifumo ya serikali haifanya kazi na mahusiano ya nje yameparaganyika. Ndio akaanza kutanzua, kufungua na kuzibua palipoziba.
Kwa sasa nchi ameituliza, mahusiano ya nje yamerudi, biashara imeanza kuimarika na uwekezaji umeanza kurudi, demokrasia inaendelea inachipua. Ugumu unao onekana ni matokeo ya uharibifu na uchafu uliofanywa na awamu ya 5. Hata hivyo Samia anapamba sana, ni kazi ngumu kweli kweli! Hadi anamaliza muhula wake wa kwanza atakuwa amemaliza kusafisha na kusawazisha uharibifu alioukuta!