Wajamaa mnisaidie, hivi Nyerere aliwezaje kuvumilia haya?

Angalau hakuna ushahidi kwamba Nyerere alinyang'anya watu mali kwa maslahi yake binafsi au ya wale waliomzunguka. Nyerere alikuwa na makosa na kasoro zake nyingi ila ni vigumu kuziona katika mrengo wa maslahi yake binafsi, familia au waliomzunguka.
 
Ule ni mfumo wa utaahira ambao ulilenga kuwafukarisha watu Ili uwatawale.

The likes of Magufuli system ilikuwa Ukiwa na tu mil.10 wewe ni mhujumu uchumi utaletewa Kila Figisu ili tuu uendelee kuwa mnyonge na kumpogia makofo Jiwe.

Jiwe anajua fika ukitaka kumtawala mtu mfanye maskini.

Tofauti na Samia anajaribu Kuwavutia wenye pesa upande wake Ili asipate shida kwenye kutawala.
 
Nyerere aliupenda sana udikteta wa China kipindi cha mwenyekiti Mao kitu kingine Nyerere huyo huyo alienda China kwa mara ya Kwanza katika miaka ya 60 kipindi ambacho China kulikuwa na ubabe wa kutisha wa genge la Mao kwa wale wasio wafuasi wake.

Hiyo miaka ya 50 na 60 ndio kipindi China ilikuwa inafanya blunder nyingi kubwa za kiuchumi zilizo wagharimu na Nyerere alicopy na zikamuangukia pua.

Utofauti wake na Mao ni baada kutokuelewana kati ya Usovieti na China Mao kuamua kuamisha upepo na kufungua milango ya magharibi miaka ya 70.
 
Tanzania bado ni masikini sana hata cha kugawana bado ni kidogo, huwa nashangaa watu wanaoshangilia ukuaji uchumi usiozidi 7%. Uchumi wa China wakatia unawaondoa raia wake wengi katika umaskini ulikuwa unakuwa hadi kwa 14%. Sisi angalau hatukapaswa kushuka chini ya 10% hata kwa miaka 10 mfululizo.
 
Anza sasa sie tutakuunga mkono.
Sio unashinda unatype JF, jichome moto kama jamaa wa Tunisia utakuwa umesukuma mabadiliko.
Kila mtu ana mbinu yake. Ww niunge mkono kwa mbinu ya huyo jamaa wa Tunisia.
 
Magufuli na Samia wote sawa.

CCM imejaza watu wa ajabu ajabu na machawa kama wewe
 
Hakika, Tanzania bado tunajitafuta kwenye suala la uchumi na maendeleo, bado tuko mbali sana.
 
Utofauti ni kwamba Nyerere yeye hakuwa tayari kuacha ukatoliki na kuwa mkana Mungu kama idol wake Mwenyekiti Mao na wakomunisti wa China.
 
Hii katiba inayomfanya Rais awe juu ya Sheria ni yeye aliiweka. Unatarajia Nini kama cheo Cha rais ndio kinapanga nani awe kiongozi? Au unadhani misingi mibovu ya hivyo inaondoka kirahisi huku afrika bila machafuko na mapinduzi ya kijeshi?
Katiba inaweza kuwa tatizo lakini kuna matatizo ya Waafrika ni common na ni vigumu mno kuyaelezea wakati mwingine.
Mfano Kenya wana Katiba nzuri ila ufisadi umetamalaki na pia viongozi wanapatikana zaidi kwa demokrasia ya ukabila, huu ni mtanziko wa aina yake.
 
Angalau hakuna ushahidi kwamba Nyerere alinyang'anya watu mali kwa maslahi yake binafsi au ya wale waliomzunguka. Nyerere alikuwa na makosa na kasoro zake nyingi ila ni vigumu kuziona katika mrengo wa maslahi yake binafsi, familia au waliomzunguka.
Ndio hapo niliposema Kuna tofauti ndogo sana ya mambo ya utawala wa Nyerere na wa sasa. Ni kweli hakufanya maamuzi mengi kwa maslahi yake binafsi, lakini Bado hakuruhusu maamuzi yaliyokuwa hayamfurahishi. Na Hawa wengine wameiga huko huko japo Kuna tofauti Fulani ya approach.
 
Lakini kwa upande wa demokrasia hasa unaolindwa na katiba ya Kenya, wako maili nyingi kulinganisha na sisi. Sisi hatuna ukabila hilo ni kweli, lakini wenye ukabila wana demokrasia nzuri kuliko sisi.
 
Mimi ni moja ya waamini kuwa Tanzania inahitaji black enterprises nyingi zaidi kuliko wawekezaji. Hapa tulipo tu uchumi umeshikiliwa na watu ambao hawana asili ya Tanzania lakini private sector imeshikiliwa na multinationals hivyo, kuhimiza uwekezaji wa foreigners ilhali Tu watanzania bado hawajafikia kiwango cha kutengeneza biashara kubwa kiasi cha kutumia rasilimali zilizopo ipasavyo,

Tutangeneza taifa lenye uchumi unaomilikiwa na wageni huku wenyeji wakibaki kama vibarua

Kwenye uchumi kwa sasa naona diversity imekuwapo haswa baada ya service and creative industry kuja juu japo, tourism inachangia pakubwa lakini nilitamani tuwekeze nguvu kwenye utalii wa mijini ili hata miji yetu ifikie global standards za kuhost watalii kama Rwanda inavyojitahidi kuifanya kigali kuwa mji wa kitalii wa kiteknolojia, burudani na mikutano.

Gaps zipo nyingi sana za kushauri na sidhani kama zitafanyiwa maana kama ulivyosema. Mfumo uliopo unanufaisha baadhi ya watu
 
Ukabila usingeweza kutokea Tanganyika.

Moja ya blunder kubwa ya Nyerere ni totally failure ya kushindwa kutengeneza nchi moja Tanzania.

Huyu mtu unamsifu kwa sababu gani nchi ya Tanganyika? Kama tu kuunda taifa moja la Tanzania alifeli ni kipi unacho msifu ?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…