Wajamaa mnisaidie, hivi Nyerere aliwezaje kuvumilia haya?

haya mambo uliyoandika hapa yanafikirisha sana!
 
Umesahau kuwa elimu ilikuwa bure mpaka chuo kikuu, huduma za afya zilipatikana bure nchi nzima, viwanda vingi vilijengwa na ajira kwa wasomi zilikuwa za kutosha nk.
Elimu ilikuwa Bure lakini ilikuwa irrelevant chini ya mfumo ule wa chama kushika hatamu wasomi hawakufurukuta, unamjua Rashid kawawa weWe alafu umletee usomi?

Miaka hiyo wasomi wengi walikiambia nchi ilikuwa ni ngumu sana nyerere kufanya kazi na wasomi wanaojitambua
 
Umesahau kuwa elimu ilikuwa bure mpaka chuo kikuu, huduma za afya zilipatikana bure nchi nzima, viwanda vingi vilijengwa na ajira kwa wasomi zilikuwa za kutosha nk.
Nakusoma mkuu, lakini naomba niulize tu:
Kipindi cha MTAKATIFU RAISI NYERERE vyuo vikuu vilikuwa vingapi na wanafunzi waliosoma walikuwa ni wangapi ?​
 
Mkuu The Boy Wonder , asante kwa bandiko hili, hata hivyo majibu ya bandiko hili, hayatasaidia lolote kwenye ule mchakato, mchakato unaendelea!.
P

Mkuu, kila nyakati zina mambo yake ambayo kwa wakati huo inaonekana ni sahihi. Wakati ule jamaa ulionekana una maana, hasa katika kulinda rasilimali za nchi.

Lakini wakati Nyerere akifanya hayo, yeye alijirundikia Mali au aliishi kijamaa?

Kila jambo na wakati wake, ndio maana utaona hata nchi za Kiarabu zimeanza kuachana na mfumo wa kiafidhina wa Kiislam, sasa wanaanza kuwa huru, utaona nchi kama Saudi Arabia mabadiliko ni makubwa, watu wako huru
 
Mkuu The Boy Wonder , asante kwa bandiko hili, hata hivyo majibu ya bandiko hili, hayatasaidia lolote kwenye ule mchakato, mchakato unaendelea!.
P

Mkuu, kila nyakati zina mambo yake ambayo kwa wakati huo inaonekana ni sahihi. Wakati ule ujamaa ulionekana una maana, hasa katika kulinda rasilimali za nchi.

Lakini wakati Nyerere akifanya hayo, yeye alijirundikia Mali au aliishi kijamaa?

Kila jambo na wakati wake, ndio maana utaona hata nchi za Kiarabu zimeanza kuachana na mfumo wa kiafidhina wa Kiislam, sasa wanaanza kuwa huru, utaona nchi kama Saudi Arabia mabadiliko ni makubwa, watu wako huru
 
Mkuu, wewe ni prominent member humu na huwa unaandika vitu vyenye msaada mkubwa kimawazo na kielimu kwetu. Ila ukweli usemwe, ktk bandiko hili haujawa objective sana. Elimu yako umeipata kipindi cha Nyerere Kam ulivyosema. Sasa kwa mfano mmoja tu huo, fananisha mtu mwenye elimu sawa na wewe kwa wakati huu utapata picha fulani ambayo utaigeneralize ktk vitu vingi vinavyoendelea baada ya uongozi wa awamu ya kwanza.
 
Nakuelewa lakini wewe ambaye ni Mkubwa naomba unisaidie kutoa haya majawabu.

Mosi, Mzee Nyerere na Mzee Mtei walipishani kwasababu gani. Je, mambo aliyoshauri Mtei yalikuwa mabaya hadi Nyerere kuamua kumfanyia vile? Hivi Unadhani Mzee Nyerere angekubali kufanya mabadiliko miaka ya 70's unadhani nchi ingepitia kipindi kigumu kama kile cha miaka ya 80's?

Pili, nchi ilianza kudorora uchumi tokea mwaka 1980, kwanini Mzee Nyerere hakutaka kuchukua hatua zozote zile kusaidia wananchi waliokuwa kwenye lindi kubwa la umasikini, mpaka kusubiri mwaka 1984 baada ya Mzee Dr Salim kufanya ziara kule Lindi na kumwambia Mzee Nyerere kwamba hali ilikuwa ni mbaya. Kwanini miaka yote hii alikuwa hawaonei huruma watanzania?

Tatu, kwanini Mzee Nyerere alikuja kuzikubali sera zote alizozikataa (Japo siyo vigezo vyote vya SAP vilikuwa vinatekelezeka), alizisaini mwaka 1984 na zikaanza kutekelezwa na Mzee Mwinyi. Kama sera zilikuwa ni mbaya kihivyo kwanini alizikubali baadaye ?

Nne, mbona Uchina alikioga mfumo wa Ujamaa walifanya mabadiliko mapema miaka ya 70's na hawakupata matatizo yoyote, zaidi zaidi walifanikiwa mno. Tanzania tulikuwa na uziada upi wa kuchelewesha mabadiliko kwa muda mrefu ilhali wananchi wakiwa wanapitia mateso?

Lengo lake haswa lilikuwa ni nini ?​
 
Hii ni baadhi ya sifa za kweli alizokuwa nazo Nyerere, ili hili likatiba alitukosea sana.
 
Malawi walifuata siasa gani ? Au nao walikuwa wajamaa....tutsjie nchi za africa ambazo azikufuata ujamaa tuona zilivyo na uchumi wa kitajiri kama nchi za asia ...ili tuone kama wewe unayo akili kichwani
Putting states in a monolith and then judging them will not spare the fallacy of generalization.

Hii tabia ya kupenda kulinganisha nchi za Afrika kwa kuziweka kwenye kundi moja kama mayai ni kichaka cha watawala wengi na wasomi wavivu kukwepa kuwajibika. Mazingira ya Tanzania ukilinganisha na nchi nyingine za Afrika yalikuwa na utofauti mkubwa sana hata kama mtalazimisha kufanana. Tanzania ilikuwa na nafasi ya kufanya vizuri pengine kuliko nchi nyingine zote za Afrika. Ukifiatilia vizuri utafahamu kwamba Tanzania ilikuwa na kila kitu kuweza kuwa tajiri zaidi ya nchi zingine zote hapa Afrika. Nyerere squandered the opportunity.​
 
Objectivity/Upembuzi yakinifu ni kuweza kuchambua sifa za kitu na kuziangalia, kuzitaja na kuzielezea kama zilivyo bila kuingiza misimamo binafsi (Personal Inclination/Ideology). Mzee Nyerere alikuwa na mazuri yake ambayo yanaimbwa, lakini alikuwa na mabaya yake ambayo yalifichwa na wengi hawapendi kuyaongelea kwasababu wanalinda heshima yake. Ukweli mchungu ni kwamba watanzania wengi hawawezi kufanya upembuzi yakinifu ndiyo maana ni ngumu kubadilika na kujifunza kutokana na makosa.

Mzee Nyerere alikuwa na nafasi ya kufanya makubwa kuliko Raisi yoyote hapa Afrika, lakini sera zake za uchumi ambazo ndizo zinaendesha kila kitu zilifeli vibaya mno kwasababu hakupenda kusikiliza ushauri na hakusoma vizuri majira na nyakati. Ujamaa ni sera ambayo tuliige Uchina na Urusi. Ujamaa ulifeli na kusababisha madhara huko Uchina na Urusi tulikouiga japo walau wenzetu walifanikiwa kwenye baadhi ya mambo. Mataifa mengi ya kijamaa yalianza kudidimia miaka ya 70's baada ya mtikisiko wa uchumi wa dunia. (Hapa sipo objective kivipi ?)

Uchina sera za Mao kama The Great Leap Forward na The Cultural Revolution zilisababisha madhara makubwa, na kuacha mamilioni ya wachina wakiwa wamekufa. Baada ya Mao kufariki wachina wakiongozwa na Deng Xiaoping wakaanza kufanya mabadiliko kwenye mfumo mzima ili kusaidia watu. Ikumbukwe kwamba mabadiliko ambayo Uchina iliyafanya miaka ya 70's chini ya Dend Xiaoping yalipendekezwa kufanywa miaka ya 60's lakini Mao na wenzake wakawafunga gerezani wakina Deng Xiaoping na kumuua Liu Shaoqi ambaye aliratibu maendeleo hayo.

Alichokifanya Mao nchini Uchina hakina tofauti na alichokifanya Mzee Nyerere nchini Tanzania. Wote walishauriwa kwamba wafanya mabadiliko miaka ya 60's lakini wakakataa. Mao aliwafunga waliomshauri afanya mabadiliko na kuwaita mabeberu hata wengine kuuawawa. Mzee Nyerere naye ndiyo aliyefanya hivyo hivyo, wakina Mtei na kina Rweyemamu hawakusikilizwa na wakaonekana kama ni vibaraka fulani hivi. Uchina bahati nzuri Mao aliondoka mapema na wakaanza kufanya mabadiliko kwa kasi na kuruhusu mfumo wa masoko.

Tanzania watu walikuwa wanahangaika lakini Mzee Nyerere aliendelea kukomaa. Hili nalo nikilesema mnashindwa kulimeza halafu mnaanza kunifundisha kuhusu OBJECTIVITY. Mzee Nyerere hakuwa na ufahamu mzuri kwenye uchumi wa masoko huu ndiyo ukweli. Hata Deng Xiaoping wa Uchina alikuwa hana huo ufahamu, hivyo akaamua kwenda Singapore kufundishwa na Waziri Mkuu Deng Xiaoping. Wasomi wa Uchina walifundishwa na wasomi wa Singapore kuendesha nchi. Huu ndiyo ukweli. Sasa mkiendelea kulazimisha kwamba Mzee Nyerere alikuwa ni malaika anayejua kila kitu ilhali wenzake kama Deng Xiaoping walikubali kufundishika, napata ukakasi mno na namna mnaitizama hii dunia.

USSR nako ilikuwa hivyo-hivyo, Andropov aliona kabisa Ujamaa unahitaji mabadiliko na akakiri mwaka 1982 mbele ya mkutano mkuu wa chama kwamba kama Urusi inataka kufanikiwa ni lazima ibadilike. Bahati mbaya alikaa madarakani miaka miwili tu, na hakufanikiwa kutekeleza aliyotaka kuyafanya. Sasa watu ambao Ujamaa mmeiga kwao wanakubali kubadilika kwasababu mfumo wa Ujamaa was not sustainable, nyie ambao mmeletewa mlikuwa mnakataa nini ?

Tunauliza Mzee Nyerere alifahamu kabisa kwamba nchi haina fedha za kigeni, lakini kwanini aliendelea kukomaa ?

Hivi unadhani Mao Zedong mbali na kukosea kwenye Uchumi, unadhani sehemu nyingine muhimu hakupatia?
===============================================================================

Mwisho kabisa, UCHUMI ndiyo moyo wa taifa lolote lile. Ukikosea UCHUMI hata uwe na jeshi imara na taifa lenye wazalendo mambo lazima yaharibike tu. Urusi alipatia mengine, alipokosea Uchumi tu ikala kwake. Uchina anakosea mengi sana, kisiasa bado lile ni taifa la kidikteta lakini wamepatia sana UCHUMI. Watu wanahitaji sana maendeleo kuliko porojo za kisiasa za demokrasia au utawala bora. Ndiyo maana mataifa kama Saudi Arabia, UAE na Qatar hayahangaiki kabisa na hizo porojo kwasababu wanafahamu fika ukishawapa watu maendeleo maneno hupungua.

Sasa nikuombe unisaidie labda kuna kitu ambacho wewe unakifahamu, mimi sikifahamu naweza kujifunza:
1. Unadhani Mzee Nyerere alifanikiwa kwenye Uchumi? (Kama jibu ni NDIYO nieleze alifanikiwa kivipi ?)
2. Nini kilipelekea matatizo ya uchumi nchini Tanzania kuanzia miaka ya 1975-1985 ?
3. Unadhani Tanzania ingeendelea kufanikiwa kwa kukomaa na mfumo wa Kijamaa?
4. Kwanini miaka ya 1980-1985 ilikuwa imejaa changamoto kubwa za kiusalama kuliko wakati wowote ule ?
5. Kwanini sera alizozikataa miaka ya 1970's alikuja kuzikubali miaka ya 1984 wakati anaondoka madarakani?
 
China ujamaa aliendelea nao mpaka sasa anaendelea nao.

Mabadiliko pekee uchina waliyo amua kuchukua ni kufanya yale yanayowezekana kufanywa ndani ya ujamaa na kupuuzia yale yasiyowezekana they decide to be more realistic.

China iliamua kwa muda waliopo na hali waliyokuwa nayo kulikuwa hakuna ulazima wa wao kukeep kuwa na mawazo ya kuujenga ukomunisti kwenye fikra tu na kutembea nao vichwani ili walazimu wao kutoka kuwa viongozi wa kifikra zaidi na kuamua kuwa viongozi watendaji zaidi kwa yale yatakayo onesha muelekeo wa wao kujenga nchi ya kikomunisti basi wao watayafuata na yale yatakayo onesha muelekeo hasi haraka wataachana nayo.

China imejifunza economic models mbalimbali kuanzia miaka yake ya mwanzo ya uhuru ili tumia Soviet economic model baada ya kufeli miaka ya 50 wakaachana nayo, China imejifunza Japan, Singapore,Taiwan, Hongkong e.t.c China imejaribu kukopa idea mbalimbali za kiuchumi katika nchi mbalimbali na kuzifanyia utekelezaji utakao endana na matakwa ya jamii ya kikomunisti ya Uchina.

Serikali ya China kuweza kuchukua hatua za haraka za mabadiliko ya kiuchumi ni miongoni mwa vitu vilivyo wanusuru na mpaka sasa vinawanusuru. toka kipindi cha mwenyekiti Mao pale sera zinapofeli haraka sana wanachukua mabadiliko Deng ameplay important role ya mabadiliko ya sera za kiuchumi wa China toka mwanzo baada ya uhuru kipindi akiwa Waziri wa fedha.

Kuhusu mabadiliko ya kisera ya China ya miaka ya 70 sio kwamba hayakuwa na matatizo wala hayakuleta shida.

Moja ya matatizo maarufu ya mabadiliko ya sera ya miaka ya 70 yaliyofanywa na Deng ni maandamano ya Tianmen Square.

Maandamano ya Tianmen Square ni matokeo ya sera kuleta matokeo makubwa hasi katika jamii ya kichina katika wakulima, umiliki wa ardhi, mfumuko mkubwa wa bei katika historia ya China, rushwa kutamalaki kila kona China hasa katika serikali, ongezeko kubwa la kati ya watu wasio nacho na wenye nacho na mengine mengi.

Wananchi wa China waliingiwa na hasira mpaka kutishia kuangusha serikali ya Beijing uzuri ni hatua za haraka zilichukuliwa na mabadiliko kufanyika bila hivyo China hii nayo inge collapse kama Soviet kwenye hiyo hiyo miaka ya 80-90
 
haya mambo uliyoandika hapa yanafikirisha sana!
Ukiwaaliza kwanini miaka ya 1980's ilijaa changamoto nyingi za usalama kuliko wakati wowote ule hawatoi majibu.

Ukweli mchungu ni kwamba hata nchi iwe imara vipi, mtikisiko wa uchumi ukitoka lazima nchi iparanganyika kwa haraka. Utakuta changamoto nyingi za usalama zinaanza kutokea. Uhalifu unaongezeka, biashara haramu inaongezeka, mauaji yanaongezeka, auasi unaweza kutokea au hata mapinduzi yanaweza kutoka. Katika tasnia ya usalama wanasema: There is a direct link between Economic Stability and Political Stability.

Bahati mbaya hili wengi linawapita kwasababu tunapenda mambo marahisi tu. Watanzania kiasili ni watu watulivu, lakini ukiona hadi wameamua kufanya uzandiki wa kumuua rasi, kutoka kujitoa kwenye muungano, kutaka kufanya mapinduzi ndani ya muda mfupi basi inabidi ukae chini. Mbona wakati wananyang'anywa nyumba zao hawakufanya lolote, au mbona wakati wanahamishiwa kwenye vijiji kinguvu hakufanya lolote. Ila kuanzia mwaka 1980 hadi 1986 walianza kufanya mambo ya ajabu hadi wakachoma Benki Kuu. Hebu nikupe mifano mizuri kihistoria:

1. UFARANSA: Nchi ilikuwa ni ya wakatoliki, lakini Mfalme Louis XIV alipopigana vita na Uingereza kugombania Makoloni nchini Marekani mwaka 1754-1763, alitumia rasilimali nyingi mno na nchi ikafilisika. Maisha yakaanza kuwa magumu kwasababu Ufaransa ilipoteza makoloni yenye utajiri mwingi kwa Muingereza. Maisha yalivyoanza kuwa magumu mbegu ya chuki ikaanza nchini Ufaransa hadi kupelekea mapinduzi ya mwaka 1789 ambayo yalimuua mjuu wake Louis XVI. Ambacho kinashangaza ni kwamba nchi iliyokuwa ya Kikatoliki zaidi duniani kote, iliamua kulibomoa kabisa kanisa Katoliki na kuua mapadri zaidi ya 30,000 kwa kuwapiga risasi na kuwanyonga. Vijana waliokulia mafundisho na kupewa kumonyo kama Maurice De Talleyland walijiunga na mapinduzi.

Chanzo kilikuwa kikibwa kilikuwa ni uongozi kuvuruga uchumi na kugoma kubadilika.

2. URUSI: Nchi ilikuwa ni imara chini ya Familia ya Ramanov. Wahuni walipojaribu kufanya mapinduzi ilishindikana. Miaka zaidi ya 200 mapinduzi hayafanikiwi nchini Urusi. Kufika mwaka 1914-1917, iliwezekana kwasababu Mfalme Nicholas Ramanov II aliingiza nchi kwenye vita ya kijinga na watu wengi wakafa na nchi ikafikilisika. Wakomunisti walipindua nchi kirahisi mno na kumuaa mfalme na familia yake. Wakaenda mbali na kubomoa makanisa zaidi ya 100,000 na kuua maelfu ya wakristo. Chanzo kikubwa ni kwamba Uchumi wa nchi ulikuwa umedorora na watu walikuwa kwenye lindi kubwa la umasikini.

3. MAREKANI: Miaka yote kabla ya mapinduzi ya mwaka 1776, makoloni ya Marekani yalikuwa yanakubali kuwa sehemu ya Ufalme wa Uingereza. Matatizo yalianza pale Mfalme George III (The Mad King) alipoanza kucheza na uchumi kiasi cha kuwaumiza watu wanaishi kwenye makoloni. Alianza kuuza chai kutoka Uchina kwenye makoloni ya Marekani bila kinyume cha utaratibu wa kodi. Akaanzisha utaratibu mwingine wa kodi kuwaumiza Wamarekani, mwishoni kikazaliwa kitu kinachoitwa The Boston Tea Party, ambacho kilichochea vita za kimapinduzi nchini Marekani kuuondoa utawala wa kinyonyaji.

Marekani tena, kuna kitu wanaficha pamoja na demokrasia yao yote, baada ya mtikisiko wa uchumi wa mwaka 1938 (The Great Depression), wanajeshi , matajiri na wamarekani wengine walijikusanya ili wampindue Raisi Franklin Delano Roosevelt. Chanzo ni kwamba alionekana kutaka kuleta sera zinazofanana na ujamaa. Walimuita General Smedley Butler ili afanya hiyo kazi, na akakataa na kwenda kutoa siri. Mambo yakamalizwa kiutu uzima. Sasa nchi ya Marekani ambayo inasifika kwa mfumo bora wa uongozi ilikutwa na haya sembuse Tanzania?

Mifano iko mingi sana na inaendana. Nchi unakuta ina watu watulivu lakini wakiwa na njaa halafu wafahamu chanzo ni serikali mambo lazima yaharibike. Mara zote uvumilivu huwa unawashinda watu.​
 
Umemezeshwa sumu mbaya sana madrasa.Pole sana.
Mwenyeheri Nyerere aliwapenda watanzania.Hakuuuza chochote kwa maarabu ambayo ni ndugu zako katika imaan.Cha zaidi hakuiba wala kuifanya ikulu kuwa pango la walowezi.Legacy yake inaishi
 
Sasa mbona vyuo vyetu vinazalisha machawa badala ya wasomi wanaojielewa
 
Duniani kote, Marxist Philosophy ina mambo makuu mawili: THE BASE vs THE SUPERSTRUCTURE.

The Base
is the foundation of a society, the material, the economy, the major means of production. While,
The Superstructure are the institutions established to exploit the base. These institutions could cultural, political, social and economic. This is how Karl Marx and other communists perceived the entire fabric of capitalist society.

Sasa popote pale duniani Ujamaa huwa unagawanywa kwenye makundi mawili, moja ni lile la SIASA ili kushughulika na The Superstructure, pili ni UCHUMI ili kushughulika na The Base. Ndiyo maana AZIMIO LA ARUSHA likikuwa na sehemu kuu mbili. Sehemu ya kwanza ikiwa ni SIASA, sehemu ya pili ikiwa ni UCHUMI. Hili lilikuwepo Uchina hata ukisoma Mao's RED BOOK utaona nachokisema. Urusi nako ilikuwa hivi, na hii ndiyo falsafa ya Ujamaa. Tanzania kuanzia mwaka 1986 tulibadilisha sehemu ya UCHUMI, na mwaka 1991 tukabadilisha sehemu ya SIASA kupitia AZIMIO LA ZANZIBAR.

Sehemu ya SIASA ya AZIMIO LA ARUSHA ndiyo ilikuwa imejaa Maadili na Miiko ya Uongozi, CCM wakaamua kufuta kabisa ili mtu asiwabane. Mwaka 2014, nikiwa sehemu na Marehemu Balozi Mzee Mahiga alisema kwamba AZIMIO LA ARUSHA, lingeendelea kubaki, tulichotakiwa kufanya ni kubadilisha sehemu ya UCHUMI na SIASA tungeacha kama ilivyokuwa. UCHINA wanafanya hivyo mpaka leo, USSR walibadilisha vyote na nchi ikaanguka.

Uchina walichofanya ni kufanya mabadiliko kwenye UCHUMI na siyo SIASA. Hivyo wameruhusu mfumo wa masoko na umiliki wa mali (Market Forces and Ownership of Property), lakini mgawanyo wa pato la taifa bado uko kijamaa. Hivyo tunasema, In China the ownership of Property is capitalist and Market Oriented, while the distribution of wealth is still Communist. Hivyo, the Welfare State is still robust and active in China.​
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…