The Boy Wonder
Kuhusu sera zake kisiasa hasa unachokiita kuua demokrasia.
Niseme kwanza, unakosea sana kutazama mapungufu ya sera za Nyerere bila kuangalia lengo la sera hizo na vipi zilifanikiwa.
Ninaamini fika unafahamu kuwa wakati Tanganyika inapata uhuru wake, kama zilivyokuwa nchi nyingi za kiafrika, zilikuwa zimetawaliwa sana na Ethnic & Racial divisions ambazo bila kuwa addressed zingeathiri sana Umoja wa kitaifa, na pengine leo hii sisi Tanzania tusingekuwa tofuati kabisa na Congo.
Nyerere mwenyewe, mwaka 1958, alihojiwa na Sunday Times ya Uingereza akisema kuwa; Miaka 15 baada ya uhuru, itakuwa chini ya utawala wa Chama kimoja ili kwanza kujenga amani na umoja wa taifa. Hufahamu kuwa Chama cha Zuberi Mtemvu—upinzani—kilindwa kwa misingi ya kibaguzi? Hufahamu kuwa nyakati hizo za ukoloni makabala ndio ilikuwa existing social understanding ya utawala. Kwa misingi ya demokrasia ya vyama vingi, unadhani kuwa kungezuilika nini Chief Kidaha kuwa na chama chake chenye base ya wasukuma? Au Chagga Democratic Party unadhani ingeshindwa vipi kupata affiliation kubwa ya jamii ya wachagga nchini? Hufahamu kuwa moja ya sababu ya kuwepo kwa Mutiny ya 1964 ni wanajeshi wale kutoridhishwa na sera za race-inclusivity za Nyerere? Au tulihitaji tufikie hali ya Congo ya mwaka 1960 kwa ukamilifu ndio Uongozi wa TANU utambue kuwa kuna hatari ya kiusalama ya hizo divisions za kikabila?—Ninaamini fika unayajua yote haya. Ndio sababu, Nyerere aliona kuwa Demokrasia ya Chama Kimoja ilifaa kwa nyakati zile. Lengo la Sera hizo za kujenga umoja wa kitaifa zilifanikiwa au la? Majibu unayo mwenyewe. So, Nyerere hakuua demokrasia, bali alikuwa na Demokrasia ya Chama kimoja ambayo iliendana na mazingira ya wakati ule na ilifaa—haimaanishi kuwa haikuwa na mapungufu so as liberal democracy.
On UDHR.
Mkataba wowote wa kimataifa, ni lazima taifa lijiridhishe na mazingira yake ndio liuridhie. Mataifa mengi yameridhia treaties chache kati ya zote 9 zilizopo kwenye Declaration. It doesn't mean hayajali haki za binadamu au hazina mechanism za kuguarantee haki hizo kwenye mifumo yao ya ndani. Hao unaowaembrace kuwa sio makatili, ndio vinara wa mauji dunia hii—US, UK, France and yet wameridhia UDHR. Wakati Uingereza anafanya mauji Kenya, alikuaa ameridhia UDHR.