Mwanamke mwenye akili hawezi kupambana achukue mali za mwanamke mwenzake aliyezichuma. Atapambana atafute za kwake na huyo anayemwita mume.
Kuna familia moja naifahamu mama na baba walikuwa na mali nyingi sana na watoto tayari walikuwa wakubwa. Mama akaja akafariki baada ya kufariki miaka ikapita yule baba akawa anahitaji kuoa. Lkn kabla hajao akakaa na watoto wake wakatafuta mwanasheria mali zote zilizochumwa wakagawana 50 kwa 50 kwa hiyo ile hamsini wakarithi watoto hamsini ikabaki kwa baba.
Baadae ndo akaja kuoa na kuanza kutafuta upya mali na yule mwanamke mpya.
Kwa hiyo familia inaendelea bila mgororo wala vita.
Wanawake tuache tamaaa. Na watu wahurumiwe pale kweli panapohitaji kuhurumiwa.
Sent using
Jamii Forums mobile app