Wajawazito kwenye Daladala, kwanini wanawake hawapishani kwenye siti?

Wajawazito kwenye Daladala, kwanini wanawake hawapishani kwenye siti?

Kwenye daladala ni ngumu sana kuona mwanamke anampisha siti mwanamke mwenzake hatakama ana ujauzito mkubwa kiasi gani hampishi.

Utashangaa mwanaume yuko nyuma kabisaa anampisha siti akae lakini mwanamke wa karibu yake anakausha.

Shida ni nini?
Uwongo
 
Karma is real nae alipokuwa hana ujauzito alikuwa akipisha watu katika seat? Ila mimba sitilii maanani wenye watoto ndo wanapaswa kupishwa na huwa wanapishwa, mimi mwanaume ila mwenye amebeba mtoto nampa kipaumbele sana
 
Karma is real nae alipokuwa hana ujauzito alikuwa akipisha watu katika seat? Ila mimba sitilii maanani wenye watoto ndo wanapaswa kupishwa na huwa wanapishwa, mi mwanaume ila mwenye amebeba mtot nampa kipaumbele sana
Nadhani wanawake wao huwa wanaamini wameumbwa kufanyiwa vitu na sio wao kufanya. Hii utaiona kila mahali mfano hata mwanamke akisimama barabarani anategemea ukipita umpe lifti, ila kamwe yeye akiwa anaendesha gari hawezi kusimama akupe lifti mwanaume.
 
Shida inakuwa mwanaume hata akisimama hana cha kupoteza, ataenda kubembea kwenye mizigo iliofungashwa na wanawake na kufaidi uumbaji wa Mungu 😜
🤣 🤣 🤣 🤣 🤣 kazi kweli kweli.
 
Wanaume wa dar hawapishi mjamzito.washamba mno.kuna siku nilikuwa naenda clinic nikapanda daladala
Nilikuwa sitaki kukaa hata .kwanza ni mita chache tu
Vijana wadogo tu wamekaa hapo wanaona kabisa tumbo wanajikausha.konda akawachamba wee ndo kunipisha ila nikawaambia me sitaki kuketi .ila nilishangaa mno.hata kwenye magroup ya mama vija wengi huwa wanalalamika
 
Binafsi hata mimi nishaacha kupisha watu kwenye siti. Kwanza washafanya ni wajibu halafu hawana shukrani.

Me nigeuze na gari wewe uje nikupishe kiboya tu.

Wengine muda wa kusafiri ndio muda wa kuchambua na kuweka mikeka.
 
Back
Top Bottom