DOKEZO Wajawazito wanasita kwenda Kituo cha Afya Nindo - Shinyanga Vijijini sababu wanatozwa hela

DOKEZO Wajawazito wanasita kwenda Kituo cha Afya Nindo - Shinyanga Vijijini sababu wanatozwa hela

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
A

Anonymous

Guest
Ninaishi Iselemagazi, Wilaya ya Shinyanga Vijijini, na ningependa kuwasilisha malalamiko kuhusu huduma zinazotolewa katika Kituo cha Afya Nindo.

Katika kituo hicho, wanawake wajawazito wanaoanza huduma za kliniki hutakiwa kulipa shilingi 10,000, na wakati mwingine fedha hizo hukusanywa bila kutolewa risiti au maelezo rasmi ya malipo husika. Hali hii imekuwa kikwazo kwa baadhi ya wajawazito kushindwa kuanza kliniki kwa wakati kutokana na changamoto za kifedha.

Aidha, wanawake wanapofika kujifungua huombwa tena kulipa shilingi 10,000 kwa madai ya gharama za vifaa vya kujifungulia. Utaratibu huu umeongeza mzigo wa gharama kwa wananchi na kuzua malalamiko miongoni mwa wakazi wa eneo hilo.

Tunaiomba mamlaka husika kufuatilia suala hili na kutoa ufafanuzi ili kuhakikisha huduma za afya ya uzazi zinapatikana kwa haki, uwazi na kwa kuzingatia taratibu na miongozo ya serikali.
 
Poleni kwa wizi wa machomacho na big up kwa kupaza sauti. Sauti imesikika vyema.
 
Kero yangu, mimi ni mkazi wa Iselamagazi iliyoko Shinyanga DC (Shinyanga Vijijini) katika Kituo chetu cha Afya Nindo wakinamama wajawazito wanapoenda kuanza kliniki wanatozwa Shilingi 10,000 na wakati mwingine bila kupewa risiti.

Hiyo imesababisha baadhi yao kutoanza kliniki kwa kukosa hela lakini pia kila mama mjamzito anapoenda kujifungua huombwa shilingi 10,000 ya mipira ya kujifungulia, huduma zimekuwa ni zagharama sana.
 
Nasikitika kusema kwamba katika Kituo cha Afya Nindo, wanawake wajawazito wanapofika kuanza kliniki wanatozwa ada ya kuanza kliniki, lakini hawapewi risiti rasmi. Badala yake, hupewa karatasi iliyoandikwa kuwa wamelipia.

Tunapohoji na kuomba risiti rasmi, kiongozi wa kituo hutoa majibu makali na wakati mwingine kutumia lugha isiyofaa, huku akiwaelekeza wanaodai risiti kwenda kupata huduma sehemu nyingine, hata katika hospitali ya wilaya.
 
Ndugu yangu alienda kuanza clinic ya ujauzito katika kituo cha afya Nindo kilichopo Iselamagazi Shinyanga DC alitozwa pesa shilling elfu 20 wakamuandikia kikaratasi kwamba Paid pasipo risiti. Alipohoji kuhusu risiti mganga mfawidhi alimfokea na kumpa maneno makali kwamba aende akapate huduma sehemu nyingine. Je huduma zetu za afya zimefikia huku? Gharama za hospital pasipo risiti hiyo ni haki?
 
Back
Top Bottom