JAMANI TULIENI KIDOGO MNISIKIE:
Japo natumia maandishi ila najua mnanisikia. Unapokuwa mtu mzima inamaanisha unakuwa na uwezo wa kuhandle situation yoyote na kufikia mwisho wenye manufaa kwako. Unapopata habari handle situation halafu utafute possibility kama ipo.
Hazina ya mjerumani kubaki nchini ilinifikisha hapa;
1.Story kuhusu meli ya MV LIEMBA kuzama katika ziwa Tanganyika. Mjerumani alikuwa anachukua Mali kutoka DRC kuja TZ kwakutumia meli ile na inasadikika meli ile ilizamishwa na hii iliyopo leo ni tela lake tu,na wajerumani walishaomba kuja kuichukua kwa ofa ya meli mbili mpya. POINT TO VIEW: je wajerumani walikuja kuchukua mali afrika na kuzipeleka kwao au kuzitawanya Tanganyika? Je kama hii MV LIEMBA iliyopo ilikuwa ni tela la ile iliyozamishwa ni kweli teknolojia ya usafiri wa majini ina mambo ya kuvutana kama barabarani mfano wa lori na tela lake?
2.Story ya kuacha mali zake kwa kukimbia vita. POINT TO VIEW. Tunajua mjerumani alipigana kumuondoa mwarabu Tanganyika,Je historia inasemaje kuhusu namna alivyoondoka mjerumani nchini Tanganyika? Je, Hakuondoka kwa baraza tu? Wataalamu wa historia mtuelezee kidogo hapa.
3. Mjerumani kupigwa na mrusi na kushindwa kuitawala dunia.POINT TO VIEW. Je, hizi sifa na uwezo mkubwa wa nanma hii juu kuficha malizake alipewa tu kutoka kusikojulikana ama ilikuwakuwaje maana ukisikiliza utagundua ni uchawi mkubwa sana sio wa kushindwa kupigana vita.
Hapo ndipo nilipofika mimi na kuhitimisha kuwa kitu kisicho na uthibitisho ni imani tu. Sijui upande wenu.
MAGUFULI4LIFE.