Mkuu, ni hatariii.....Ngoja nikupe kisa changu kilichonipata katika hizo pilika.
Kwanza nilivutiwa na jamaa fulani hivi tukiwa Mbeya huko wilaya XYZ,jamaa walifankkiwa kuopoa sanduku la dhahabu kwa Style hyhy ya kusaka Mali za wajerumani. Walikula bata sana na hadi muda huu ni malordilofa,yaani pesa bado wanayo.
Basi bhana,nikasafiri hadi wilaya kwa wajomba zangu baada ya kujifunza Code chache ambazo wajelumani walitumia kama alama na nikagundua hivi vitu nilivionaga kwa wajomba zangu nikiwa nachunga ng'ombe milimani.
Nilipofika kwa babu,nikanyoosha msituni kwenda kuhakiki kama zile alama kwenye miti,mawe na michoro kama ipo, bahati nzuri bhana nikavikuta kama vilivyo,wala havijaharibiwa sana na waharibifu wa mazingira. Nikashauriana na vijana wa pale tukaanza utaratbu wa kuchimba.
Huku tukiendelea kukutana na code na ninazisoma vizuri na kusonga mbele,baada ya siku 6 hatimaye tukalifikia sanduku bhana....!! Tulichokiona humo......mmamaye ,nikikumbuka huwa hata sijielewagi,maana ni hatari.
Tulikutana na marehemu mzungu humo.....ashamong'onyoka kawa unga tu,sijui walimtia nini hakuoza,kawa vumbi tu na mifupa, hilo vumbi likaingia vifuani, tulikohoa karibia ya kunya......!!!!
Aisee.....tulirudi nyumbani tukatengeezwa kienyehi ndio mambo yakawa sawa, lakini kuna mzee akasema mgetoa lile sanduku ndio mgekutana na mzigo wenyewe....!! Alinistua mbaya,lakini cha ajabu,nasema tena chaa ajabu niliporudi kule porini ile sehemu sijaikuta na wala sikuiona tena hadi leo, nilienda takribani mara 6 kwa siku tofauti lakini mpaka leo sipajui eti.....!!
Kuna sehemu tena nipo ugenini,nilikwenda kucheki shamba la kununua nimekutana na code tena za ajabu aisee.....!!! Sasa sijajua nini wameficha...!!
Kwanza nilikuta Mti mkubwa una mzizi upo nje,mzizi huo umetobolewa,nikaufuatilia kidogo nikakuta tobo la pili, nikaendelea kufukua nikakuta nikakuta tena mzizi umekunjwa kuelekea direction ya kusini,nikaendelea kuufuata, mbele ya huo mzizi kulikuwa na jiwe kubwa sana kama tani 30 hivi, nilipolizoom vizuri kabisa na kulichunguza,nikagundua kuwa huyo ni picha iliyojchongwa picha ya bundi...!!!! Nikafukuafukua kuzungua hilo hiwe nikakuta ramani aisee.....!!! Bahati mbaya sijui kijerumani .
Mzee nikaazimia kazi, tukaenda kwa mchawi wetu akasema kuna mzigo wa kufa jamaa....vizuri vyote ruby,gold na sapphire akasema zipo. Akatupa masharti tukaingia mzigoni...!!
Baba tumefungua ardhi huku tukifuata masharti makamanda tulikuwa 6, tuliikosea ramani kidogo tukajikuta kuna mwamba una ninginia juu yetu.
Tulichokifikia ni kwanza kuna vigae vya mawe vimefunika kitu tusichokijua hapo chini, pili kuna ukuta umejengwa kwa mawe ya kupondekezwa hapo chini shimoni...!!
Tuliogopa kupondwa na tulikuwa tumechoka sana,maana kazi ilikuwa ya ngumu na ilituchukua miezi 3,tukasema labda tusake katapila.
Sasa tumeliacha tu na tumeamua tulime tu kwanza lakini tukiwa na matumaini kwamba ipo siku.
Sasa najiuliza,au tutakuta marehemu mzungu tena au la ....nakaribisha wadau,kama unaweza kuleta Scaveta njoo tujaribu bahati.
Sent using
Jamii Forums mobile app