Wajerumani Walificha Mali Nyingi Kwenye Ardhi ya Tanzania

Wajerumani Walificha Mali Nyingi Kwenye Ardhi ya Tanzania

kila muafrika anaetumwa kuficha Mali ilikuwa lazima afie kule kule mafichoni.Wajerumani walikua wanamchukua muafrika mmoja halafu wanachukua kichwa cha chatu wanamuwekea mdomoni kisha wanafunika pamoja na Mali
Mtaalamu alisema kuna vito vya kutosha sana, tulipofiikia kuna vigaae vikubwa vimefunika na pembeni yake kuna ukuta wa mawe umejengwa,sasa kuna ngema juu imeninginia na kuna kiwe, inafaa lilipuliwe na litolewe.

Tulikutana na mauza uza kibao lakini tyliyashinda,kubwa ilikuwa nyoka wa kutisha wa kutosha, tuliambiwa hapana kumuuwa hata mmoja,mbinde ilikuwa kuwatoa humo shimoni.

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Vipi kuhusu maeneo ambayo kuna alama (handaki,misaraba, zege n.k)ziliwekwa na hao hao wajerumani zilikua za nini? Ninao ushahidi alikuja Padre mmoja mjerumani akaondoka na mzigo na wala hakuchimba umbali mkubwa ,walitumia jembe tu ilikuwa 2016
Ni nani aliyefanikiwa kuchimba na kupata hiyo hazina? Mkuu hii kitu nimeufuatilia kwa karibu sana zaidi ya miaka ishirini. Nilichokiandika nakifahamu fika. na ukweli ni wale wanaotaka utajiri kwa ganda la ndizi ndio wanafanya hii ishu au wanahamasisha wengine nao wafanye. Inauma sana lakini bahati mbaya ukishakolea inakuwa kama umelishwa uganga. No hazina ya Mjerumani full stop.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Vipi kuhusu maeneo ambayo kuna alama (handaki,misaraba, zege n.k)ziliwekwa na hao hao wajerumani zilikua za nini? Ninao ushahidi alikuja Padre mmoja mjerumani akaondoka na mzigo na wala hakuchimba umbali mkubwa ,walitumia jembe tu ilikuwa 2016

Sent using Jamii Forums mobile app
Hiyo ni kweli pia na Mm nineshuhudia kuna mzee mmoja kama wa miaka 89 au 90 alikuwa na ramani ya hazina kubwa sana iliyopo around Mwadui Shinyanga.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndugu zangu wanajamvi.
Nimekuwa katika utafiti wa mali kale na mambo ya asili kwa muda mrefu.
Katika utafiti wangu nimekuja kugundua wajerumani wameficha mali nyingi sana kawenye ardhi ya Tanzania.
View attachment 1022278

Wakati wa utawala wa wajerumani kulikuwa na fedha ambazo zilikuwa zikitumiaka.
Heller na Rupee zilikuwa zikitumiaka. Coin hizo zilikuwa na madini mengi sana tofauti na coin za sasa.
Kwa mfano 1 Heller kwa sasa inauzwa kwa $900 - $1000.
View attachment 1022271

View attachment 1022276

Kwenye vita vya kwanza vya dunia wajerumani walizichimbia hizo mali sehemu mbalimbali kwenye ardhi ya Tanzania kwa ustadi mkubwa.

Katika tafiti nilizozifanya mpaka hivi leo. Maeneo yafuatayo na mengine mengi ndiko zilipogichwa mali hizo. Inatakiwa kujua sasa ni eneo gani masanduku yenye mali yalichimbiwa:-

  1. Ikombe
  2. Mibirizi
  3. Kasanga
  4. Ilembule
  5. Rombo
  6. Nyakanazi
  7. Uvinza
  8. Mlalo
  9. Kisarawe
  10. Kazimzumbwi
  11. Kirondatal
  12. Tukuyu
  13. Leganga
  14. Igulwa
  15. Ushetu
  16. Mnazi
  17. Mikese
  18. Shume
  19. Lumbira
  20. Mbulu
  21. Nansio
  22. Sekenke
  23. Galula
  24. Liuli
  25. Manda
  26. Lushoto
Hizi ni sehemu kadhaa zinazohitajika utafiti wa kina ili kujua ni sehemu zipi mali hizo zilifichwa.

Asanteni
Uko sahihi mkuu,niliwahi kukaa Uvinza miaka ya nyuma sana,hizi hela za zamani zilikuwa nyingi sana...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu Venus Star hio kitu habari yake ni kubwa sana. Niliwahi kushiriki katika moja ya mapango ambayo inasemekana kuna mali za wajeru, Rafiki yangu mmoja alinialika kwenda walau siku moja kuona nini wanafanya. Ilikuwa ni kazi ya siku 5 iliowashirikisha wachungaji na masheikh….. muziki wake si wamchezo mkuu, hasara kubwa na mali haikupatiana. Acha kabisa baba
una maanisha mazingaombwe yalikuwa kibao?
 
Nina ankal wangu anaishi vanga aliwahi kunambia mwaka jana mambo haya, kuna mercury, hizi sarafu, stove, pasi, jambia na sufuria alikua na saraf imeandikwa heller na nyingine doa kuna moja ni kubwa ndani ina kitu kama kidude ukiitikisa ambiwa hilo jambia ukilichomeka chini lazama naona anidanganya hivi hivi na ukizamia huko ni kupoteza muda na pesa tu naskia wakitaka kutafta hizo hazina lazima wakatambike na wanakutana na mauza uza si ya nchi hii
Neno "ambiwa" hili nimelisikia sana Tanga, wanawake wakitanga wanaoenda sana kulisema hili neno

.
 
Back
Top Bottom