Wajerumani Walificha Mali Nyingi Kwenye Ardhi ya Tanzania

Wajerumani Walificha Mali Nyingi Kwenye Ardhi ya Tanzania

Kuna mmoja kyela eneo lake inasemekana chini kuna pango huko masanduku na gari moja lipo wazungu wakaomba wampe gari na wamjengee nyumba nzuri ilo eneo wapewe wao jamaa akakataa akasema atachimba yeye..

kitu cha kushangaza kila lipokua anachimba vile vitu vinashuka chini... Akatengeneza mashimo makubwa matatu na maji kwake bila mafanikio

Hivyo vitu vya kishirikina hatari

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna mmoja kyela eneo lake inasemekana chini kuna pango huko masanduku na gari moja lipo wazungu wakaomba wampe gari na wamjengee nyumba nzuri ilo eneo wapewe wao jamaa akakataa akasema atachimba yeye..

kitu cha kushangaza kila lipokua anachimba vile vitu vinashuka chini... Akatengeneza mashimo makubwa matatu na maji kwake bila mafanikio

Hivyo vitu vya kishirikina hatari

Sent using Jamii Forums mobile app
Kyela sehemu gani mkuu?
 
Nitakutafuta
Mkuu, ni hatariii.....Ngoja nikupe kisa changu kilichonipata katika hizo pilika.

Kwanza nilivutiwa na jamaa fulani hivi tukiwa Mbeya huko wilaya XYZ,jamaa walifankkiwa kuopoa sanduku la dhahabu kwa Style hyhy ya kusaka Mali za wajerumani. Walikula bata sana na hadi muda huu ni malordilofa,yaani pesa bado wanayo.

Basi bhana,nikasafiri hadi wilaya kwa wajomba zangu baada ya kujifunza Code chache ambazo wajelumani walitumia kama alama na nikagundua hivi vitu nilivionaga kwa wajomba zangu nikiwa nachunga ng'ombe milimani.

Nilipofika kwa babu,nikanyoosha msituni kwenda kuhakiki kama zile alama kwenye miti,mawe na michoro kama ipo, bahati nzuri bhana nikavikuta kama vilivyo,wala havijaharibiwa sana na waharibifu wa mazingira. Nikashauriana na vijana wa pale tukaanza utaratbu wa kuchimba.

Huku tukiendelea kukutana na code na ninazisoma vizuri na kusonga mbele,baada ya siku 6 hatimaye tukalifikia sanduku bhana....!! Tulichokiona humo......mmamaye ,nikikumbuka huwa hata sijielewagi,maana ni hatari.

Tulikutana na marehemu mzungu humo.....ashamong'onyoka kawa unga tu,sijui walimtia nini hakuoza,kawa vumbi tu na mifupa, hilo vumbi likaingia vifuani, tulikohoa karibia ya kunya......!!!!

Aisee.....tulirudi nyumbani tukatengeezwa kienyehi ndio mambo yakawa sawa, lakini kuna mzee akasema mgetoa lile sanduku ndio mgekutana na mzigo wenyewe....!! Alinistua mbaya,lakini cha ajabu,nasema tena chaa ajabu niliporudi kule porini ile sehemu sijaikuta na wala sikuiona tena hadi leo, nilienda takribani mara 6 kwa siku tofauti lakini mpaka leo sipajui eti.....!!

Kuna sehemu tena nipo ugenini,nilikwenda kucheki shamba la kununua nimekutana na code tena za ajabu aisee.....!!! Sasa sijajua nini wameficha...!!

Kwanza nilikuta Mti mkubwa una mzizi upo nje,mzizi huo umetobolewa,nikaufuatilia kidogo nikakuta tobo la pili, nikaendelea kufukua nikakuta nikakuta tena mzizi umekunjwa kuelekea direction ya kusini,nikaendelea kuufuata, mbele ya huo mzizi kulikuwa na jiwe kubwa sana kama tani 30 hivi, nilipolizoom vizuri kabisa na kulichunguza,nikagundua kuwa huyo ni picha iliyojchongwa picha ya bundi...!!!! Nikafukuafukua kuzungua hilo hiwe nikakuta ramani aisee.....!!! Bahati mbaya sijui kijerumani .

Mzee nikaazimia kazi, tukaenda kwa mchawi wetu akasema kuna mzigo wa kufa jamaa....vizuri vyote ruby,gold na sapphire akasema zipo. Akatupa masharti tukaingia mzigoni...!!

Baba tumefungua ardhi huku tukifuata masharti makamanda tulikuwa 6, tuliikosea ramani kidogo tukajikuta kuna mwamba una ninginia juu yetu.

Tulichokifikia ni kwanza kuna vigae vya mawe vimefunika kitu tusichokijua hapo chini, pili kuna ukuta umejengwa kwa mawe ya kupondekezwa hapo chini shimoni...!!

Tuliogopa kupondwa na tulikuwa tumechoka sana,maana kazi ilikuwa ya ngumu na ilituchukua miezi 3,tukasema labda tusake katapila.


Sasa tumeliacha tu na tumeamua tulime tu kwanza lakini tukiwa na matumaini kwamba ipo siku.
Sasa najiuliza,au tutakuta marehemu mzungu tena au la ....nakaribisha wadau,kama unaweza kuleta Scaveta njoo tujaribu bahati.





Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huu ni uvumi usio na ukweli wowote. Binafsi nimeshuhudia baadhi ya marafiki zangu wakifilisika kutokamna na huu upuuzi. kuna mmoja alifukuzwa kazi yake ya Jeshi kwa kuwa alikuwa bise kutafuta hazina ya kijeruman. Haingii akilini mjerumani pamoja na level ya maendeleo aliyoifikia eti achimbie "hazina" chini. tena atafute "majini na vinyamkela" vya kulinda. Kama yeye alifukia kwa nini asije tu wakati huu kuifukua hazina yake? Watch out mtawapa waganga fedha za bure, mtawalipa watu wa kuchimba fedha za bure. Tafadhali ukiona jamaa yako anaota hizi ndoto mzindue hata kwa kumpiga kofi atakushukuru kesho kutwa.
Mkuu hii kitu ni real, Mjerumani kaacha vitu vingi sana ardhini na wajukuu huwa wanarudi na Ramani na kuvichomoa, Nimeishi mazingira ambayo yana code zao kuonesha kuwa vitu vipo, Ata chuo cha sheria lushoto, nimesikia Nyerere alikijenga kwa maana kuwa Pasichimbwe mana chini kuna mzigo heavy sana
 
Mtaalamu alisema kuna vito vya kutosha sana, tulipofiikia kuna vigaae vikubwa vimefunika na pembeni yake kuna ukuta wa mawe umejengwa,sasa kuna ngema juu imeninginia na kuna kiwe, inafaa lilipuliwe na litolewe.

Tulikutana na mauza uza kibao lakini tyliyashinda,kubwa ilikuwa nyoka wa kutisha wa kutosha, tuliambiwa hapana kumuuwa hata mmoja,mbinde ilikuwa kuwatoa humo shimoni.
Usijari,hilo si swala la kuogopa

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
kuna ugumu fulani wa kupata hizo mali kwasababu maeneo ambayo wajurumani walificha hizo mali yamekuwa ni makazi ya kudumu ya majini na majoka makubwa ya kutisha.

ili kupata hizo mali inabidi ujizatiti kweli kweli. vinginevyo utaishia kupata ukichaa au kufa kifo cha ajabu.
 
Mkuu hii kitu ni real, Mjerumani kaacha vitu vingi sana ardhini na wajukuu huwa wanarudi na Ramani na kuvichomoa, Nimeishi mazingira ambayo yana code zao kuonesha kuwa vitu vipo, Ata chuo cha sheria lushoto, nimesikia Nyerere alikijenga kwa maana kuwa Pasichimbwe mana chini kuna mzigo heavy sana

Ni nani aliyefanikiwa kuchimba na kupata hiyo hazina? Mkuu hii kitu nimeufuatilia kwa karibu sana zaidi ya miaka ishirini. Nilichokiandika nakifahamu fika. na ukweli ni wale wanaotaka utajiri kwa ganda la ndizi ndio wanafanya hii ishu au wanahamasisha wengine nao wafanye. Inauma sana lakini bahati mbaya ukishakolea inakuwa kama umelishwa uganga.

No hazina ya Mjerumani full stop.
 
Back
Top Bottom