Wajerumani Walificha Mali Nyingi Kwenye Ardhi ya Tanzania

Kubali kwa hili ndugu wewe ni mbumbumbu, mambo haya yapo,na wenye bahati zao wanatusua,mie nimeona kwa macho yangu, na mwisho ilikuwa ni singida, bibi kizee aliuza pasi kwa Muizraeli, alikuja na helicopter akachukua pasi yake na akaondoka na ajuza huyo na mjukuu wake,japo walipewa pesa kiduchu sana, mil 30 na ushee hivi.

Wapo wanaochemka kutokana na mauzauza hayo,wengine wanakutana na maiti na wengine wachache pia wanabahatika. Utajiri baba unanjia nyingi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Dah sasa hyo heller ina Ounce ngapi hadi kugonga Usd 900 ndugu,? kifupi mapesa ya kale sishauri mtu kutafuta kuwa yatamtoa zaidi ya kumtia mtu umasikini wa kutupwa
 
Biashara hizi ni za kitapeli sana, sio za kujaribu kufanya
 
Nakielewa ulichoandika , ni mali iliyofichwa kwa nguvu ya giza kubwa mno .

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ukisikia watu walioishi siku nyingi wanakueleza jambo ni vyema kutafakari. Sisi ambao Mungu ametujalia kuona haya mambo tumejasikia hii kitu mara nyingi inatengezwa na pande mbili ambazo ziko pamoja. Moja inasema tunatafuta Rupia ya Kijerumani sijui yenye tundu tunanuna labda kwa Million 100.

Sasa afadhali sasa tunajua huko ebay na collector wengine ni $900 ambazo ni sawa na takriban 2m. Sasa inatangazwa demand ila huyo anayetoa hizo m 100 anakuwa ajawahi kuonekana ila unakuwa unasikia tuu kuna jamaa kuna jamaa ukiforce kuonana na mtu anayetaka kununua mzigo huonyeshi ila unaambiwa wewe tafuta ukipata hela iko na ukiangalia wazee walioaminishwa au wanaokueleza kama huna jicho la tatu lazima uingie kingi. Sasa wewe ukianza kuifanyia kazi anakuja mwingine kwenye team anakueleza kuna mtu wapi huko ana mzigo yeye labda anataka 30m ukichukua na yule aliyekueleza kuangalia Genuity anakuambia mzigo ndio huo sasa wewe nunua mzigo tumpeleke jamaa tupate 70 yetu ukilongwa huoni anayenunua wala nini.

Ndio maana waliona jua siku nyingi wanakuambia huu mchezo ulianza toka 70 huko ni moja ya utapeli wa siku nyingi. Ila uzuri siku hizi kuna taarifa za wazi mtu akitapeliwa kiihivyo watu wanashangaa ila inatokana mara nyingi na tamaa za haraka haraka za mali
 
Tena hata hiyo 30m uliyolipa unaporwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…