na watu wengi wanaofatilia hizi mali za wajerumani, wanaishia kuwa kama machizi, sijui wanakosea masharti?? na wakirudi wanakuambia hali ngumu sanaa!! wachache wamefanikiwa!!
......
Barjun hizi Pasi zenyewe zikoje?? maana kuna jamaa huko geita ,mfuasi mzuri sanaa wa kutafuta hizi mali,ndugu wameshauri mno,lakini jamaa mbishi, katumia almost 10 years ,searching for HAZINA YA MJERUMANI!! one day alirudi na Pasi, ndo kama wadau walivyochangia hapo juu, ukiipata hiyo mali wanunuzi wote wanayeyuka,anakumbia flani ndo ananunua, ukimfata naye anasema flani alinielekeza,mwishowe pasi ikakosa mteja. Sasa sifa za hii pasi, ni model ya pasi za mkaa, ila sasa yenyewe haihitaji huo mkaa wa moto, yenyewe inanyoosha nguo automatically bila kuweka/kutia mkaa wa moto, Kinachotakiwa ni wewe tu uiongoze/uishikilie upigapo pasi. Maajabu mengine ya hii pasi ni kuwa inahama, leo ukiiacha sebuleni kesho unaikuta chumbani, siku nyingine unaikuta jikoni. ukihitaji kuitumia yaani shwari kabisa unanyoosha nguo. Balaa lingine ya hii pasi ni kuwa ilianza kuua(kwa mujibu ya wataalamu wa jadi) kila baada ya miezi kadhaa mwanafamilia anafariki, ndani ya miezi 10 tokea pasi iwepo nyumbani walifariki watoto wawili na mtu mzima mmoja!! mtaalamu wa jadi(mganga) alipofuatwa ,akasema ile pasi aliyoileta ndugu yenu ndo sababu ya vifo!! hivyo kikao cha familia kikaitishwa ,Jamaa akaamuliwa na wazee airudshe hiyo pasi alikoitoa, Jamaa akatii, akasafiri kurudi kwenye hizo area zenye code walikoichimbua hiyo pasi, akairudsha, Akarudi hom, sasa jamaa akili zake ni kama zimeyumba hivi, wanafamilia wakampatia mashamba alime, na aoe,akapigwa marufuku na wazee ,asifuatlie hazina tena!!!
●●●●●●●●
Katika stori, kujionea pia, watu watafuta mali hizi, wale ambao wana ajira za kudumu,ama wana pesa zao tayari, wakiwa wanatafuta hazina hizi HAWAHARIBIKIWI/AKILI ZAO HAZIYUMBI/HAWAWEHUKI , lakini ambao hawana pesa,hawana plan B za maisha, hawana vipato vingne, Wakirudi toka kwenye hizo coded Areas huwa wamewehuka ,au akili zao si sawa na walizoondoka nazo. lkn mabwana wenye pesa hapo juu,hata kama hakurudi na chochote still anakuwa yuko mentally fit,
,I don't know the mechanism behind the scene!!!