#COVID19 Wajinga wameibuka na hoja kwamba waliochomwa jana sio chanjo ni maji!

#COVID19 Wajinga wameibuka na hoja kwamba waliochomwa jana sio chanjo ni maji!

ngebe

JF-Expert Member
Joined
Jun 8, 2020
Posts
1,789
Reaction score
5,117
Hakika Mzee wetu Lowassa alikua sahihi sana kisema kipaumbele chake ni ELIMU, ELIMU, ELIMU

Rais Samia unakazi sana kuongoza vichwa vya namna hii.

Mtu unamuuliza nipe sababu za kukataa chanjo anakwambia mbona chanjo ya malaria na UKIMWI wazungu bado hawajaigundua, hivi hizi ni akili za kawaida kweli au kuna tatizo?

Maana kama ni ujinga basi Taifa hili ujinga ni wa hali ya juu sana, Serikali naomba iwekeze zaidi kwenye elimu,

Hivi kipindi ebora Imepamba moto Congo, chanjo yake siilitengenezwa faster, chanjo siilileta majibu chanya mpaka sasa hakuna Ebora, Waliochanjwa Ebora mlisikia wamekuabmazombi? Alietemgeneza chanjo ya Ebora ni nani? si mzungu huyohuyo?

Unaacha kuamini wataalamu wa Afya ambao tangu umezaliwa unatibiwa kwa dawa zao unaenda kumuamini Askofu Rashidi ambae hajui hata Paracentamol inatengenezwaje?

Kazi ipo!

Wenye akili ya kuona yajayo mbeleni ngoja tukachanjwe.

Over!
 
Mkuu, Meko I mean Yesu wa Chato alifanikiwa sana kuvuruga mind za watu kwamba chanjo ni mbaya na zinaletwa kutumaliza.

Hii imeleta madhara makubwa na ndio huu mtanziko wote unaotokea hivi sasa.

Uzuri corona aliyokuwa anaidharau ndio ikamfyeka.

Wenye akili tukachanjwe.
 
Hakika Mzee wetu Lowasa alikua sahihi sana kisema kipaumbele chake ni ELIMU, ELIMU, ELIMU

Rais Samia unakazi sana kuongoza vichwa vya namna hii...
Duh! kweli hao ni wajinga kabisa.

Lakini wahenga walisema fumbo mfumbie mjinga, mwerevu ataling'amua.
 
Hakika Mzee wetu Lowasa alikua sahihi sana kisema kipaumbele chake ni ELIMU, ELIMU, ELIMU

Rais Samia unakazi sana kuongoza vichwa vya namna hii...
Acha basi kuita watu wajinga kisa tu wanamtazamo tofauti na wako!

Disbelief iliopo juu ya chanjo sio kitu chepesichepesi kama unavyochukulia!

Unawaita wajinga kwa kuamini kuwa SSH alichanja normal saline! Mjinga sidhani kama anaweza waza hivyo...huyo ni mdadisi! Na kwa bahati mbaya hata ww huwezi toa jibu lililo na uhakika pasi chembe ya shaka! Ukweli wanao waliotoa hizo chanjo in the 1st place, siyo ww!

Umesema Gwajima hatakiwi kuaminiwa kwa kuwa hajui hata panadol inavyotengenezwa wakati huohuo unaamini daktari anajua panadol inavyotengenezwa...I'm sorry to disappoint you madam, hata daktari wa ktz hajui hiyo panadol inatengemezwaje!

Lakini ww mwerevu, ulipaswa kujua, ulimwengu tulionao ni ulimwengu wa information technology, kila mtu anayo access ya taarifa sahihi! Unaweza kuta huyo Gwajima anazo taarifa ambazo hata hao madocta hawana!

Ndio maana wagonjwa wa siku hizi wanakwenda kumuona daktari huku wakijua wanachoumwa na matibabu wanayotegemea kupewa! Sasa akikutwa daktari mwepesi shida inaanzia hapo, anaanza kuelekezwa na mgonjwa😜!

Zama za kuhodhi taarifa zilishapita kitambo ndugu, usitukane watu kienyeji ukageuka kuwa liability kwa aliyekutuma😜!
 
Hakika Mzee wetu Lowasa alikua sahihi sana kisema kipaumbele chake ni ELIMU, ELIMU, ELIMU

Rais Samia unakazi sana kuongoza vichwa vya namna hii...
Serikali isipokua makini na wasomi wapumbavu wanaoneza ujinga kwa wananchi wetu maskini wasiojua dunia jinsi inavoendelea, taifa litaangamia.

Ujinga kama huu nchini Nigeria zidi ya chanjo ya POLIO ulienezwa na MASHEIKH wenye msimamo mkali, kwa kuwaabia wananchi kuwa chanjo ya POLIO ni mpango wa nchi za magharibi kuzibiti waafrika na waislamu wasizaliane, matokeo yake watoto wengi wamekufa kwa POLIO na wengine wakapooza kwa kukosa chanjoya POLIO.
 
Next time wafanyie kazi mawazo ya Antony Diallo.

Japo CCM kuna unafiki wa hali ya juu ila ni likely vichaa walijipenyeza kipindi cha nyuma na kugombea uongozi na wakapewa dhamana hiyo !

Ni muda sasa tuangalie tulijikwaa wapi tusirudie tena makosa! 100% mawazo hayo ya kupinga chanjo yalitoka kwa kichaa baada ya kushauriana na vichaa wenzie
 
Wewe una uhakika gani kwamba ile ilikuwa chanjo halisi? Tumia akili kufikili
 
Hakika Mzee wetu Lowasa alikua sahihi sana kisema kipaumbele chake ni ELIMU, ELIMU, ELIMU

Rais Samia unakazi sana kuongoza vichwa vya namna hii.

mtu unamuuliza nipe sababu za kukataa chanjo anakwambia mbona chanjo ya malaria na UKIMWI wazungu bado hawajaigundua, hivi hizi ni akili za kawaida kweli au kuna tatizo?

Maana kama ni ujinga basi Taifa hili ujinga ni wa hali ya juu sana, Serikali naomba iwekeze zaidi kwenye elimu,

hivi kipindi ebora Imepamba moto Congo, chanjo yake siilitengenezwa faster, chanjo siilileta majibu chanya mpaka sasa hakuna Ebora, Waliochanjwa Ebora mlisikia wamekuabmazombi? Alietemgeneza chanjo ya Ebora ni nani? si mzungu huyohuyo?

unaacha kuamini wataalamu wa Afya ambao tangu umezaliwa unatibiwa kwa dawa zao unaenda kumuamini Askofu Rashidi ambae hajui hata Paracentamol inatengenezwaje?

Kazi ipo!

Wenye akili ya kuona yajayo mbeleni ngoja tukachanjwe.

Over!
Huu siyo ujinga tu bali ni upumbavu uliopitiliza. Nia yao ni mbaya. Wanataka tuendelee kuangamizwa na janga hili. Serikali iwashughulikie na kuwashitaki kama wauwaji.
 
Watu hao lazima ni sana CCM tupu.
Matendo yao na akili zao zinasadifu tafiti nyingi zilizo fanyika kuwa ni sana CCM.
Kuhusu huyu Askofu, bila shaka ni Mataga. Kifupi hana weledi wiwote, maisha yake ni ya ujanjaujanja, sio mkweli, kama anaweza kumdharau Mungu wake kwa kuongopea watu wasio jitambua masikinibakajipatia kipato kisicho halali kwa watu wenye matatizo wanao mtafuta Mungu kwa msaada, gatashindwa kuhadaa yeyote ilimradi yeye anapata pa kuongeza kipato. Ndo mana simshangai Askofu anaedai kutumwa na Mungu wa kweli kujiunga na genge la wauaji na wakandamizaji haki za raia mchana kweupe ili ale najisi.
Askofu wa kweli ukemea wa ovu. Haiwezi kunishawishi huyu aliyevkumbatia uovu eti Leo ana huruma na watu kwa kuwaonya juu ya chanjo. Angeanza kumwonya sliye mwingiza ubunge kwa hila, ndo aje awaonye masikini hawa.
 
Serikali isipokua makini na wasomi wapumbavu wanaoneza ujinga kwa wananchi wetu maskini wasiojua dunia jinsi inavoendelea, taifa litaangamia.
Ujinga kama huu nchini Nigeria zidi ya chanjo ya POLIO ulienezwa na MASHEIKH wenye msimamo mkali, kwa kuwaabia wananchi kuwa chanjo ya POLIO ni mpango wa nchi za magharibi kuzibiti waafrika na waislamu wasizaliane, matokeo yake watoto wengi wamekufa kwa POLIO na wengine wakapooza kwa kukosa chanjoya POLIO.
That was fake, wewe huoni hata mchomaji alikuwa hasukumi dawa??? Hivi wanapoleta kukabidhi hundi ya mfano huwa unadhani ni cheki kweli kweli??? Wewe na wenzako ni majinga kama mnadhania zile zilikuwa chanjo za kweli. Ile ilikuwa ni maigizo tu.
 
Back
Top Bottom