Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 53,857
- 121,995
Wanabodi,
Japo mimi ni mwandishi tuu wa habari na mtangazaji wa kujitegemea kwa kujitolea, nimegundua kumbe wito wangu ni ualimu, kufundisha watu, hivyo from time to time nitakuwa napiga humu darasa la bure la katiba, sheria na haki.
Somo la leo ni kuhusu halali, batili na batilifu, ambapo kuna sheria halali, batili na batilifu, kuna mikataba halali, batili na batilifu, kuna ndoa halali, batili na batilifu, na sii wengi wanajua kuwa hata Katiba ya JMT ni katiba batilifu yenye ubatili fulani ndani yake uliochomekewa kiubatili.
Kwa vile katiba ndio kitabu chetu kitakatifu, Ikulu ni mahali patakatifu petu, mpangaji wa patakatifu petu lazima awe mtakatifu, kwanini watendaji wanamtia najis mtakatifu wetu?!, kwanini kitabu chetu kitakatifu kiwe batilifu?. Kwanini serikali yetu itunge muswada wa sheria batili, Bunge letu litunge sheria batili na kumpelekea Rais wetu kuisaini sheria batili kuanza kutumika?!.
Outline
Halali, Batili na Batilifu
Utangulizi.
Tanzania tumetawaliwa na Waingereza hivyo tulipopata uhuru ile 1961, tulirithi sheria nyingi za kiingereza ambazo tuli copy na ku paste kutoka sheria za India iliyopata uhuru wake mwaka 1947, India nayo wali copy and paste kutoka sheria za Afrika Kusini iliyopata uhuru mwaka 1910. Kitendo cha copy and paste sheria za mahali fulani kinaitwa para materiale yaani ku copy neno kwa neno. Halali ni legit au legal, batili ni void na batilifu voidable.
Neno halali ni kitu ambacho ni cha halali kisheria, batili ni kitu ambacho sii halali kisheria, yaani haramu, na batilifu ni kitu chenye hitilafu au najis, hitilafu ikiondolewa kinakuwa halali. Najis ikitakaswa inatakasika lakini haramu hairekebishiki.
Katiba ndio sheria mama, sheria nyingine zote zinazotungwa lazima ziendane na katiba, sheria yoyote ikiwa inakwenda kinyume cha Katiba, sheria hiyo ni batili. Anayebalisha sheria batili ni katiba yenyewe.
Serikali yetu, Bunge letu zimekuwa zinatunga sheria batili na Mahakama yetu kuzitengua from time to time.
Mfumo wa utawala wetu ni kupitia mihimili 3 ya Bunge, Serikali na Mahakama.
Kazi ya Bunge ni kutunga sheria, kazi ya mahakama ni kutafsiri sheria, kazi ya serikali ni kutekeleza sheria.
Somo la Pili
Sheria Halali, Batili na Batilifu ni zipi?
Kama nilivyoeleza mwanzo, katiba ndio sheria mama, sheria nyingine yoyote inayokwenda kwa mujibu wa Katiba, ni sheria halali. Sheria yoyote itakayo kinzana na katiba, sheria hiyo inakuwa ni batili.
Na sheria yenye hitilafu za kisheria, ambazo zinaweza kurekebishika zinakuwa ni sheria batilifu.
Sheria batilifu zinarekebishika na kugeuka sheria halali, lakini sheria batili, hazirekebishiki kabisa na hakuna namna ya kuzihalalisha.
Somo la Tatu
Mikataba Halali, Batili na Batilifu ni ipi?
Mikataba, yaani contract ni makubaliano yenye nia ya mahusiano ya kisheria na kuna makubaliano tuu, yaani agreement.
Makubaliano yanaweza kuwa ya kukubaliana jambo lolote, ila ili agreement iwe ya kisheria, lazima jambo hilo liwe
1. Liwe ni jambo halali kisheria
2. Wana mkataba lazima wawe na akili timamu na legal age.
3. Makubaliano yawe yaliingiwa kwa ridhaa.
4. Lazima yawe na lengo mahsusi linalotekelezeka.
5. Lazima uwe na kipengele cha ukomo.
Hili nimelifafanua vizuri hapa Je, Wajua Kuwa Tanzania Hatuna Mkataba wa Muungano? Kilichopo ni Makubaliano Tuu ya Muungano?
Kuna mikataba mingi inaitwa ni mikataba lakini kiukweli sio mikataba bali ni makubaliano tuu, ukiwemo IGA ya DPW na Bandari zetu Japo Bunge Limeridhia, DPW Kuendesha Bandari Zetu, ni Makubaliano Tu, Tukithibisha Kuna Matatizo, Tunarekebisha Mkataba wa HGA, Kazi Nzuri Iendelee! kwenye HGA, ile IGA iliwekwa pembeni ila kwa vile HGA ni siri, watu hawajui.
Somo la Nne
Ndoa Halali, Batili na Batilifu
Ndoa halali ni mahusiano yanayofuata kanuni za mkataba
1. Wanandoa watimize umri halali
2. Watu wa jinsia tofauti
3. Mahusiano ya hiari ya kudumu milele
4 Wenye Akili timamu
4. Wasiwe maharimu
5. Kutimiza wajibu wa ndoa kwa performance
Wanandoa wakifunga ndoa performance ikashindikana kabisa, ndoa hiyo inakuwa ni ndoa batili, void marriage.
Consummation performance ikishindikana lakini baada ya muda utawezekana, ndoa hiyo inakuwa ni batilifu mpaka pale performance itakapowezekana na kuwa consummated
Kuna ndoa nyingi watu wanaishi tuu kwenye dhana ndoa, ama kuna ndoa kibao zina hati za ndoa lakini in reality sio ndoa, ni just a mare sham!.
Somo la Tano
Katiba Halali, Batili na Batilifu
Kama nilivyosema hapo mwanzo, Katiba ndio sheria mama, sheria yoyote inayokwenda kinyume cha katiba, sheria hiyo ni batili.
Kwa vile katiba ndio sheria mama, katiba haiwezi kuwa batili, inaweza tuu kukosa legitimacy lakini sio kuwa batili kwasababu katiba ndio source ya sheria zote.
Katiba ya Tanzania ya mwaka 1977, ilitoa haki mbili kuu za kisiasa, haki ya kuchagua na haki ya kuchaguliwa.
Asanteni.
Paskali.
Mada za Mwandishi kuhusu Katiba Mpya

- Halali, Batili na Batilifu ni nini?
- sheria halali, batili na batilifu ni zipi?
- mikataba halali, batili na batilifu ni ipi?
- Ndoa halali, batili na batilifu.
- Katiba halali, batili na batilifu.
- A way forward nini kifanyike.

- Haki ya kuchagua ni kwa mujibu wa Ibara ya 5 ya Katiba, kila Mtanzania akifkisha umri wa miaka 18, yuko huru kumchagua kiongozi anayemtaka.
- Ibara ya 21, imetoa haki kwa kila Mtanzania akifikisha umri wa miaka 21, yuko huru kugombea nafasi yoyote ya uongozi kuanzia serikali za mitaa hadi serikali kuu, bila kikwazo chochote.
- Sheria ya uchaguzi ikaweka shurti la ili kugombea ni lazi kwanza ujiunge na chama cha siasa, uwe mwanachama, kisha chama kikudhamini ndipo uruhusiwe kugombea.
- Mchungaji Mtikila akafungua kesi ya kikatiba kupinga sheria hiyo iko kinyume cha katiba. Mahakama Kuu, ikaitegua.
- Serikali ikakata rufaa, ikashindwa!, ndipo serikali yetu tukufu ikafanya jambo la ajabu, ikafanya mabadiliko batili ya katiba, ikauchukua ubatili huo, ikauchomekea kiubatili ndani ya katiba yetu!. Hivyo sasa mgombea kudhaminiwa na chama cha siasa ni kwa mujibu wa katiba!.
- Mtikila hakukubali katiba yetu inajisiwe, akafungua kesi nyingi kupinga mabadiliko hayo ya katiba. Akashinda. Mahakama Kuu ikashikilia msimamo shurti hilo ni batili, na mabadiliko ya katiba yaliyofanywa ni batili.
- Serikali ikakata rufaa Mahakama ya Rufaa, haikutengua hukumu ya mahakama kuu kuhusu ubatili wa kifungu hicho, ilikubali kweli ni batili, ila mahakama haiwezi kuliingilia bunge, hivyo kulishauri Bunge ndilo liondoe ubatili huo, Bunge halijaundoa mpaka kesho.
- Katiba ni single entity, ni kitu kimoja, ikichomekewa ubatili, inageuka ni katiba batilifu, siku zote tunafanya chaguzi zetu na ubatili huu.
- Sasa tumetunga sheria mpya ya uchaguzi yenye ubatili ule ule!. Kwanini Tanzania tuwe na katiba batilifu yenye ubatili?.
Asanteni.
Paskali.
Mada za Mwandishi kuhusu Katiba Mpya
- Mchakato huu wa Katiba ni umasikini wetu. Tujikubali, tuukubali, tuupigie kura ya ndio
- Bora Katiba tuikubali, tusiichukie CCM kwa sababu CCM itahukumiwa na Karma kwa Uovu wake
- Je Wajua Kuwa Kura ya "Hapana" Kwa Katiba Mpya! Ni Kura ya "Ndiyo!" Kwa Katiba Hii Iliyopo?
- Mabadiliko ya Sheria Bila Mabadiliko ya Katiba,Sawa na Kula Bila Kunawa!. Je Watanzania Tuna Haraka Sana na Uchaguzi Hadi Tukimbilie Kula Bila Kunawa?
- Katiba mbovu, sheria mbovu, mikataba mibovu. Leo tumetozwa zaidi ya Tsh. Bilioni 260. Kufanywa kichwa cha Mwendawazimu hadi lini?
- Pascal Mayalla: CHADEMA watengeneze kwanza Katiba mpya ya chama chao kabla ya kukimbilia katiba ya nchi, wawatendee haki wabunge 19
- Ijue Katiba ya JMT-1: Katiba ni nini, ya nani, ya kazi gani? Msemo "Katiba ndio kila kitu" Una maana gani? Katiba ina umuhimu gani?
- Tuombe Mwaka 2024 Uwe ni Mwaka wa Mageuzi ya Kweli ya Kidemokrasia ya Kweli Tanzania. Tume Huru, Uchaguzi Huru na wa Haki! Happy New Year!
- Watanzania ni maneno maneno na kulialia, Vitendo 0. Katiba ni maneno tu! Je, 2023 tuendeleze maneno matupu na kulialia au tubadilike tufanye kitu?
- Pongezi Rais Samia, Serikali, Kukubali Kubadili Sheria ya Uchaguzi, Tume Huru ya Uchaguzi!. Tuanze na Katiba Kwanza Ndipo Sheria Au?.
- Tahadhari ya hatari: CCM Imepania Kufanya Kinyume cha Maumbile!