Wajua Kuna Sheria Halali, Batili na Batilifu, Ndoa Halali, Batili na Batilifu, Je Wajua Katiba ya JMT ni Batilifu?. Why Ubatili Huu wa Katiba Yetu?!

Wajua Kuna Sheria Halali, Batili na Batilifu, Ndoa Halali, Batili na Batilifu, Je Wajua Katiba ya JMT ni Batilifu?. Why Ubatili Huu wa Katiba Yetu?!

Katiba ya nchi hii ya Tanzania ni BATILI KWA UJUMLA WAKE kwa sababu Kuu Moja tu kwamba MCHAKATO WOTE KABISA WA UTUNGWAJI WAKE NA UANDAAJI WA KATIBA HIYO HAUKUPATA RIDHAA YA UMMA WA WANANCHI WA NCHI HII YA TANZANIA. Umma wa Wananchi wa nchi hii ya Tanzania KAMWE haukuwahi kushirikishwa kuhusu kutungwa kwa Katiba hii iliyopo hivi sasa.
Kutokushirikisha watu kwenye utungaji wa katiba hakuifanyi katiba kuwa batili, ubatili ni jambo lolote la kisheria ambalo ni kinyume cha sheria.
Hakuna fast and hard rules za utungaji wa katiba, katiba ya Uingereza haijatungwa na watu na wala haijaandikwa popote!.

Kitendo cha kutowashirikisha watu kwenye utugwaji wa katiba kunaifanya tuu hiyo katiba kukosa legitimacy ya people's mandate.

Kwa vile katiba ya JMT ya mwaka 1977, ilitungwa wakati wa chama kimoja, Bunge la CCM ndio wawakilishi halali wa wananchi, lilijigeuza na kuwa Bunge la katiba likaijadili na kuipitisha katiba for just 45 minutes, tukapata katiba. Katiba hiyo ilikuwa nzuri ikaja kunajisiwa.
Kasoro hii kubwa iliyopo kwenye Katiba ya nchi hii Kamwe HAIREKEBISHIKI.
Njia pekee iliyopo ili kuepukana na kasoro hiyo ni moja tu, nayo ni Kutunga Katiba Mpya ambayo Mchakato wake wa Utungaji Utashirikisha Umma wa Wananchi wengi zaidi katika nchi hii ya Tanzania.
Hata mchakato wa katiba ya Warioba ungetupatia bora katiba na sio katiba bora!. Mchakato huu wa Katiba ni umasikini wetu. Tujikubali, tuukubali, tuupigie kura ya ndio
P
 
Back
Top Bottom