REMSA
JF-Expert Member
- Jan 25, 2012
- 2,579
- 956
Ndugu yangu, pole sana. Na yeyote anayepata hofu juu ya hili suala na yanayofanana na hayo. Wala haipo sababu ya kuwa na hofu yoyote. Hawa woote na mapesa yao, madhahabu yao, almasi na madaraka yao kwa hii dunia, amini nakuambia ni ubatili mtupu. Naamini kuwa haya mambo yapo 100%. Na anavyoeleza mleta mada ni kweli. Lakini huna sababu ya kuogopa. Sikiliza:
Ukiangalia tafsiri ya alama-mficho zilizo kwenye noti ya dola ya marekani, lile jicho moja ambalo liko juu kabisa ya pyramid, lile ni jicho la Lucifer. Na habari yooote hii unayoona na usiri wake wote, agenda ni moja tu, sio kumdhuru binadam kwa hali ya mwili, bali kwa hali ya roho. Hapa panahitaji ufaham kuelewa maana yake. Agenda kuu ya masuala yote haya ni KUMPINGA YESU KRISTO.
Nasema bila woga (sina nia ya kuoffend imani ya mtu hapa) kuwa hawa watu watafanya fujo zoote na kuwahangaisha wanadam hasa kwa kuwaficha ukweli ama wasione au kuipotosha kweli iliyopo, lakini shida yao kubwa na hofu yao ni YESU KRISTO. Huyu ndiye wanayemuogopa kama moto. Na kwa waamini, huyu YESU amesema katika agano jipya hasa Ufunuo kuwa mambo haya yatakuwapo siku za mwisho. Hawa watu na utajiri wao linapokuja suala la YESU KRISTO, wanakuwa wadogo kama pilton. Sasa kwanini wanahangaika na binadam?
Ni hivi, kwa waamini, ni kuwa Lucifer na YESU KRISTO wao wako katika war. Na hii ni kwa vile, sisi binadam tukiwa hai hatujahukumiwa bado, mpaka tufe. Lakini Lucifer yeye tayari alishahukumiwa kuwa ataenda Jehanam milele na milele na milele wakati huo ukifika. Sasa anachofanya ni kuwahadaa wanadam ili wao pia wakifa wahukumiwe kama yeye na wote wamjoin huko motoni. Na wanajua anayeweza kuwasaidia wanadam kuepuka hili ni YESU KRISTO. Maana mimi na wewe tunasema tunamjua YESU? Nakwambia hatuwezi kumjua YESU kuliko jinsi ambavyo Lucifer anamjua YESU. Usisahau Lucifer anapajua mbinguni palivyo na alitimuliwa huko.
Hivyo basi usiwe na hofu juu yao maana kinga yako ni imani yako katika Mungu wa kweli. Wao watahangaika sana na hii dunia na kusumbua wanadam lakini mwisho wao utafika na wote hawana ujanja hata utajiri wao ni ubatili mtupu hautawasaidia kuepuka kipondo kutoka kwa YESU KRISTO.
Na kuhusu utajiri huo wala usipate tabu, kwa waamini, yale maswali ambayo lucifer alimuuliza YESU kule jangwani kuwa ukinisujudia ntakupa hiki au kile "kwa kuwa dunia yote na milki zake ni mali yang" hadi leo anawauliza maelfu ya watu na wanaokubali ni kweli anawapa mali ila sharti ni moja tu - waende kinyume na ALIYE JUU (THE MOST HIGH). Pia ukisoma biblia utaona biblia yenyewe inamuita lucifer ni "mungu wa dunia hii"
Hivyo ni kuomba na kusali sana hayo yote ni ubatili mtupu.
Asante umeeleza si kwa kirefu sanaa,but imebeba maana yoote na msaada wa mwanadamu anaoweza kuupata kupitia kwa KRISTO YESU. So ni uamuzi wa mtu kuchagua kumwamini YESU ili asalimike na mkakati huu ovu wa ibilisi au kuendelea kuanguka katika mtego wa ibilisi na kunasaw'