Crocodiletooth
JF-Expert Member
- Oct 28, 2012
- 23,234
- 28,473
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dkt. Rhimo Nyansaho, pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mahmoud Thabit Kombo, wamefanya mazungumzo na ujumbe maalum wa wajumbe 11 wa Baraza la Wawakilishi la Marekani (Congress).
Ujumbe huo uliongozwa na Ronny Jackson, Mwenyekiti wa Kamati Ndogo ya Huduma za Kijeshi, Ulinzi na Usalama ya Baraza la Wawakilishi la Marekani (House Armed Services Subcommittee).
Mazungumzo hayo yamefanyika katika Makao Makuu ya zamani ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania, Ngome Upanga, jijini Dar es Salaam.
Katika mazungumzo hayo, Tanzania imeeleza umuhimu wa kuondolewa kwa baadhi ya vikwazo, ikiwemo vinavyohusu utoaji wa visa kwa Watanzania wanaosafiri kwenda Marekani, ili kuimarisha uhusiano kati ya wananchi wa nchi hizo mbili.
Kwa upande wake, ujumbe wa Marekani umeipongeza Tanzania kwa mchango wake katika kudumisha amani na usalama wa kikanda, hususan kupitia juhudi za kupambana na ugaidi na ushiriki katika operesheni za kulinda amani barani Afrika.
Pande hizo mbili zimekubaliana kuendelea kuimarisha ushirikiano wa kimkakati katika maeneo yenye maslahi ya pamoja na kuendelea na majadiliano kuhusu masuala yaliyowasilishwa na Tanzania katika vikao vijavyo.
N.b,Huwezi haribu uhusiano wetu mzuri na marekani,unajichosha tu akili.
°Uzi kama huu ungeliandikwa na chadema wangeandika mambo ya hovyo kabisa,kuharibu sifa nzuri ya taifa hili,maana ndiyo kiu yao!