Wajumbe Bodi ya Simba upande wa Wanachama wagoma kujiuzulu

Wajumbe Bodi ya Simba upande wa Wanachama wagoma kujiuzulu

Frank Wanjiru

JF-Expert Member
Joined
Apr 12, 2012
Posts
22,719
Reaction score
40,739
Yaliyojiri kwenye mkutano ulliofanyika leo wa Wanachama Simba SC.

๐—ช๐—ฎ๐—ท๐˜‚๐—บ๐—ฏ๐—ฒ ๐˜„๐—ฎ๐—บ๐—ฒ๐—ด๐—ผ๐—บ๐—ฎ ๐—ธ๐˜‚๐—ท๐—ถ๐˜‚๐˜‡๐˜‚๐—น๐˜‚ :
Wajumbe wote wa bodi upande wa Wanachama wa Simba SC wenye 51% ya hisa kwa kauli moja wamesema kuwa HAWAJIUZU. Hawajiuzulu kwa sababu hawajafanya kosa lolote, wao wamejitoa sana kwa klabu sometimes bila sapoti ya upande wa muwekezaji. Wamesema kujiuzulu ni UDHAIFU, na wao si DHAIFU.

Wamesema hata hizo kamati za usajili zinazotajwa kuwa zimebadilishwa ni UONGO, labda zimebadilishwa mitandaoni, kwa sababu kamati zote hupitishwa na bodi na wao wako kwenye bodi na hawajapitisha jambo kama hilo. Wamekaa kimya sana sasa wameamua kusema kinachoendelea.

๐—ž๐˜‚๐—ต๐˜‚๐˜€๐˜‚ ๐— ๐—ผ ๐——๐—ฒ๐˜„๐—ท๐—ถ
Kwa niaba ya wajumbe wa bodi ya wakurugenzi Simba SC upande wa wanachama, Issa Massoud amesema kuwa.

Mohamed Dewji amegeuza fedha ambazo amekuwa akitoa Kwa klabu kama msaada kuwa deni au zimegeuzwe kuwa mtaji maana yake Simba haimdai BILLION 20 tena.

"Fedha zote ambazo Mo Dewji alikuwa anazitoa yaani za kununua mchicha, kununua kandambili boxer za wachezaji zozote zile ambazo ametoa kwenye Simba Sports Club amesema anazidai, na ameelekeza zibadilishwe ndio ziwe mtaji wake ambao anatakiwa autoe Simba Sports Club."

"Kama tunakopeswa hizo hela kwani lazima tukope kwa MO? Taasisi za fedha si zipo nyingi tunaweza tukakopa? Kwanza kama ni mkopo haujafuata taratibu alikopa nani na kwanini walikopa, na mkopo huo unawekwa kwa ajili ya aseti ipi, hapa ukiondoa udhamini maana ana udhamini."

๐—ž๐˜‚๐—ต๐˜‚๐˜€๐˜‚ ๐˜‚๐˜€๐—ฎ๐—ท๐—ถ๐—น๐—ถ
"Kamati yoyote ya Simba Sports Club inaundwa na Bodi, kwa hivyo basi kamati zote zilizoundwa nje ya bodi sisi hizo kamati hatuzitambui, na hata usajili utakaofanyika nje ya bodi sisi huo hatuutambui kwasababu tutakuwa tunakiuka utaratibu wa Simba SC." - CPA Issa Masoud Mjumbe wa Bodi Simba SC.

"Sisi wenyewe tunasikia tu mtandaoni mara kamati ya usajili imeteuliwa, sasa sisi hizo kamati hatuzitambui kama bodi."

ยฉ๏ธ CPA. Issa Masoud.
Mjumbe wa bodi ya wakurugenzi Simba.

PIA SOMA

- Salim Abdallah 'Try Again' ajiuzulu uenyekiti bodi ya wakurugenzi Simba

- Bodi ya Simba upande wa mashabiki wanataka kumtapeli Mo Simba yake

- Tetesi: - Simba imepasuka. Kuna Simba ya Try Again na Simba ya Mo, Kila upande unauroga upande mwingine

- Tetesi: - Simba inatarajia kumrejesha tena Barbara Gonzalez kwenye Bodi

- - Hivi lile sakata la baadhi ya mashabiki wa simba kumshinikiza Mwenyekiti wao Mangungu kujiuzulu, limefikia hatua gani mpaka sasa?
 
Watoke waende zao,wamefeli wamefeli wamefeli sanaaa na kuifikisha timu sehemu mbaya.Wanakula hela za bure tu.

Watu wapya waje wapuuzi hao
 
Nadhani viongozi upande wa wanachama walikuwa na makosa kabla pesa walipokea bila shaka mkopo Kwa maana wangerejesha mo yeye anataka hiyo hela aailipwe iwekwe kwenye mtaji
 
Tujiuzuru kwenda wapi?

Kamwe hatutajiuzuru, haiwezekani wale wahuni wachcahe watake kupora uhuru, mawazo na haki ya 51% ya Klabu.
hawa wetu ni matapeli. wamemtapeli mo team. wapo hapo for 3+ years leo ndo wa naongea. tena lugha ya kitapeli kabisa. wana quality players. bodi ina usajili tangu lini?? means hata report ya kocha awana. maana bodi wanapokea report Na players, wanapitisha budget.

tapeli kwa mo
 
Back
Top Bottom