Wajumbe wa bunge la katiba Zanzibar yawaka

Wajumbe wa bunge la katiba Zanzibar yawaka

MAGEUZI KWELI

JF-Expert Member
Joined
Jul 16, 2011
Posts
1,947
Reaction score
253
Baada ya uteuzi wa wajumbe 201 wa bunge la katiba, baadhi ya wazanzibar wameanza kuwaka kwa hasira wakisema nchi mbili zimeungana, inakuwa je bara watoke 14 na zanzibar watoke 6? Hata wengi walioteuliwa wengi wahamiaji hakuna mzanzibar halisi.

Sijui kitatokea nini, radio fm za zanzibar ni watu wanapiga simu na kuongea .

Jamani lengo la katiba kwa Amani litafika?

Nawakilisha
 
Hawa wazanzibar watatusumbua sana kama tutaendelea kuwachekea..
 
Kwani zanzibar kuna mwenyeji?wote si wakuja...yakheee mie mwaraaab wa oman!!!
 
Wa Zanzibar wasiwe na wasiwasi maana ma CCM always ni full kujipendekeza kwao...
 
Pamoja na kwamba nchi zimeungana lakini pia tunaanalia population ie idadi ya watu, na eneo. Zanzibar ina watu milioni moja wakati bara ina watu milioni 43 plus. Lazima idadi ya wajumbe itofautiane
 
CDM waligomea hii sheria hadi wakapigwa bungeni.
 
Waacheni wadai haki yao. Unless mtuambie kwenye muungano wa hizi nchi mbili kuna "Big Brother".
 
Katiba ni ta watanzania lazima ipatikane tena kwa amani kabisa hakuna kelele wala vurugu.
 
Bora irudi Tanganyika ...na sisi tumechoka our partners are too whining..
 
Sheria inasema fika watanzania bara na Zanzibar haijasema wazanzibari weusi au waarabu au wapemba imesema wazanzibari!

Tufikirie kwenye bunge la katiba maana majina tayari! Haturudi nyuma kamwe!
 
Pamoja na kwamba nchi zimeungana lakini pia tunaanalia population ie idadi ya watu, na eneo. Zanzibar ina watu milioni moja wakati bara ina watu milioni 43 plus. Lazima idadi ya wajumbe itofautiane
Kama ingekuwa mnajali idadi ya watu basi isingekuwa nafasi za wajumbe kutoka Tanganyika zimehodhiwa na Wakristo.
 
Hao wazanzibar tunawalea sana sijui kwa nn tusiwaache waende zao. Watu gani hawana shukurani na sisi tunakomaa tu.
Eti kisa tunaenzi muungano.
Hii mambo sijui itaisha lini?
 
Wazanzibari wasiwe na hasira maana sasa tunatafuta katiba ya kuitoa ccm madarakani. Tukimaliza hili tutarudi kwenye mchakato wa kupata katiba tuitakayo.
 
Baada ya uteuzi wa wajumbe 201 wa bunge la katiba, baadhi ya wazanzibar wameanza kuwaka kwa hasira wakisema nchi mbili zimeungana, inakuwa je bara watoke 14 na zanzibar watoke 6?
Hata wengi walioteuliwa wengi wahamiaji hakuna mzanzibar halisi.

Nawakilisha


1. Vipi hawaja HOJI kuwa kuna WAUNGUJA wangapia na WAPEMBA WANGAPI?

2. Ni Yupi mzanzibari halizi?
a. Mnzazi bara
b. Mnzanzi unguja
c. Mnzanzi Pemba
d. Mnzaznzi Oman
e.......
 
Back
Top Bottom