Mathanzua
JF-Expert Member
- Jan 4, 2017
- 17,449
- 23,124
Hayo ni mawazo yao mkuu,na huwezi kumkataza mtu kutoa mawazo yake,ilimradi havunji sheria.Ila ukweli ni kwamba Rais alishasema mara nyingi kwamba hataongeza hata dakika moja.Leo kulikuwa na kikao cha halmashauri kuu mkoa cha kupokea taarifa za utekelezaji wa ilani ambao mkuu wa mkoa wa Ruvuma Christine Mndeme alikuwa anawasilisha, Katika kikao hicho kilichorushwa moja kwa moja na Chanel Ten, wajumbe wa haashauri kuu mkoa wa Ruvuma wamekubaliana Rais Magufuri aendelee KUONGOZA kwa miaka 20 zaidi.
Kama mawazo hayo yataungwa mkono na mikoa mingine ina maana inawezekana Magufuli ndiye Rais atakayekaa madarakani miaka mingi Ikulu kuliko hata Nyerere
Viongozi wastaafu wanasemaje kuhusu hilo suala? Kwa sababu tangu lianzishwe hakuna kiongozi yeyote mstaafu aliyewahi kukemea hiyo michezo. Kukaa kwao kimya unaleta shaka kama wanaunga mkono au la
Tujadili kwa pamoja haya ma
Kingine ni kwamba hata kama ikitokea Rais akibadili mawazo,itabidi katiba ibadilishwe na swala hilo lipelekwe kwa wananchi kwa maamuzi ya mwisho.Hili si swala la kuamuliwa na wajumbe wa CCM wa ngazi yeyote ile mkuu.