Uchaguzi 2020 Wajumbe wa Kamati ya Uchaguzi CCM jimbo la Butiama mtalaaniwa

sopinta

Member
Joined
May 28, 2020
Posts
46
Reaction score
93
Wajumbe wa Kamati ya Uchaguzi wa CCM jimbo la Butiama, mmefanya kitendo kibaya sana. Katika kura za maoni mmeshindwa kumuenzi Baba wa Taifa Mwl. Nyerere kwa kumchagua mtoto mmoja wa Baba wa taifa kweli mmeshindwa?

Familia ya Baba wa Taifa imetoa wagombea wawili katika hao mmeona hakuna anayefaa? Mnasema kuwa mzee Makongoro au Madaraka kwa maoni yenu mmeona wote hawatoshi?

Uchaguzi wa mwaka huu ni tarehe 28 Oktoba ambapo ukirudisha siku 14 nyuma ni siku ambayo tunamuenzi Baba wa taifa. Mtasema mnamuenzi vipi Baba wa Taifa hili?

Pamoja na juhudi zote za Baba wa Taifa za kuanzisha chama cha CCM na kutumia muda wake mwingi katika kukijenga chama leo mnaona familia yake haiwezi kuongoza! Kama sio BABA wa taifa hiki chama mngekijulia wapi?

Tukumbuke tu Mzee Makongoro na Madaraka katika utoto na ujana wao wameishi maisha ya upweke sana hii ni kutokana na Baba wa taifa alikua bize katika mapambano mbalimbali juu ya taifa hili kama vile kupigania Uhuru wa taifa , mapambano ya kukijenga chama kutoka katika mifumo ya kikoloni.

Leo mnawaona kuwa ni watu wasiofaa ndani ya chama !!!!!

Hebu rudisheni heshima ya BABA WA TAIFA.
 
katika kula za maoni mmeshindwa kumuenzi Baba wa Taifa Mwl. Nyerere kwa kumchagua mtoto mmoja wa Baba wa taifa, kweli mmeshindwa? familia ya Baba wa Taifa imetoa wagombea wawili katika hao mmeona hakuna anayefaa?
Mkuu, hii Mimi nimeipenda sana, imenipa kuona ni jinsi gani watu hasa vigogo ama watoto wa vigogo wasivyoishi vema na jamii.

Hilo ni funzo, haiwezekani, na ijulikane, jamii unayoishi nayo wakati mwingine ndio yaweza kuamua hatima ya mtu!

Unataka kuwa kiongozi Wakati jamii inayokuzunguka haioni msaada wowote wa kile ulicho nacho!

Tunategemeana! Mtu yeyote mwenye kuthamini Neno hilo, hufika mbaaali sana kimaisha.
 
Yule mwingine ambaye baba yupo watoto wanapewa nafasi za urais, watoto wa vigogo wengine ambao baba zao wapo wanapitishwa.

Anyways Nyerere alikua mjamaa Sana kuliko hata waasisi wa ujamaa wenyewe ndio maana hata familia yake imekua Kama ilivyo
 
Moja ya kosa kubwa la Nyerere ni kutowasomesha watoto wake na kutowapa exposure. Hili limeicost sana familia yake na kupelekea kuishi kwa kudra za maraisi waliopo.

Kinachoitokea familia ya Nyerere ni matokeo ya kujisahau na kuisahau familia yake.
 
Aliyaweka maslahi ya taifa mbele kuliko ya familia yake.

Ndio maana anafahamika vizuri zaidi kama Baba wa Taifa kuliko Baba wa familia yake.
 
Moja ya kosa kubwa la Nyerere ni kutowasomesha watoto wake na kutowapa exposure. Hili limeicost sana familia yake na kupelekea kuishi kwa kudra za maraisi waliopo.

Kinachoitokea familia ya Nyerere ni matokeo ya kujisahau na kuisahau familia yake.
Una hakika?
 
Wajumbe wa kamati ya uchaguzi chama cha CCM jimbo la Butiama, mmefanya kitendo kibaya sana, katika kura za maoni mmeshindwa kumuenzi Baba wa Taifa Mwl. Nyerere kwa kumchagua mtoto mmoja wa Baba wa taifa kweli mmeshindwa?

Familia ya Baba wa Taifa imetoa wagombea wawili katika hao mmeona hakuna anayefaa? Mnasema kuwa mzee Makongoro au Madaraka kwa maoni yenu mmeona wote hawatoshi?

Uchaguzi wa mwaka huu ni tarehe 28 Oktoba ambapo ukirudisha siku 14 nyuma ni siku ambayo tunamuenzi Baba wa taifa. Mtasema mnamuenzi vipi Baba wa Taifa hili?

Pamoja na juhudi zote za Baba wa Taifa za kuanzisha chama cha CCM na kutumia muda wake mwingi katika kukijenga chama leo mnaona familia yake haiwezi kuongoza! Kama sio BABA wa taifa hiki chama mngekijulia wapi?

Hebu rudisheni heshima ya BABA WA TAIFA.
Butiama nao wawe wanakuwa wazalendo, wameanza kuonyesha dalili za kupoteza uzalendo siku hizi. Baada ya Madaraka Nyerere kutangaza nia, walitakiwa wakubaliane mtu mwingine asichukue fomu, alitakiwa abaki Madaraka tu.

Hawa watu nao mimi siku hizi wameshaanza kunichanganya, inaoenekana kama wameparanganyika baada ya Mwalimu kuondoka!
 
Makongoro kashakuwa Mbunge, Naona ajitambui uroho , pia ili ushinde kura za maoni ccm mpaka utoe hela.
 
Mtoa post hivi unawafahamu vizuri hao unaowatetea ama?
Hao watoto wa nyerere hawana nidhamu wengi ni walevi sana hata makongoro nyerere ambaye awamu zote wamejitahidi kumsaidia habebeki kwa sababu ya ulevi mwingi, endapo wangekuwa ni vijana watulivu waadilifu wangekuwa wapo mbali sana kusingekuwa na uhitaji wa kuwapigia kelele
 
Wajumbe wa Kamati ya Uchaguzi wa CCM jimbo la Butiama, mmefanya kitendo kibaya sana. Katika kura za maoni mmeshindwa kumuenzi Baba wa Taifa Mwl. Nyerere kwa kumchagua mtoto mmoja wa Baba wa taifa kweli mmeshindwa?

Familia ya Baba wa Taifa imetoa wagombea wawili katika hao mmeona hakuna anayefaa? Mnasema kuwa mzee Makongoro au Madaraka kwa maoni yenu mmeona wote hawatoshi?

Uchaguzi wa mwaka huu ni tarehe 28 Oktoba ambapo ukirudisha siku 14 nyuma ni siku ambayo tunamuenzi Baba wa taifa. Mtasema mnamuenzi vipi Baba wa Taifa hili?

Pamoja na juhudi zote za Baba wa Taifa za kuanzisha chama cha CCM na kutumia muda wake mwingi katika kukijenga chama leo mnaona familia yake haiwezi kuongoza! Kama sio BABA wa taifa hiki chama mngekijulia wapi?

Hebu rudisheni heshima ya BABA WA TAIFA.
Ujumbe unatakiwa uwe umefika "laud and clear" hii nchi si ya hisani tena.
 
Kaka kule Butiama 95% wananchi uelewa ni zero kabisa bila hela hupati kura hata 1,Nimrod Mkono aliwazoesha vibaya alikuwa anagawa hela kama njugu sasa Familia ya Nyerere Makongoro,Madaraka na yule Jackton Manyerere hela hawana .Hata huyo Jumanne sagini na Frank Mahemba waliongoza kwa kura kuna jamaa alikuwa ananiambia kuwa wamemwaga hela vibaya sana.

Kitu kingine ni kuwa ukiangalia neno Butiama fikra zinazoingia akilini mwako ni kwa Wazanaki tu kitu ambacho sio kweli kwa sasa asilimia zaidi ya 70 wakazi wa Butiama ni wakurya,hivyo wamegawanyika katika ukanda kuna ukanda una wakurya wengi sana ambao ndio wanahela kuliko wazanaki.
 
Back
Top Bottom