Uchaguzi 2020 Wajumbe wa Kamati ya Uchaguzi CCM jimbo la Butiama mtalaaniwa

Uchaguzi 2020 Wajumbe wa Kamati ya Uchaguzi CCM jimbo la Butiama mtalaaniwa

Mkuu, hii Mimi nimeipenda sana, imenipa kuona ni jinsi gani watu hasa vigogo ama watoto wa vigogo wasivyoishi vema na jamii.

Hilo ni funzo, haiwezekani, na ijulikane, jamii unayoishi nayo wakati mwingine ndio yaweza kuamua hatima ya mtu!

Unataka kuwa kiongozi Wakati jamii inayokuzunguka haioni msaada wowote wa kile ulicho nacho!

Tunategemeana! Mtu yeyote mwenye kuthamini Neno hilo, hufika mbaaali sana kimaisha.
Makongoro/Madaraka walipata dingi ambae hakua na Nepotism na wala hakujali mambo ya future za watoto wake either kwa kuwapendelea wapate vitengo serikalini au ufisadi wowote ule.

Unataka kusema Huyu mtoto wa Mwinyi(Rais mtarajiwa zenji) na wakina Rizwan Kikwete hawa wameishi vipi vyema na jamii zao zaidi ya kutumia nafasi za wazazi wao kupata nafasi hizo.

Kitu pekee ninachomlaumu Nyerere ni kutokuiba kadri iwezekanavyo na kutowapa upendeleo maalumu watoto/ndg zake maana viongozi wote waliofuata baada ya yeye wote wanawapa mashavu familia zao na ukwasi wanao wa kutosha sana tu.

Kama yupo kiongozi ambae hajafanya hayo baada ya Nyerere mtaje hapa.
 
kwanza wao wenyewe wamebugi kuchukua form wote wawili inaonekana hawako pamoja
 
Mwinyi TUNAMWONA HUSSEN
Mkapa mtoto wake simfahamu
Kikwete TUNAMWONA RIDHI 1

Sema utakuwa utawala wa kiukoo
Angalia E.L. YUPO FREDRICK
 
Magufuli na Kamati yake ya CCM kule Butiama ni mara 100 wachukue Mtia nia aliyepata zero kuliko wale waliongoza kwa kura huku wamemwaga ni hela tu.
 
Wajumbe wa Kamati ya Uchaguzi wa CCM jimbo la Butiama, mmefanya kitendo kibaya sana. Katika kura za maoni mmeshindwa kumuenzi Baba wa Taifa Mwl. Nyerere kwa kumchagua mtoto mmoja wa Baba wa taifa kweli mmeshindwa?

Familia ya Baba wa Taifa imetoa wagombea wawili katika hao mmeona hakuna anayefaa? Mnasema kuwa mzee Makongoro au Madaraka kwa maoni yenu mmeona wote hawatoshi?

Uchaguzi wa mwaka huu ni tarehe 28 Oktoba ambapo ukirudisha siku 14 nyuma ni siku ambayo tunamuenzi Baba wa taifa. Mtasema mnamuenzi vipi Baba wa Taifa hili?

Pamoja na juhudi zote za Baba wa Taifa za kuanzisha chama cha CCM na kutumia muda wake mwingi katika kukijenga chama leo mnaona familia yake haiwezi kuongoza! Kama sio BABA wa taifa hiki chama mngekijulia wapi?

Hebu rudisheni heshima ya BABA WA TAIFA.

Butiama wanajitambua. Shida ni Zanzibar wanaochaghuliwa Rais na Tanganyika.
 
Wasubilie tu ubunge wa viti maalumu wa kuteuliwa, kosa ni baba yao aliwapa elimu ya jeshini badala elimu ya kichwani mfano, uhandisi, udactari,

pili ma genius mara nyingi huzaa watoto famba kwa hiyo sio kosa lao walishindwa vip kuachiana mmoja agombee.

Ila wajumbe wa butiama hawangalii usoni wamewachinja tu bila huruma
 
Kaka kule Butiama 95% wananchi uelewa ni zero kabisa bila hela hupati kura hata 1,Nimrod Mkono aliwazoesha vibaya alikuwa anagawa hela kama njugu sasa Familia ya Nyerere Makongoro,Madaraka na yule Jackton Manyerere hela hawana .Hata huyo Jumanne sagini na Frank Mahemba waliongoza kwa kura kuna jamaa alikuwa ananiambia kuwa wamemwaga hela vibaya sana.

Kitu kingine ni kuwa ukiangalia neno Butiama fikra zinazoingia akilini mwako ni kwa Wazanaki tu kitu ambacho sio kweli kwa sasa asilimia zaidi ya 70 wakazi wa Butiama ni wakurya,hivyo wamegawanyika katika ukanda kuna ukanda una wakurya wengi sana ambao ndio wanahela kuliko wazanaki.

Sawa natumaini kamati kuu itafanya kitu, uzuri mmoja chama kiliweka vijana wengi wa kuchunguza mienendo ya wagombea kama mshindi alitumia pesa kushinda basi ajue kuwa ubunge haupati.......
 
Makongoro kashakuwa Mbunge, Naona ajitambui uroho , pia ili ushinde kura za maoni ccm mpaka utoe hela.

Kwa mwaka huu mgombea yoyote aliyetoa hela ili ashinde basi ajue kamati kuu itamkata tu....
 
Mkuu,
Unataka kusema Huyu mtoto wa Mwinyi(Rais mtarajiwa zenji) na wakina Rizwan Kikwete hawa wameishi vipi vyema na jamii zao zaidi ya kutumia nafasi za wazazi wao kupata nafasi hizo.
Mtoto wa Mwinyi smjui vizuri, Ila Ridhiwan namfahamu vema, ni kijana mwenye kujichanganya na watu, saa ingine unaweza kudhani si mtoto wa Rais na maisha yake kitaa ni ya kawaida Sana!!

Mimi Bado nasisitiza tu kwamba, Maisha ya kubebwa siku lazima mtu alie, lakini maisha ya wewe mwenyewe uyaboleshe Kwa namna ipi, ni lazima jamii itambue uwepo wako!!

Baba wa Taifa Ni Baba Bora Sana Kwa wanae, Ila nahisi watoto ndio tatizo!
Ukaribu na jamii haihitaji ubebebwe, jibebe mwenyewe
 
Wajumbe wa Kamati ya Uchaguzi wa CCM jimbo la Butiama, mmefanya kitendo kibaya sana. Katika kura za maoni mmeshindwa kumuenzi Baba wa Taifa Mwl. Nyerere kwa kumchagua mtoto mmoja wa Baba wa taifa kweli mmeshindwa?

Familia ya Baba wa Taifa imetoa wagombea wawili katika hao mmeona hakuna anayefaa? Mnasema kuwa mzee Makongoro au Madaraka kwa maoni yenu mmeona wote hawatoshi?

Uchaguzi wa mwaka huu ni tarehe 28 Oktoba ambapo ukirudisha siku 14 nyuma ni siku ambayo tunamuenzi Baba wa taifa. Mtasema mnamuenzi vipi Baba wa Taifa hili?

Pamoja na juhudi zote za Baba wa Taifa za kuanzisha chama cha CCM na kutumia muda wake mwingi katika kukijenga chama leo mnaona familia yake haiwezi kuongoza! Kama sio BABA wa taifa hiki chama mngekijulia wapi?

Hebu rudisheni heshima ya BABA WA TAIFA.

Mkuu umesahau kulikuwa na mjadala humu baada ya Hussein Mwinyi kupitishwa kupeperusha bendera kwamba amependelewa/ fadhila ya baba yake. Sasa wale wa Nyerere ...................!, hata hivyo watu wa Mara wanapenda ukweli na wala si wanafiki.
 
Mtu mwenye busara na mwenye malengo makubwa juu ya maisha yake, huitumia elimu yake Kwa ajiri ya wengine (jamii)na sio yeye kujinufaisha, naye Jamii ndio itamnufaisha Kwa kile alichotoa Kwa jamii

The Bible says
Kipimo kilekile utoacho, ndicho utakachopimiwa!

Unaishije na jamii?

Muulize mwenye Degree 4 atakwambia maneno hayo, naye yamemkuta huko kwake,
 
Mkuu,
Mtoto wa Mwinyi smjui vizuri, Ila Ridhiwan namfahamu vema, ni kijana mwenye kujichanganya na watu, saa ingine unaweza kudhani si mtoto wa Rais na maisha yake kitaa ni ya kawaida Sana!!

Mimi Bado nasisitiza tu kwamba, Maisha ya kubebwa siku lazima mtu alie, lakini maisha ya wewe mwenyewe uyaboleshe Kwa namna ipi, ni lazima jamii itambue uwepo wako!!

Baba wa Taifa Ni Baba Bora Sana Kwa wanae, Ila nahisi watoto ndio tatizo!
Ukaribu na jamii haihitaji ubebebwe, jibebe mwenyewe
Saaa katika watu wanajichanganya na raia wa kawaida kabisa kitaa ni wakina Makongoro/Madaraka hao mpk wanalewaga na kuzima huko uswahili na wala mtoto wa ushuani Ridhiwani hajawazidi hao majamaa kwa kujichanganya na watu.

Ridhiwani kupitia cheo cha dingi ake amefanya biashara sana tu,ametengeneza networks za kutosha,alikua ana sponsor wasanii kwny mambo yao ya music,amewapa watu michongo ya kazi kwa sana tu(Na wala simlaumu kwa chochote alichofanya maana hata mimi ningefanya hivyo hivyo tu).Sasa mtu ataenda kuwashobokea wakina Madaraka watampa nini Connections au nini wkt wenyewe mfukoni ni choka mbovu tu.

Nyerere hakuiba wala kutumia nafasi yake kujinufaisha yeye na familia yake hio ndio bahati mbaya pekee aliyoifanya,ilitakiwa wakina Makongoro wawe kama wakina Uhuru Kenyatta robo ya ardhi nzima nzima hapa Tz ni yao,biashara kubwa kubwa hapa bongo zote zao ndipo tungewaheshimu na ungeona. kama wasingekua marais wa nchi hii au ku-influence siasa za nchi.

Nyerere alikua mzalendo sana kwa nchi yake.
 
Saaa katika watu wanajichanganya na raia wa kawaida kabisa kitaa ni wakina Makongoro/Madaraka hao mpk wanalewaga na kuzima huko uswahili na wala mtoto wa ushuani Ridhiwani hajawazidi hao majamaa kwa kujichanganya na watu.
Sina hoja tena mkuu, Ila nimecheka Sana aisee,

Labda sasa jamii imeona itawapoteza zaidi pindi wakipata Ulaji mahali watalewa mara dufu na kuhatarisha maisha yao
 
Mkuu umesahau kulikuwa na mjadala humu baada ya Hussein Mwinyi kupitishwa kupeperusha bendera kwamba amependelewa/ fadhila ya baba yake. Sasa wale wa Nyerere ...................!, hata hivyo watu wa Mara wanapenda ukweli na wala si wanafiki.
Yule mmoja wa Nyerere wamepa U-Nec lkn nje ya hapo hana chochote yaani hata kwny ukuu wa mkoa huwa hawakumbukwi aisee.
 
Mkuu, hii Mimi nimeipenda sana, imenipa kuona ni jinsi gani watu hasa vigogo ama watoto wa vigogo wasivyoishi vema na jamii.

Hilo ni funzo, haiwezekani, na ijulikane, jamii unayoishi nayo wakati mwingine ndio yaweza kuamua hatima ya mtu!

Unataka kuwa kiongozi Wakati jamii inayokuzunguka haioni msaada wowote wa kile ulicho nacho!

Tunategemeana! Mtu yeyote mwenye kuthamini Neno hilo, hufika mbaaali sana kimaisha.
Nikweli inawezekana hawatoshi kwenye jamii wanayoishi
 
Sina hoja tena mkuu, Ila nimecheka Sana aisee,

Labda sasa jamii imeona itawapoteza zaidi pindi wakipata Ulaji mahali watalewa mara dufu na kuhatarisha maisha yao
Hahah wale ni wapiga maji hatari,mmoja alishalewaga akaenda nje ya ofisi(Nyeti) anakofanyia kazi mkewe akaanza kupiga honi ovyo ovyo mkewe akaamuru awekwe ndani kwa muda.
 
Mwinyi TUNAMWONA HUSSEN
Mkapa mtoto wake simfahamu
Kikwete TUNAMWONA RIDHI 1

Sema utakuwa utawala wa kiukoo
Angalia E.L. YUPO FREDRICK
Nicolas MKapa
Fanya tafiti Kama sikosei ni katibu mkuu msaidiz ndani ya waizara moja
 
Back
Top Bottom