Uchaguzi 2020 Wajumbe wa Kamati ya Uchaguzi CCM jimbo la Butiama mtalaaniwa

Watoto wa mwalimu nyerere hawakulelewa kwa mazingira ya kupokea Wala kutoa rushwa hivyo wamenyimwa kura kisa hatatoi rushwa.ea jk kapita,wa lowasa kapita hao Sasa ndio vinara wa kutoa rushwa. Ila butiama mungu anawaona, baba yao kaanzisha chama leo mnawachinjia watoto wake ziwani?kwa Kura 2 na 5 jumla Kura 7?
 
Nyerere wacheni apumzike kwa Amani. Watoto wake hawajawajenga Kama watoto wa mtu aliyeongoza nchi kwa zaidi ya miaka 20, angalia watoto wa viongozi wengine si kwenye ubunge Wala uraisi, wanarithi vyeo vya wazazi wao
 
Hahah wasimamishe hapo watoto wa Nyerere Vs watoto wa (Lowassa+Kikwete+Mkapa+Magufuli+Mwinyi+Sumaye+Other vigogo) ndipo utajua kweli Nyerere alikua Ni Maskini wa Mali aisee.
 
Kweli wangeheshimu kama monduli naona fred lowasa kaula
 
Moja ya kosa kubwa la Nyerere ni kutowasomesha watoto wake na kutowapa exposure. Hili limeicost sana familia yake na kupelekea kuishi kwa kudra za maraisi waliopo.

Kinachoitokea familia ya Nyerere ni matokeo ya kujisahau na kuisahau familia yake.
Nani kakuambia hawakusoma? Unawajuwa? Unajua historia yao? Unakurupuka tu kuandika kiti usichojua.
 
kumbuka hizo kura 5 walizopata wote 2 ni kati ya kura 545 za wajumbe wote.
 
Hakika CCM Butiama mtajibu makosa haya ya kutomuenzi Mwalimu.
 
Nakubaliana na Sopinta. Kwa kweli hata mimi hiyo Kamati imeniboa. Wangempa mmoja aidha Makongoro au Madaraka. Lakini kuwaacha kabisa kwa kweli hawakututendea haki sisi "Nyerereists"
 
Wao ndio wanawajua vizuri sisi hatukai nao sanasana tunawasoma magazetini
 
Acha uongo.
Mi nimekaa Butiama na nimeona jinsi familia ya Mwalimu ilivyo down to earth.
Ukiacha jina kubwa la Mwlimu, watoto hao hawajiinui na wanaongea na kila mtu.
Tatizo ni kwamba baba yao(MMwalimu) hakjilimbikizia mali.
 
Moja ya kosa kubwa la Nyerere ni kutowasomesha watoto wake na kutowapa exposure. Hili limeicost sana familia yake na kupelekea kuishi kwa kudra za maraisi waliopo.

Kinachoitokea familia ya Nyerere ni matokeo ya kujisahau na kuisahau familia yake.
Watot o wale wamesoma vizuri tu kama watoto wengine lakni shida ni kutokuw akaribu na jamii inayowazunguka. Makongoro amekuwa hadi Mbunge wa Kuteuliwa, Mbunge wa Afrika Mashariki, Mwenyekit wa CCM ngazi ya Mkoa na sasa ni Mjumbe wa Kamati Kuu alishindwa vipi kuwa karibu na jamii (cham chake huko Butiama)? Pia walishindwa kweli hata kushauriana ili mtoto mmoja ndiye agombee badala ya wote wawili kutia nia . Kwa hiyo, wapiga kura wana sababu nzuri kabisa za kuwaacha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…