Wajumbe wa Simba (tunawapongeza) msikubali kuiuza timu kwa shida ya siku moja

Sawa Mo anaweza kuondoka lakini hatutotaka kusikia simba inataka kurudi kwenye mfumo wa wanachama, kwahiyo watutafutie mtu sahihi wampe 49% ambaye hataihujumu timu
Naunga mkono apatikane mwekezaji anayefuata kanuni
 
51 ni pmj na mashabiki wanaojaza viwanja
Wakiacha kwenda kwa kususia club itakuwaje
Hao hawajawahi zungumzia hisa zao hata siku moja wametoa mijicho kwenye 49% ndio matumbo ndio yamewaweka hapo, hii timu bora ingeuzwa tu wanatuboa sana mashabiki
 
Aliwahi kujaribu huko nyuma kwa club kadhaa inasemekana alifeli sana akakimbia
Cha muhimu Mo aanzishe team yake binafsi from the scratch kama alivyofanya mwenzake Bakhresa
 
Tuzungumze ukweli wachezaji wanaolipwa zaidi ya million tano kwa mwezi hawzidi kumi wengine ni chini ya mikion
 
Tunasafari ndefu mwekezaji anataka aogopeke tu baada ya kufuata kanuni
 
Muhimu tunahitaji maendeleo ya club ,hiyo mifumo ya uanachama haijawahi kutupeleka popote, miaka miwili ya Mo tumeona matunda yake,inavyoonekana viongozi wameona hakuna njia za upigaji tena,wanaanza figisu
Wasiturudishe zama za ujima, Kuna wanaojitutumua eti mo atuachie timu yetu utadhani huko nyuma ilivyokua mikononi mwao hakukua na migogoro.

Cha msingi ni wakae chini waweke mambo Sawa, kwa hatua ya sasa simba imeonyesha mafanikio.
 
Hao wajumbe wanalipa mishahara ya wchezaji, tuanzie hapo... Kama mwenye kumiliki hisa 49% anaweka mezani bil 20 hao wanahisa wanaomiliki 51% wameweka ngapi nao mezani?
Swali zuri
 
Mbona alishaharibu CV siku nyingi tu bwana kwa kushindwa kuindesha African Lyon
Ukweli usemwe hata km ni tajiri
 
Wabongo bana,mtu atoe bilion ishirini,wewe hujatoa kitu ni mjumbe tu,unataka uwe na maamuzi ya management ya mradi?,,yale yale ya bagamoyo port,,,hakuna mwekezaji anaweka bilions halafu asitake zirudi
 
Yalimshinda siku nyingi hayo akakimbia kule African lion
 
Hao hawajawahi zungumzia hisa zao hata siku moja wametoa mijicho kwenye 49% ndio matumbo ndio yamewaweka hapo, hii timu bora ingeuzwa tu wanatuboa sana mashabiki
Wana shangaza sana mkuuu.kazi kukodolea macho tuuu hisa za mo, miaka yote wapo na hatukuona chochotee cha maaana.

Nilishangaa kusikia kua hata ule uwanja wa bunju ni msaada toka kwa mkwele .

Izingatiwe kua hata hayo mabadliko ya mfumo wa clab yaliwezekana baada ya wale jamaaa kuwekwa rupango, lasivyo hadi leo ingekua bado ni ngonjeraa tuu.
 
Mkuu sidhani kama anaweza, hivi African Lyon si ilikuwa yake!?
 
Kilicho wazi sana kwa sasa watu wanaoleta mtafaruku simba ni wale ambao mirija ya kuitafuna simba imezibwa ndiyo maana wanataka kuharibu mfumo mpya waendelee kula pesa za bure za club.

Wanataka Mo aweke mzigo kwenye hisa zake hizo 49% hizo 51% wameshalipia au wanataka waendelee kumkamua pesa bila wao kutoa hata mia?

By the way simba hivi sasa imeshatoka kwenye mfumo wa uanachama ni watu gani hao ambao wanalalamikia klabu yao ilhali hawajui hata jezi za Simba zinapatikanaje ?

Tuache uswahili, tuache wizi, tutafute vya kwetu siyo kula jasho la watu wengine kwa kisingizio cha kulinda maslahi ya wanachama.

Stand united waligombana kwa pesa za ACACIA leo hii wako daraja la kwanza na waliogombana walishatokomea kusikojulikana.

Mpira wetu unaharibiwa na watu wenye njaa za kishamba sana kama hao wanaochochea mgogoro simba.
 
Watu wanataka waanze kupata dividends bila kuwa na hisa.

Wanataka Mo atoe mzigo twenty billion na uwanja juu wao hata hisa Moja hawajanunua.

Kufanya biashara na waswahili yataka moyo sana.
Wabongo bana,mtu atoe bilion ishirini,wewe hujatoa kitu ni mjumbe tu,unataka uwe na maamuzi ya management ya mradi?,,yale yale ya bagamoyo port,,,hakuna mwekezaji anaweka bilions halafu asitake zirudi
 
Huu ndio wakati wenu kwenda kuongoza club, na tusipoona mafanikio yoyote hesabuni nyie ni wachawi wa maendeleo!! Hao wajumbe walishafanya kitu ipi toka simba ianze? Mwenye hisa 49 tunaona anachoweka je nyie wenye 51 mmeweka nini? Embu acheni uchawi nyie
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…