Wajumbe wa Simba (tunawapongeza) msikubali kuiuza timu kwa shida ya siku moja

Wajumbe wa Simba (tunawapongeza) msikubali kuiuza timu kwa shida ya siku moja

Sawa Mo anaweza kuondoka lakini hatutotaka kusikia simba inataka kurudi kwenye mfumo wa wanachama, kwahiyo watutafutie mtu sahihi wampe 49% ambaye hataihujumu timu
Naunga mkono apatikane mwekezaji anayefuata kanuni
 
51 ni pmj na mashabiki wanaojaza viwanja
Wakiacha kwenda kwa kususia club itakuwaje
Hao hawajawahi zungumzia hisa zao hata siku moja wametoa mijicho kwenye 49% ndio matumbo ndio yamewaweka hapo, hii timu bora ingeuzwa tu wanatuboa sana mashabiki
 
Aliwahi kujaribu huko nyuma kwa club kadhaa inasemekana alifeli sana akakimbia
Cha muhimu Mo aanzishe team yake binafsi from the scratch kama alivyofanya mwenzake Bakhresa
 
Tuzungumze ukweli wachezaji wanaolipwa zaidi ya million tano kwa mwezi hawzidi kumi wengine ni chini ya mikion
Mo naomba ajiuzuru turudi kule tulipotoka!

mishahara inayolipwa kwa wachezaji kwa mwezi mmoja si chini ya million mia mmoja hapo hujajumlisha safari kambi na viposho vya uendeshaji; club kama simba inahitaji si chini ya million 300 kujiendesha yenyewe. Kilomoni na genge lake wakabidhiwe timu tuone

yajayo yanafurahisha
 
Tunasafari ndefu mwekezaji anataka aogopeke tu baada ya kufuata kanuni
Mpira ni pesa,uwekezaji lakini katika Vilabu vikongwe vya Simba na Yanga siasa ni nyingi saaana.
Hata wawekezaji nao wanafichaficha mambo hawapo wa wazi kihivyo.
Wengi ni wafadhili ambao wana mambo yao kimaslahi tu .. wakikamilisha wanakimbia.
Simba imeanza mchakato huu vizuri lakini nilijua tu kwa siasa zetu hizi na wanachama hali zao zilivyo na mwekezaji mwenyewe alivyo nilijua safari itakuwa ya mashaka.
Kuendeleza mpira Tanzania ni kuachana na vilabu hivi kwanza.
Vilabu hivi lazima vikihitaji mafanikio wabadilike kuanzia wanachama hadi viongozi.
Simba hadi leo hii bado mambo hayapo wazi kiwanja cha mpira nacho bado na maneno yameanza.
Kama Simba ilivyo hakuna haja ya maneno ya chini kwa chini au mafumbo weka mambo hadharani omba ushauri.
Vilabu hivi shida tupu. Na ndio shida ya maendeleo ya kandanda nchini.
 
Muhimu tunahitaji maendeleo ya club ,hiyo mifumo ya uanachama haijawahi kutupeleka popote, miaka miwili ya Mo tumeona matunda yake,inavyoonekana viongozi wameona hakuna njia za upigaji tena,wanaanza figisu
Wasiturudishe zama za ujima, Kuna wanaojitutumua eti mo atuachie timu yetu utadhani huko nyuma ilivyokua mikononi mwao hakukua na migogoro.

Cha msingi ni wakae chini waweke mambo Sawa, kwa hatua ya sasa simba imeonyesha mafanikio.
 
Hao wajumbe wanalipa mishahara ya wchezaji, tuanzie hapo... Kama mwenye kumiliki hisa 49% anaweka mezani bil 20 hao wanahisa wanaomiliki 51% wameweka ngapi nao mezani?
Swali zuri
 
Mbona alishaharibu CV siku nyingi tu bwana kwa kushindwa kuindesha African Lyon
Ukweli usemwe hata km ni tajiri
Tunaowapa kiburi hao viongozi ni siye washabiki siye tunaoenda viwanjani wenzetu washabiki wa ulaya huwa wanaisusia timu na pia kushinikiza viongozi kutoka.

Nampa pole Mo kufanya kazi na waswahili nikujiaribia cv yake, waswahili bado tuko kwenye evolution tunahitaji kutawaliwa badala ya kujitawala just imagine timu ina miaka zaidi ya 80 no uwanja no kitega uchumi chochote bado tunaendelea kuziamini fikra zilezile ziendelee kusimamia timu.

Hata watu wanaosema hizi timu ni za wanachama miye nakataa hizi timu zinamilikiwa na kigenge fulani ambacho kinaishi kupitia hizi timu hivyo kuchukua hizi klabu zijiendeshe na sawa na kukiua hicho kigenge kitu ambacho ni impossible
 
Wabongo bana,mtu atoe bilion ishirini,wewe hujatoa kitu ni mjumbe tu,unataka uwe na maamuzi ya management ya mradi?,,yale yale ya bagamoyo port,,,hakuna mwekezaji anaweka bilions halafu asitake zirudi
 
Yalimshinda siku nyingi hayo akakimbia kule African lion
Huwa namshangaa sana MO jinsi anavyowekeza pesa yake SIMBA, MO angetakiwa asuke timu yake kama Bakressa.

Timu yenye asilimia 100 za umiliki wake, atumie hizo pesa zake ajenge bonge la uwanja, ashushe makocha na wachezaji wa viwango vya kimataifa.

Mashabiki wataongezeka tuu Man city, chelsea hazikuwa na mashabiki wengi hivi kabla hazijanunuliwa.

MO piga simba chini pesa uliyowapa mpaka sasa ifanye sadaka, tengeneza timu yako
 
Hao hawajawahi zungumzia hisa zao hata siku moja wametoa mijicho kwenye 49% ndio matumbo ndio yamewaweka hapo, hii timu bora ingeuzwa tu wanatuboa sana mashabiki
Wana shangaza sana mkuuu.kazi kukodolea macho tuuu hisa za mo, miaka yote wapo na hatukuona chochotee cha maaana.

Nilishangaa kusikia kua hata ule uwanja wa bunju ni msaada toka kwa mkwele .

Izingatiwe kua hata hayo mabadliko ya mfumo wa clab yaliwezekana baada ya wale jamaaa kuwekwa rupango, lasivyo hadi leo ingekua bado ni ngonjeraa tuu.
 
Huwa namshangaa sana MO jinsi anavyowekeza pesa yake SIMBA, MO angetakiwa asuke timu yake kama Bakressa.

Timu yenye asilimia 100 za umiliki wake, atumie hizo pesa zake ajenge bonge la uwanja, ashushe makocha na wachezaji wa viwango vya kimataifa.

Mashabiki wataongezeka tuu Man city, chelsea hazikuwa na mashabiki wengi hivi kabla hazijanunuliwa.

MO piga simba chini pesa uliyowapa mpaka sasa ifanye sadaka, tengeneza timu yako
Mkuu sidhani kama anaweza, hivi African Lyon si ilikuwa yake!?
 
Hakika mficha maradhi kifo humuumbua ndio kauli nzuri ya kusema kwa sasa

Hali si shwari ndani ya club ya Simba wajumbe wanaoiwakilisha timu wanalalamika chini kwa chini wanasema hawashirikishwi kwa chochote wenyewe ni kupewa taarfa tu wenye sauti wamebaki ni magori tu ambaye anatumika kuiibia club
Ndugu zangu kuwa mwekezaji wa timu sio ujanja ujanja
Sasa anapikuja mwekezaji mwenye lengo la kuvuna tu hiyo haileti maana faida inatakiwa ipatikane kwa pande zote mbili

Baadhi ya wajumbe ambao wamekataa kuihujumu club wanasema huyu mwekezaji mwaka Jana alisema million 250 zinatosha kujenga uwanja wa mazoezi kule bunju lakini mpaka sasa hata greda zimeacha kufanya kazi zile milion 250 zimetumikaje? Sema wajumbe wanaogopa kumwambia boss kwenye kikao kwa kuogopa usalama wao ukizingatia yule ni tajiri

Pia wajumbe wanasema club iliingiza zaidi ya billion mbili kwenye mechi za kimataifa pamoja zawadi walizopewa kutoka Caf
Ilo hizo pesa zimeingia kwenye account ya kampuni ya MTU na sio kwenye account ya club
Wajumbe wanajiuliza kamawekezaji anavunja sheria kwenye mwaka wa pili tu je akishakaa miaka sita wanachama watakuwa na sauti juu ya timu yao?

Motto unaofuka ni mbaya sana ndani ya uongozi wa Simba

Viongozi wengi wasimba wamekuwa wanawatumia wanahabari kufukisha ujumbe kwa mo kwani anaogopeka sana

Ahsanteni
Kilicho wazi sana kwa sasa watu wanaoleta mtafaruku simba ni wale ambao mirija ya kuitafuna simba imezibwa ndiyo maana wanataka kuharibu mfumo mpya waendelee kula pesa za bure za club.

Wanataka Mo aweke mzigo kwenye hisa zake hizo 49% hizo 51% wameshalipia au wanataka waendelee kumkamua pesa bila wao kutoa hata mia?

By the way simba hivi sasa imeshatoka kwenye mfumo wa uanachama ni watu gani hao ambao wanalalamikia klabu yao ilhali hawajui hata jezi za Simba zinapatikanaje ?

Tuache uswahili, tuache wizi, tutafute vya kwetu siyo kula jasho la watu wengine kwa kisingizio cha kulinda maslahi ya wanachama.

Stand united waligombana kwa pesa za ACACIA leo hii wako daraja la kwanza na waliogombana walishatokomea kusikojulikana.

Mpira wetu unaharibiwa na watu wenye njaa za kishamba sana kama hao wanaochochea mgogoro simba.
 
Watu wanataka waanze kupata dividends bila kuwa na hisa.

Wanataka Mo atoe mzigo twenty billion na uwanja juu wao hata hisa Moja hawajanunua.

Kufanya biashara na waswahili yataka moyo sana.
Wabongo bana,mtu atoe bilion ishirini,wewe hujatoa kitu ni mjumbe tu,unataka uwe na maamuzi ya management ya mradi?,,yale yale ya bagamoyo port,,,hakuna mwekezaji anaweka bilions halafu asitake zirudi
 
Hakika mficha maradhi kifo humuumbua ndio kauli nzuri ya kusema kwa sasa

Hali si shwari ndani ya club ya Simba wajumbe wanaoiwakilisha timu wanalalamika chini kwa chini wanasema hawashirikishwi kwa chochote wenyewe ni kupewa taarfa tu wenye sauti wamebaki ni magori tu ambaye anatumika kuiibia club
Ndugu zangu kuwa mwekezaji wa timu sio ujanja ujanja
Sasa anapikuja mwekezaji mwenye lengo la kuvuna tu hiyo haileti maana faida inatakiwa ipatikane kwa pande zote mbili

Baadhi ya wajumbe ambao wamekataa kuihujumu club wanasema huyu mwekezaji mwaka Jana alisema million 250 zinatosha kujenga uwanja wa mazoezi kule bunju lakini mpaka sasa hata greda zimeacha kufanya kazi zile milion 250 zimetumikaje? Sema wajumbe wanaogopa kumwambia boss kwenye kikao kwa kuogopa usalama wao ukizingatia yule ni tajiri

Pia wajumbe wanasema club iliingiza zaidi ya billion mbili kwenye mechi za kimataifa pamoja zawadi walizopewa kutoka Caf
Ilo hizo pesa zimeingia kwenye account ya kampuni ya MTU na sio kwenye account ya club
Wajumbe wanajiuliza kamawekezaji anavunja sheria kwenye mwaka wa pili tu je akishakaa miaka sita wanachama watakuwa na sauti juu ya timu yao?

Motto unaofuka ni mbaya sana ndani ya uongozi wa Simba

Viongozi wengi wasimba wamekuwa wanawatumia wanahabari kufukisha ujumbe kwa mo kwani anaogopeka sana

Ahsanteni
Huu ndio wakati wenu kwenda kuongoza club, na tusipoona mafanikio yoyote hesabuni nyie ni wachawi wa maendeleo!! Hao wajumbe walishafanya kitu ipi toka simba ianze? Mwenye hisa 49 tunaona anachoweka je nyie wenye 51 mmeweka nini? Embu acheni uchawi nyie
 
Back
Top Bottom