Mimi kama mshabiki muhimu kwangu ni team kufanya vizuri kila mwaka ndani na nje ya Africa ndio furaha ya mshabiki yoyote sijali nani anaendesha. Nashabikia Liverpool nje huko sijali nani anaendesha team kikubwa team inanifurahisha kila wiki. Simba mwaka jana tumeona imefanya vizuri baada ya kubadili mfumo mwaka mmoja tu wakati miaka zaidi ya 80 tulikuwa kama homa ya vipindi hatuna assets wala team nzuri tupo tupo tu kama tatu mzuka. Mimi nadhani tatizo kubwa kuna watu hawana kazi wanaishi kutegemea hizi team kula sasa mfumo wa kibishara mirija inakatwa hapo njaa ndio inaanza hawa wanaosema turudi kule ni wale wasioitakia mema team ila wanatumia kujifanya wanajali team kutimiza maslahi yao binafsi. Mshabiki anataka team bora uwanjani na nje basi. Tukishindwa hapa basi tusahau tena kama kuna mtu atakuja kutokea kuwekeza katika team zetu na kwa hali ngumu hii ya sasa ndio basi ma team makubwa ulaya wanatafuta wawekezaji wapya sisi hatutaki na utakuta huyu mtu sitaki hawezi hata kutimiza mahitaji ya family yake tu nyumbani.