Wajumbe wa Simba (tunawapongeza) msikubali kuiuza timu kwa shida ya siku moja

Wajumbe wa Simba (tunawapongeza) msikubali kuiuza timu kwa shida ya siku moja

Mimi kama mshabiki muhimu kwangu ni team kufanya vizuri kila mwaka ndani na nje ya Africa ndio furaha ya mshabiki yoyote sijali nani anaendesha. Nashabikia Liverpool nje huko sijali nani anaendesha team kikubwa team inanifurahisha kila wiki. Simba mwaka jana tumeona imefanya vizuri baada ya kubadili mfumo mwaka mmoja tu wakati miaka zaidi ya 80 tulikuwa kama homa ya vipindi hatuna assets wala team nzuri tupo tupo tu kama tatu mzuka. Mimi nadhani tatizo kubwa kuna watu hawana kazi wanaishi kutegemea hizi team kula sasa mfumo wa kibishara mirija inakatwa hapo njaa ndio inaanza hawa wanaosema turudi kule ni wale wasioitakia mema team ila wanatumia kujifanya wanajali team kutimiza maslahi yao binafsi. Mshabiki anataka team bora uwanjani na nje basi. Tukishindwa hapa basi tusahau tena kama kuna mtu atakuja kutokea kuwekeza katika team zetu na kwa hali ngumu hii ya sasa ndio basi ma team makubwa ulaya wanatafuta wawekezaji wapya sisi hatutaki na utakuta huyu mtu sitaki hawezi hata kutimiza mahitaji ya family yake tu nyumbani.
 
Nyie mnaitaka Timu ya Simba au Mnaitaka Simba yenya Mafanikio ?
Kama Mnataka Simba yenye mafanikia basi,
Ni lazima mkubali uwekezaji ndani ya Simba na mjenge mahusano mazuri na Mwekezaji.
Kama mnaitaka Timu ya Simba iwepo hapa nchini bila kujali maendeleo yake basi Mpeni timu Kilomoni na hao viongozi wengine ambao wanasema wanauchungu na timu yao.
Kama Serikali imebariki uwekezaji ndani ya Simba basi hamna budi kuuheshimu uwekezaji.
 
Hao wajumbe wanalipa mishahara ya wchezaji, tuanzie hapo... Kama mwenye kumiliki hisa 49% anaweka mezani bil 20 hao wanahisa wanaomiliki 51% wameweka ngapi nao mezani?
Kumbuka

Baada ya kuweka bil 20 ndio anakuwa anamiliki 49%

Kwa hiyo anza upya kuuliza swali lako, Baada ya MO kuweka 20 bil. amewekeza Tsh ngapi nyingine kisha uulize na hao Wanasimba wengine wameweka kiasi gani

By the way, nasikia ile bil 20 aliyoahidi bado hajatoa hata sumni

Huyu Muhindi wenu ni mjanja mjanja sana, ni muoga kuwekeza kwenye timu (kama Bakhresa). African Lyon ilikuwa ni timu yake/mali yake kwa 100% lakini akaitelekeza baadae

Huko Singida pia aliwahi kuwa na timu ikamshinda, matokeo yake anakuja kwenye ready made club halafu anataka awapangie cha kufanya wakati haimiliki timu kwa 50%+
 
Mo naomba ajiuzuru turudi kule tulipotoka!

mishahara inayolipwa kwa wachezaji kwa mwezi mmoja si chini ya million mia mmoja hapo hujajumlisha safari kambi na viposho vya uendeshaji; club kama simba inahitaji si chini ya million 300 kujiendesha yenyewe. Kilomoni na genge lake wakabidhiwe timu tuone

yajayo yanafurahisha
Na huo ndio ujanja alioutumia

Ameiingiza Simba kwenye life style/operation costs ambayo bila yeye simba haitaweza kujiendesha

Lengo lake simba ione hakuna simba bila Mo
 
Simba ina Mali gani?
Unajua Moo anatoa kiasi gani kwenye timu?
 
Njaa mbaya sana ukifatilia kwa umakini wanaosema moo anataka kuhujumu SSC hawana uwezo wakutengeneza pesa kwaajili ya familia zao.utakuta hata mabinti wa kazi majumban wanawakopa mishahara ya 40000, mtu kama huyu ukimuuliza ukimpa mkude tu amlipe milion tano kwa miezi sita anawezaa?? Kina kagere sasa...!tusikimbilie kumlaumu moo huendeshaji wa timu sio mrahisi mpira wa sasa hivi unahitaji pesa atakama anataka Hati apewe taratibu za kisheria zifatwe kwa makubaliano sahihi sasa mzee kilomoni anakomaa utafikiri anaweza kujaza hata bus la simba mafuta lifike namungo na kurudi..
 
Je nyie mna nia ya dhati ya kufuata kanuni .mana knachotokea nyie wazee hampendi mambo ya nyooke mnajua mtashindwa kuiba pesa za club na janja janja za hapa na pale nyie ndo mmefanya maisha ya wachezaji zaidi ya 300 ya miatatu kuwa ya ovyoovyo kwa kushabikia mfumu wa kipuuzi wa kuua ndoto za vijana mitaani mana maendeleo ya mpira wa Tanzania yanategemea uwekezaji bora wa simba na yanga natamani ni kutukane kwasababu maisha ya vijana na watoto wenye vipaji ni ya ovyoovyo kwa upumbavu watu wachache mpaka mpira wa miguu una dhalaurika nchini ina onekana ni mchezo wa kupoteza muda tu kumbe kuna wapuuzi wa chache kama wewe na genge lako mnafanya makusudi kukwamisha maendeleo ya mpira acheni usenge mna haribu maisha ya watu mitaani huku ajira zenyewe ndio zilibidi ziwe hizi.Nina mengi sana moyoni mana hali ya wachezaji mpira daraja la kwanza na baadhi ya timu za ligi kuu si nzuri.
Tunasafari ndefu mwekezaji anataka aogopeke tu baada ya kufuata kanuni
 
Na huo ndio ujanja alioutumia

Ameiingiza Simba kwenye life style/operation costs ambayo bila yeye simba haitaweza kujiendesha

Lengo lake simba ione hakuna simba bila Mo
Mbona unaji contradict! Huku unasema ameeingiza simba kwenye operation cost ambazo bila yeye timu haiwezi kuzimudu. Huku unasema anawaibia. Hebu tujuze kabla ya uwekezaji wa Mo klabu ilikuwa na kiasi gani bank? Hali ya klabu ilikuaje? Hao viongozi wameleta maendeleo gani kwa klabu?
 
Kilimoni ana ubavu wa kumlipa mshahara hata mchezaji mmoja? Jeuri ya Kilomoni kuna watu wapo nyuma yake sio bure
 
Hao wajumbe wanalipa mishahara ya wchezaji, tuanzie hapo... Kama mwenye kumiliki hisa 49% anaweka mezani bil 20 hao wanahisa wanaomiliki 51% wameweka ngapi nao mezani?
Mo ili atambulike kama mwanahisa wa SSC ni lazima kwanza aweke mezani 20 bill maana hawezi kujiita muwekezaji wakati hakuna alichowekeza! Nakushangaa unapouliza wanachama wameweka kiasi gani, inamaana hujui kuwa wanachana wameweka mezani hisa za club!!? Mo anatakiwa kabla ya yote atoe kwanza mzigo wa kununua hizo hisa ndo wakae mezani sasa kujadili mengineyo.
Uhalali wa Mo kuwepo pale msimbazi kama muwekezaji ni zile hisa 49% kwahiyo kama hajazilipia basi hana haki wala nguvu ya kufanya maamuzi yoyote kama mmiliki.
 
Unaposema "Wasikubali kuiuza timu kwa shida ya siku moja"... una maana gani?
Simba inauzwa?
 
Hakika mficha maradhi kifo humuumbua ndio kauli nzuri ya kusema kwa sasa

Hali si shwari ndani ya club ya Simba wajumbe wanaoiwakilisha timu wanalalamika chini kwa chini wanasema hawashirikishwi kwa chochote wenyewe ni kupewa taarfa tu wenye sauti wamebaki ni magori tu ambaye anatumika kuiibia club
Ndugu zangu kuwa mwekezaji wa timu sio ujanja ujanja
Sasa anapikuja mwekezaji mwenye lengo la kuvuna tu hiyo haileti maana faida inatakiwa ipatikane kwa pande zote mbili

Baadhi ya wajumbe ambao wamekataa kuihujumu club wanasema huyu mwekezaji mwaka Jana alisema million 250 zinatosha kujenga uwanja wa mazoezi kule bunju lakini mpaka sasa hata greda zimeacha kufanya kazi zile milion 250 zimetumikaje? Sema wajumbe wanaogopa kumwambia boss kwenye kikao kwa kuogopa usalama wao ukizingatia yule ni tajiri

Pia wajumbe wanasema club iliingiza zaidi ya billion mbili kwenye mechi za kimataifa pamoja zawadi walizopewa kutoka Caf
Ilo hizo pesa zimeingia kwenye account ya kampuni ya MTU na sio kwenye account ya club
Wajumbe wanajiuliza kamawekezaji anavunja sheria kwenye mwaka wa pili tu je akishakaa miaka sita wanachama watakuwa na sauti juu ya timu yao?

Motto unaofuka ni mbaya sana ndani ya uongozi wa Simba

Viongozi wengi wasimba wamekuwa wanawatumia wanahabari kufukisha ujumbe kwa mo kwani anaogopeka sana

Ahsanteni
Hivi ni kweli bundi aliyetoka jangwani bado yuko kariakoo????
 
Swala la Dewji ni kama lile la wakati ule la Glazer na Manchester united. Unaanza na hisa kidogo, unanunua mafanikio, wanachama wanakuamini halafu unajimilikisha klabu. Mpaka leo Manchester wanalia na ile familia. Lakini hii ya Dewji ni mbaya zaidi. Wote tunamjua Dewji, asipodhibitiwa Simba itapotea. Serikali ilipokua inabinafsisha viwanda, Dewji alinunua kwa gharama ndogo sana ili aviendeleze. Matokeo yake imekua sifa tu kwamba Dewji ana viwanda na ukihesabu mali anazomiliki inaonekana ana zaidi ya dollar billioni moja. Dollar billioni moja ni sifa kubwa sana kwake kuliko kufanya biashara na kukuza uchumi wa Tanzania kama malengo ya kubinafsishiwa viwanda yalivohitaji. Wafanyakazi wa MeTL ndio wanaolipwa kidogo zaidi kwa viwanda vya aina moja Tanzania. Huyu bwana alichukua ubunge wa Singida, lengo lake lilikua nini? Alifanikisha? Dewji ana akili za kitoto bado, akili za kukuza CV kwenye majarida ya matajiri. Simba ni timu kubwa, brand kubwa sana, ikiandikwa Dewji ni mmiliki wa Simba jamaa atakua amemalizana na sisi. Bora huu huu uhusiano uliopo ubaki hivi hivi. Dewji anatafuta sifa kwa simba tuendelee kumbana hivi hivi. Siungani mkono na Kilomoni kua mbishi lakini kama linazuia Dewji kupata ujiko kwa simba nalibariki. Dewji akichoka aondoke tutakua tumemchuna vya kutosha tayari.
 
Bila hela kwa sasa hufanyi chochote kile; hata mwanamke wako lazima.akutose baharini....Mwenye hela jiunge naye kumnunia tajiri wakati mfukoni hata buku huna ni mawazo ya kifukara... ni kupoteza muda!!
 
Back
Top Bottom