Wajumbe wa Simba (tunawapongeza) msikubali kuiuza timu kwa shida ya siku moja

Wajumbe wa Simba (tunawapongeza) msikubali kuiuza timu kwa shida ya siku moja

Bakheresa ni suala la muda tu, waliokaribu nae wanajua. Ni vigumu sana kwa Tanzania uanzishe timu yako nje ya hizi timu za kariakoo na ukaiendesha kibiashara. Muulize Bayser atakwambia siri ni kwanini Mtibwa imedumu mpaka sasa.
kuna siku nilimsikia anasema hakuna faida yoyote anayoipata kwa team mtibwa sugar zaidi ya kuigaramia tu, kuna ukweli?
 
Huwa namshangaa sana MO jinsi anavyowekeza pesa yake SIMBA, MO angetakiwa asuke timu yake kama Bakressa.

Timu yenye asilimia 100 za umiliki wake, atumie hizo pesa zake ajenge bonge la uwanja, ashushe makocha na wachezaji wa viwango vya kimataifa.

Mashabiki wataongezeka tuu Man city, chelsea hazikuwa na mashabiki wengi hivi kabla hazijanunuliwa.

MO piga simba chini pesa uliyowapa mpaka sasa ifanye sadaka, tengeneza timu yako
kuanzisha team anaweza, kujenga uwanja anaweza pia
je hao mashabiki wa kushabikia team yake na kujaza uwanja atawatoa wapi?
ndio maana kina Abromavich, sheikh mansuli walinunua vilabu ambavyo tayari vipo na misingi na mashabiki wapo!

kumbuka team sio uwanja na wachezaji tu mashabiki ndio watakupa faida
 
Kwanini asiweke wakati anatangaza bidhaa kupitia club
Wabongo bana,mtu atoe bilion ishirini,wewe hujatoa kitu ni mjumbe tu,unataka uwe na maamuzi ya management ya mradi?,,yale yale ya bagamoyo port,,,hakuna mwekezaji anaweka bilions halafu asitake zirudi
 
Hataki hisa aziziwe MTU mwengine anataka awe yeye tu watu wamuabudu
Kilicho wazi sana kwa sasa watu wanaoleta mtafaruku simba ni wale ambao mirija ya kuitafuna simba imezibwa ndiyo maana wanataka kuharibu mfumo mpya waendelee kula pesa za bure za club.

Wanataka Mo aweke mzigo kwenye hisa zake hizo 49% hizo 51% wameshalipia au wanataka waendelee kumkamua pesa bila wao kutoa hata mia?

By the way simba hivi sasa imeshatoka kwenye mfumo wa uanachama ni watu gani hao ambao wanalalamikia klabu yao ilhali hawajui hata jezi za Simba zinapatikanaje ?

Tuache uswahili, tuache wizi, tutafute vya kwetu siyo kula jasho la watu wengine kwa kisingizio cha kulinda maslahi ya wanachama.

Stand united waligombana kwa pesa za ACACIA leo hii wako daraja la kwanza na waliogombana walishatokomea kusikojulikana.

Mpira wetu unaharibiwa na watu wenye njaa za kishamba sana kama hao wanaochochea mgogoro simba.
 
Kifupi MO hawezi kuendesha club ya mpira wa miguu. Yeye anafikiri ukiwa na pesa tu unaweza kuamua chochote,wakati kujenga brand sio kazi nyepesi. Timu za wanachama au hisa zinahitaji Utaalam wa hali ya juu. Na principle Namba moja ni uwazi ,katika mikataba ya wachezaji ,ofa zinazokuja klabuni ,Matangazo ya biashara,mishahara yote, mapato na matumizi.n.k.
 
Mo naomba ajiuzuru turudi kule tulipotoka!

mishahara inayolipwa kwa wachezaji kwa mwezi mmoja si chini ya million mia mmoja hapo hujajumlisha safari kambi na viposho vya uendeshaji; club kama simba inahitaji si chini ya million 300 kujiendesha yenyewe. Kilomoni na genge lake wakabidhiwe timu tuone

yajayo yanafurahisha
Kwani simba imeanzishwa mwaka juzi? Kama hpn miaka yote iliwezaje kusajiri na kulipa mishahara? Au huyo mnyaturu alikuwa analipa yeye! Acha kujibu kishabiki tumia akili kidgo mtani
 
Huwa namshangaa sana MO jinsi anavyowekeza pesa yake SIMBA, MO angetakiwa asuke timu yake kama Bakressa.

Timu yenye asilimia 100 za umiliki wake, atumie hizo pesa zake ajenge bonge la uwanja, ashushe makocha na wachezaji wa viwango vya kimataifa.

Mashabiki wataongezeka tuu Man city, chelsea hazikuwa na mashabiki wengi hivi kabla hazijanunuliwa.

MO piga simba chini pesa uliyowapa mpaka sasa ifanye sadaka, tengeneza timu yako
Mbona hayo yote bakhresa kafanya niambie kapata nini? Usimba na uyanga ni kama kabila tunaambukiza mpaka na watoto wetu
 
Wana shangaza sana mkuuu.kazi kukodolea macho tuuu hisa za mo, miaka yote wapo na hatukuona chochotee cha maaana.

Nilishangaa kusikia kua hata ule uwanja wa bunju ni msaada toka kwa mkwele .

Izingatiwe kua hata hayo mabadliko ya mfumo wa clab yaliwezekana baada ya wale jamaaa kuwekwa rupango, lasivyo hadi leo ingekua bado ni ngonjeraa tuu.
Wao ndiyo wenye timu sasa huyo mo ni wakuja tu, hata serikali inalijua hilo ndiyo maana ili ingilia kati. Unadhani yale Maneno alizungumza Rostam yalikuwa ni yake? Alitaka afanye kama mo akastuliwa
 
Kwani simba imeanzishwa mwaka juzi? Kama hpn miaka yote iliwezaje kusajiri na kulipa mishahara? Au huyo mnyaturu alikuwa analipa yeye! Acha kujibu kishabiki tumia akili kidgo mtani
Timu itaendelea kuwepo; lakini kwa kusua kama ilivyokuwa zamani, rejea uongezi wa kina aveva mpaka rage uko nyuma. Madeni ya simba kudaiwa yalikuwa mengi, mpaka ajibu kwenda yanga alikimbia njaa za simba timu ilikuwa haina kitu, zama za timu kuendeshwa kienyeji zimeshapitwa na wakati ndio mana miaka yote iyo tulikuwa hatufanyi vizuri.

Matunda ya msimu mmoja tu yaliyotokana na uwekezaji sasa tunauwakilishi wa timu 4 CAF. Simba na yanga zikiebdeshwa kiswahili Swahili kama ulivyozoea uko nyuma soka la ushindani Africa hatutaliweza kiongozi.

Moo akiondoka ni disaster; japo mnapiga piga porojo. Ona Leo yanga inashindwa lipa mishahara ya wachezaji unafikiri ni kitu kizuri icho
 
Kwani simba imeanzishwa mwaka juzi? Kama hpn miaka yote iliwezaje kusajiri na kulipa mishahara? Au huyo mnyaturu alikuwa analipa yeye! Acha kujibu kishabiki tumia akili kidgo mtani
Wakati wote huo Simba ilikua na mafanikio gani? Hujui kuwa mfumo wa kiuchumi umebadilika! Hujui hata mfumo wa uendeshaji vilabu umebadilika?
 
Huu ndio wakati wenu kwenda kuongoza club, na tusipoona mafanikio yoyote hesabuni nyie ni wachawi wa maendeleo!! Hao wajumbe walishafanya kitu ipi toka simba ianze? Mwenye hisa 49 tunaona anachoweka je nyie wenye 51 mmeweka nini? Embu acheni uchawi nyie
Jiandaeni kushuka daraja msimu huu dogo, mwenzio kayoma kashajiunga na timu ya wananchi, unakaribishwa pia.
 
Hao wajumbe wanalipa mishahara ya wchezaji, tuanzie hapo... Kama mwenye kumiliki hisa 49% anaweka mezani bil 20 hao wanahisa wanaomiliki 51% wameweka ngapi nao mezani?
Piga "Cross Multiplication" hapo tuone wanatakiwa kuleta ngapi.
 
Back
Top Bottom