Uchaguzi 2020 Wajumbe wamezidi kuyeyuka na propaganda za maji taka

Uchaguzi 2020 Wajumbe wamezidi kuyeyuka na propaganda za maji taka

Ndugu zangu, hakika chama chetu kikongwe kimejaa propaganda za maji taka, makada walijitokeza na propaganda kuwa Lissu hawezi kurudi Tanzania,Lissu aliwathibitishia watanzania kuwa angerudi tu, wakabadili gia kuwa akirudi atakamatwa airport, Jamaa akarudi tena kwa kishindo wakashindwa kumkamata airport.

Wakasema Chadema haiwezi kumpa nafasi ya kugombea Urais maana Mbowe na Lema hawamtaki wanamtaka Lazaro, Chadema ikampa kugombea tena kwa kura nyingi sana. Wakasema tume lazima itamwengua maana ana kesi kwahiyo hatatoboa, akateuliwa kugombea.

Wakasema hana pesa za kufanya kampeni hawezi kuzunguka nchi nzima, leo yupo anazunguka kila kona tena kwa speed ya 5GB. Wakasema hata pata watu kwenye mikutano yake, sasa ni mafuriko.

Mgombea wao akawaambia wafuasi wake kwamba picha za mikutano ya Lissu ni za ku edit, wamegundua kuwa mgombea wao hakuwa sahihi wamekuja na propaganda mpya kuwa watu wanaojaa kwenye mikutano ya Lissu siyo wapiga kura kwa kuwa hawajajiandikisha ila wanafunzi na wale wanaojaa kwenye fiesta ndio wapiga kura. Hakika wajumbe wamezidi kuyeyuka na propaganda za maji taka. Mwaka huu kazi mnayo wajumbe,a.k.a makada a.k.a uvccm walioagizwa kujibu hoja.
Wanatafakari,Sasa ukweli waliokuwa wakiukataa.wameanza kuona jinsi maji yalivyowafika shingoni.
 
Hakunaga speed ya 5GB
Ni 5G yaani Fifth Generation.

Mkuu uwe makni
 
Jee unajua Lissu ilikuwa asirudi nchini hadi ahakikishiwe usalama wake?. Hakuhakikishiwa huo usalama!. Jee unajua ni nani alimshauri Lissu arejee tuu hivyo hivyo hata bila kuhakikishiwa usalama?.
Kamanda Lissu, Usisubiri Jibu la IGP Kuhusu Usalama Wako, Aliyekulinda na Shambulio Lile Yupo, Yeye Aweza, na Ataendelea Kukulinda, Welcome Back Home!
P
Pamoja ya kwamba tunatofautiana kimtazamo now days but hili bandiko lako limenifurahisha japo sijalisoma Bado.

Ila uncle kipindi Kama hichi ungekua huru kuchambua mwenende wa kampeni na uchaguzi kwa ujumla ila ndo hivo Tena umetunyong'onyeza saana ku declare Ni kada.😥😥😥
 
Huna lolote wewe , hivi ulijua Lissu anaweza kutishwa na vikelele vyako vya kizushi ? Never Ever ! Lissu siyo wa hivyo na nakuhakikishia Lissu anamuondoa Magufuli madarakani

Ila Pascal ndiye aliyemshauri Lissu agombee kupambana na Magu
 
[emoji23][emoji23][emoji23] Nilikuwa naongea na mdau mmoja , nikamuuliza kampeni za Jana airport Mbeya mjini zilikuaje, akanijibu walimu na wanafunzi walikuwepo pamoja na wafanyakazi wengine walikusanywa maeneo mbalimbali ya jiji na nje ya jiji,

Walimu na wanafunzi nao naona wanatafuta Uhuru kimyakimya watamchagua Lissu 28/10/2020.

Maendeleo hayana chama,
 
Back
Top Bottom