Wajuzi wa mambo ya ujenzi

Wajuzi wa mambo ya ujenzi

kikoozi

JF-Expert Member
Joined
Jun 24, 2015
Posts
2,094
Reaction score
3,108
Habarini ndugu zangu,

Nataka kuanza kujenga nyumba ya kuishi, maeneo ni Dar es Salaam, naombeni mbinu bora ya kufanya ujenzi katika angle ya kuwalipa awa mafundi ujenzi, kuna fundi nimeongea nae kuhusu kuniwekea msingi tu wa mita 12 kwa 12 aliniambia almost milion 1.8 nimechoka na kuchoka wakuu.

Maana mimi uko sikufikiria kabisa, ebu nipeni njia bora ambayo wenzangu mnatumia kujenga kwa ubora na unafuu ukianzia na msingi kisha kupandisha nyumba.
 
Hebu weka vizuri taarifa, hiyo 1.8m ni msingi au nyumba kujengwa mpaka lintel?

Materials yote ushanunua? Sand, Aggregates, blocks, Cement

Tupatie taarifa sahihi ili tukusaidie ikibidi fundi nae tukupatie maana unaweza kulalamika hiyo 1.8m wakati unajenga ghorofa au eneo lako lina bonde n.k
 
Hebu weka vizuri taarifa, hiyo 1.8m ni msingi au nyumba kujengwa mpaka lintel?
Materials yote ushanunua? Sand, Aggregates, blocks, Cement,
Tupatie taarifa sahihi ili tukusaidie ikibidi fundi nae tukupatie maana unaweza kulalamika hiyo 1.8m wakati unajenga ghorofa au eneo lako lina bonde n.k

Sent from my SM-G610F using JamiiForums mobile app
Mkuu aliniambia hiyo ni gharama ya ufundi wa msingi wa nyumba tuu, ni nje ya material (namaanisha material ni juu yangu ni nje ya hiyo 1.8M)
 
Wewe unataka watu wakudanganye ukweli hiyo hela sio nyingi inategemea naeneo husika kuna sehemu msingi unajengwa kwazaidi yahiyo wambie watu eneo lako liko wapi au likoje hapo wanaweza kukusaidia
Kiwanja kipo Mbezi, tambalale.
 
iyo mkuu aliniambia ni gharama ya ufundi tuu material ni juu yangu
Jihadhari usipotoshwe na watu humu, bei hiyo ikiwa ni fundi mzuri mchukue lakini afanye haya;
1. Kwenye msingi amimine ka zege angalau inch 2
Ndipo aanze kujenga tofali
2. Pili kiuno cha msingi akuwekee beam asuke nondo 3 au 4 na amimine zege ya sakafu/floor

Bei sio kubwa kwa fundi mzuri.
Usikimbilie bei nafuu halafu nyumba ije kupasuka utaingia gharama kubwa. Wabongo wanapenda vitu vizuri kwa macho visivyo na ubora, chukua tahadhari.
 
Jihadhari udipotoshwe na watu humu, bei hiyo ikiwa ni fundi mzuri mchukue lakini afanye haya;
1. Kwenye msingi amimine ka zege angalau inch 2
Ndipo aanze kujenga tofali
2. Pili kiuno cha msingibakuwekee lenta/prince beam na amimine zege ya sakafu/floor

Bei sio kubwa kwa fundi mzuri.
Usikimbilie bei nafuu halafu nyumba ije kupasuka utaingia gharama kubwa.
Wabongo wanapenda vitu vizuri kwa macho visivyo na ubora chukua tahadhari
Asante mkuu kwa ushauri wako mzuri
 
Kama ni nyumba ya vyumba vitatu jiko na vyoo ndani andaa tofali 2,500 mawe trip 9 hizi Lori za size 4.5 mchanga, halafu tafuta million 1.2 unapata fundi anakujengea kuanzia msingi hadi kunyanyua boma lote, material na gharama za ufundi zitaangukia kwenye Kama 6M inabaki kupaua tu na kuendeleza jengo unajikusanya tena, achana na huyo fundi wa 1.8M kwenye msingi tu atakutapisha damu.
 
Kama ni nyumba ya vyumba vitatu jiko na vyoo ndani andaa tofali 2,500 mawe trip 9 hizi Lori za size 4.5 mchanga alaf tafuta million 1.2 unapata fundi anakujengea kwanzia msingi had kunyanyua boma lote material na gharama za ufundi zitaangukia kwenye Kama 6M inabaki kupaua tu na kuendeleza jengo unajikusanya tena achana na huyo fundi wa 1.8M kwenye msingi tu atakutapisha damu
Wengi ni wapotoshaji tu.
Mmeona ramani ya nyumba?
Unapata wapi uhalali wa kuchangia kwa ujasiri hivi ilhali hujui chochote?
Unalinganishaje na ujenzi wako?
Mbona hamuongelei ubora?
 
kiwanja kipo mbezi, tambalale
Mbezi Luis? Angeweza akapunguza kidogo japo bado sina uhakika sana na hiyo tambalale kama hivyo unavyoielezea kama itaendana na ujenzi, mimi nikukumbushe kidogo ujenzi wa maeneo mengi ya Mbezi Kimara na sehemu zinazokaribiana na hapo ni maeneo magumu kwenye ujenzi, wakati ukitafuta unafuu ukumbuke na ufanisi tunajua ugumu wa kudunduliza, usikurupuke usije ukaumia.
 
Karibu mkuu, lakini pia muombe punguzo hadi 1.5ml kama ataridhia lakini epuka kuambiwa upewe fundi mwingine unaweza kujutia ushauri huo.
Hapa watu wanatafutiana kazi nawajua wabongo wengi wapo kimaslahi
Umesema vizuri kikubwa hapo ni uhakika wa huyo fundi na kazi yake.
 
Back
Top Bottom