Wajuzi wa mpira, nini sababu ya Simba kufungwa na Al Ahly?

Wajuzi wa mpira, nini sababu ya Simba kufungwa na Al Ahly?

Mpira wa jana ni bahati ndio imeamua mpira Al Ahly walikua Unga sana jana aisee Simba wangekua makini walikua wanatupia goli nyingi sema ndio hivyo wao mechi za kina Galaxy wanatulia kweli wakina Chama unaona wanapiga pass sahihi ila wakicheza na Timu nzuri tu wanapotea sehemu ya kutoa pass wao wanapiga na sehemu ya kupiga wanatoa pass...angalieni mpira leo saa kumi Mazembe vs Petro muangalie watu wanaojua mpira sio kubahatisha Inonga yupo peke yake anataka kumfunga kipa wake...
 
The ultimate reason ya simba kufungwa ni kipa kushindwa kudaka mpira uliolekezwa kwake na mu-al ahly mmoja
 
Binafsi niliona matatizo yafuatayo.
~Simba hawana clinical number 9
~Wachezaji wa simba ni wagumu kufanya maamuzi ya haraka kwenye maeneo ambayo inahitajika kufanya hivyo.
~Simba wachezaji wengi umri umewatupa mkono
~Bado Simba tuna tatizo la kupoteza mipira kizembe tena kwenye maeneo hatarishi.
~Simba tuna changamoto kwenye eneo zima la kiulinzi.
~Simba hawapo vizuri kwenye kutumia ipasavyo mipira iliyokufa pamoja na kona
~mastrika wa simba wanahitaji walau chance nyingi ili wafunge goli moja.
NINI KIFANYIKE CAIRO?
~Wawaheshimu Al ahly kwa kukaba zaidi then watumie kaunta kupata goli na washikilie bomba kwelikweli,kinyume na hapo habari yetu ndio imeisha hapa
Number 9 sio tatizo kama timu inaweza kufunga kutokea popote issue ni quality ya wachezaji mechi ya Jwaneng mbona hakukua na hizo lawama za number 9?
 
Kweli kabisa.
Mdomo kaka,hawa makolo walishadadia mambo ya mamelodi kuliko kujiandaa kuukabili mchezo wao na al ahly,kingine hizi mechi za mtoano watu timu haziangalii takwimu Bali wanaangalia ushindi wa magoli.

Hizo takwimu za umiliki za Simba usifikirie kuziona Cairo maana mametumia nguvu nyingi Sana lakn wamepigwa kwahy automatically miili imechoka na watawenda Cairo kukamilisha ratiba tu.
 
Wadau wa Soka na wapenzi wa SIMBA poleni sana kwa kilichowapata jana.

Nimeona takwimu za Mchezo wa Jana SIMBA imeongoza sehemu kubwa lakini ikafungwa.

JE nini SABABU za SIMBA KUFUNGWA? Inawezekana ikawasaidia Mechi yao huko MISRI.
Bahati
 
Ahly hawako vizuri ila ubovu wao si uzuri wa Simba, Ahly na mpango mkakati wao ndio ume amua mechi.
Ahly kama wangekua hawajapata goli wangewalazimisha Simba kwa namna wanavyo taka mpaka wangepata goli.

Kwakua walishapata goli waka amua wakabie kuanzia kati apo ndipo Simba walionekana wakishambulia kwa muda mwingi.
Angalia Dk 15 za mwisho, Ahly wakaingiza watu wakae na mpira waimalize mechi na wakafanikiwa.

Mechi ya Cairo, Ahly wata anza kushambulia kwa kasi kubwa na ndani ya dk 15 wakipata goli watarudi na kucheza kama Dar, wakikosa goli wataendelea kushambulia mpaka wapate goli baada ya goli wata waacha simba wacheze.
Dk 15 za mwisho watakaa na mpira na kumaliza gemu.
Simba ili wafanikiwe kupunguza shida mechi ijayo pale mbele waanze na vijana wenye kasi hasa pembeni vijana watakao weza kukimbia kushambulia na kurudi kusaidia kwenye kiungo na beki za pembeni

Washambulie kwa kushtukiza yaani pasi zisizidi tatu kutokea kwenye transition wanaweza pata kitu kwakua muda mwingi eneo lao la kuzuia litakua na namba kubwa.
 
Simba hata wangefunga bado Ahly wangeongeza,mashambulizi ya Ahly yalikuwa clinical ukilinganisha na Yale ya Simba
 
Simba hata wangefunga bado Ahly wangeongeza,mashambulizi ya Ahly yalikuwa clinical ukilinganisha na Yale ya Simba
Ahly ndivyo wa chezavyo wakiwa ugenini, wanatafuta sare/suluhu ukilegea wanakufunga na uo ndio mpango wao wa miaka yote.
Ukiwatangulia kwa goli watahakikisha wana sawazisha na ndio msingi wa kutamba kwao katika soka la Afrika.
 
Number 9 sio tatizo kama timu inaweza kufunga kutokea popote issue ni quality ya wachezaji mechi ya Jwaneng mbona hakukua na hizo lawama za number 9?
Sidhani kama jwaneng galaxy ni sample sahihi,Jwaneng hawana ubora kiasi kwamba wanaweza kupishana na simba,japo sio wabovu

Kwenye level kama hizi hasa mtoano,inatakiwa timu iwe imekamilika kila idara walau kwa 90% kitu ambacho kwa simba hakuna.

Naungana na wengine waliosema UTOFAUTI WA UBORA BAINA HIZI TIMU MBILI NDIO ULIOAMUA MATOKEO.
 
Ahly ndivyo wa chezavyo wakiwa ugenini, wanatafuta sare/suluhu ukilegea wanakufunga na uo ndio mpango wao wa miaka yote.
Ukiwatangulia kwa goli watahakikisha wana sawazisha na ndio msingi wa kutamba kwao katika soka la Afrika.
Uko sahihi hawajawahi kucheza tofauti na walivyocheza jna sema nao pale kwa Modeste naona wamepigwa jamaa hana speed na Wala sio katili la hasha Jana wangepata goli tatu clear
 
Kuna mtu alisema al ahly anapigwa 4 nikajiuliza Al ahly imekuwa mbovu kuliko singida big stars
 
Mashabiki wa Simba kwa kujifariji. Eti kuishambulia sana Al Ahly jana na kuongoza possession basi wanajiona wao ni bora zaidi. Hawajui kuwa lengo la Al Ahly lilikuwa ni kulinda goli lisisawazishwe na hakika lengo lao lilifanikiwa.
 
Back
Top Bottom