WAJUZI: Wachezaji Wanavaa au Kufunga nini Mkononi wakati wa Mechi

WAJUZI: Wachezaji Wanavaa au Kufunga nini Mkononi wakati wa Mechi

MoroGent

Senior Member
Joined
Jan 10, 2018
Posts
149
Reaction score
473
Salam sana Wanajukwaa,
Niende moja kwa moja kwenye mada. Nikiri mimi ni mpenzi wa mprira wa miguu, naangalia mechi za club za ulaya, Kimataifa na za Nyumbani apa NBC. Kwa muda mrefu nimekuwa nikichunguza hili jambo kwa muda mrefu na kuuliza watu kwamba ina maana gani, nimekosa majibu rasmi na ya uhakika.
Kuna hii sijui niseme ni tamaduni au tabia ya wachezaji, sio wote ila ni wengi wao kufunga vitu kama BANDEJI au Tape au sijui niseme VINGUO😀😀 sijui niiteje, lakini huwa wanafunga mkononi au kwenye vidole wakati wa mechi, kisha wakati wa kutolewa nje anavifungua na kutupa uwanjani wakati anatoka.
Mfano mzuri ni kwa bongo ni Cota Chama yeye hufunga mikono yote miwili, Bacca na Mudathir wanafunga kwenye vidole, na wengine wengi hufunga uwanjani. Nilijua ni bongo tu, kumbe hata ulaya, ama itakumbuka ZIDANE alipompiga kichwa mwenzake na akatolewa kwa red card alionekana akitoka uwanjani akiwa anafungua hicho kibandeji cheupe mkononi na kukitupa.
Nikiuliwa walio wengi husema ni urembo tu, au utamaduni wa kurithi au kuoga, wengine husema ni imani za kismart.
Hivyo nimekuja kuuliza wafuatiliaji wa michezo, je hii kitu ina maana gani kwa wachezaji na mpira kwa ujumla, je kiko oficial na kinatambulika.
Naomba elimu kuhusu hili.
Naomba kuwasilisha.
 
BENZEMA Anafunga kwa sababu kateguka kidole chake wengne sijafuatilia
 
Wengi wao huwa wanafunika pete za ndoa.
 
Back
Top Bottom