Wakati China ikijitahidi kujenga jumuiya ya binadamu yenye hatma ya pamoja, Marekani inadhuru maslahi ya nchi nyingine ili kujiendeleza

Wakati China ikijitahidi kujenga jumuiya ya binadamu yenye hatma ya pamoja, Marekani inadhuru maslahi ya nchi nyingine ili kujiendeleza

ldleo

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2010
Posts
1,116
Reaction score
1,121
src=http___p9.itc.cn_q_70_images03_20210527_f1ce240ac90544b7a24a63e38989d63b.jpeg&refer=http__...jpg
Shirika Kuu la Utangazaji la China (CMG) limetoa tahariri ikisema, wakati China inapohimiza ujenzi wa jumuiya ya binadamu yenye hatma ya pamoja, Marekani inanyakua nafasi ya maendeleo ya nchi nyingine ili kujiendeleza zaidi.

Hivi karibuni, Waziri wa mambo ya nje wa China Wang Yi alihudhuria Mkutano wa Usalama wa Munich na kusisitiza kuwa, China haidhuru maslahi ya nchi nyingine wakati inapojiendeleza. Wang alisema maendeleo ya China hayagharimu maslahi ya nchi nyingine, na badala ya kufanya hivyo, China inazingatia sana kushirikiana na nchi nyingine ili kupata mafanikio kwa pamoja. Amesema mchango wa China kwa ukuaji wa uchumi wa dunia umezidi asilimia 30 kwa zaidi ya miaka 10 mfululizo.

Tangu mwaka 2008, China imepokea asilimia 25 ya mauzo ya nje ya bidhaa za nchi zilizoko nyuma zaidi kimaendeleo, na pia ni nchi iliyotekeleza kivitendo zaidi pendekezo la kuchelewesha malipo ya madeni ya nchi hizo ikilinganishwa na nchi nyingine za Kundi la Nchi 20. China pia imeandaa Maonesho ya Bidhaa Zinazoagizwa Kutoka Nchi za Nje kwa miaka mitatu mfululizo. Tangu kutolewa kwa pendekezo la “Ukanda Mmoja, Njia Moja”, China imefanya uwekezaji wa zaidi ya dola bilioni 110 za kimarekani kwa nchi za nje, na thamani ya biashara kati yake na nchi nyingine zilizojiunga na pendekezo hilo imezidi dola trilioni 7.8 za kimarekani. Licha ya hayo, China inajitahidi kufungua mlango zaidi, ili nchi nyingine zinufaike na soko lake kubwa.

Kwa upande mwingine, Marekani, ikiwa nchi iliyoendelea zaidi duniani, imedhuru maslahi ya nchi nyingine mara kwa mara ili kujipatia maendeleo. Rais wa awamu iliyopita ya nchi hiyo Donald Trump anayejulikana kama mmoja wa marais wakubwa na wenye ushawishi zaidi katika historia ya Marekani, alikuwa anadai “Marekani Kwanza” siku zote, na kutanguliza maslahi ya Marekani mbele ya maslahi ya nchi nyingine. Ili kulazimisha pande nyingi zitoe upendeleo kwa Marekani, serikali ya Trump ilijitoa kwenye makubaliano mbalimbali yakiwemo Makubaliano ya Uhusiano wa Wenzi wa Kuvuka Pasifiki CPTPP na Makubaliano ya Paris kuhusu mabadiliko ya tabianchi, na pia ilijitoa kwenye mashirika mbalimbali ya kimataifa, ikiwemo Shirika la Afya Duniani WHO, na Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa. Zaidi ya hayo, Marekani ilianzisha vita ya kibiashara dhidi ya nchi nyingi haswa China.

Sera ya “Marekani Kwanza” si kama tu inalenga nchi zilizoendelea na nchi zinazoibuka kiuchumi, bali pia inatekelezwa katika uhusiano kati ya Marekani na nchi zinazoendelea. Katika suala la biashara na nchi za Afrika, Marekani inatumia njia ya “Karoti na Fimbo”, na kuzilazimisha nchi hizo kuridhia makubaliano ya kibiashara yasiyo na haki na usawa kupitia Sheria ya Ukuaji na Fursa Afrika (AGOA).

Kwa muda mrefu, nguo za mitumba kutoka nchi za magharibi haswa Marekani zimejaa kwenye soko la Afrika, na kuleta athari kubwa kwa maendeleo ya sekta ya nguo barani humo. Katika miaka ya hivi karibuni, nchi za Afrika Mashariki zikiwemo Kenya, Tanzania, Rwanda na Uganda ziliamua kuongeza ushuru wa forodha kwa nguo hizo. Lakini uamuzi huo umepingwa vikali na Marekani, ambayo ilitisha kusimamisha AGOA kwa nchi hizo. Hatimaye nchi hizo za Afrika zilirudi nyuma na kufungua tena soko lake kwa nguo za mtumba za Marekani. Rosa Whitaker aliyekuwa mshauri mwandamizi wa serikali ya Marekani anayeshughulikia biashara na Afrika amesema, Marekani imefanya umwamba katika jambo hili, na “waafrika wanafuatilia, wanashangazwa na wanakasirika”.

Tangu serikali mpya ya Marekani iingie madarakani, nchi hiyo imerejea kwenye baadhi ya mashirika na makubaliano ya kimataifa, lakini haijaacha sera ya “Marekani Kwanza”. Katika suala la biashara, serikali ya Joe Biden ilirithi msimamo wa serikali ya awamu iliyopita, na kuendelea kutoza ushuru wa nyongeza kwa bidhaa za nchi za nje. Ili kuendeleza uchumi, Marekani imechapisha na itachapisha dola nyingi zaidi, ambazo zitaleta mfumoko mkubwa wa bei duniani, na “kutega bomu” kwa uchumi wa dunia.

China inapendekeza kujenga jumuiya ya binadamu yenye hatma ya pamoja, na kujitahidi kushirikiana na nchi nyingine ili kupata maendeleo ya pamoja, lakini wakati huohuo, Marekani ikichukua bendera ya “Marekani Kwanza”, inacheza “michezo ya sifuri”. Marekani inapaswa kurekebisha makosa yake mapema, na kubeba majukumu ya kulinda maslahi ya binadamu wote.
 
Hivi ndivyo vyakula vya ubongo wa Great thinker sasaa.Wakati huu China inapotuongelea katika fikra za kutukwamua kwani na Africa yenyewe inaelewa?Inasemaje pia! Africa inafanyaje kukazia hapa walipoanzishiwa kujielewa? Africa tunapiganiwa huko,sisi yaani kichwani yanapitapita mengi lakini ukija kuangalia Tanzania yako ambao wapo front kukupigania ndo hao hapo.[emoji23][emoji23][emoji23].
 
Japo madai ya bidhaa za China yapo chini ya kiwango, it's ok! Lakini hebu tujaribu kufikiria sisi Kama Africa Lau Kama si China product tungekuwa wapi wakati huu?

Najaribu kufikiria ajira za vijana hapa kwetu Tanzania za uendeshaji wa Pikipiki za abiria nadhani Ni elfu kadhaa, hii imekua faida kwao wenyewe hao vijana maarufu bodaboda, familia zao, wananchi ambao Ni abiria, pamoja na serikali na taifa kwa ujumla.

Najaribu pia kuwaza ni bidhaa gani ya marekani ambayo imekua msaada kwa taifa letu nakosa, najaribu kufikiria Ni kampuni gani ya kiuwekezaji ya marekani imekua na maslahi ya moja kwa moja na taifa letu kwa Sasa nakosa!

Lakini kwa China tunaweza kuongea kinyume chake.

Kwa hio mtazamo wangu China Ina hoja.
 
Japo madai ya bidhaa za China yapo chini ya kiwango, it's ok! Lakini hebu tujaribu kufikiria sisi Kama Africa Lau Kama si China product tungekuwa wapi wakati huu?

Najaribu kufikiria ajira za vijana hapa kwetu Tanzania za uendeshaji wa Pikipiki za abiria nadhani Ni elfu kadhaa, hii imekua faida kwao wenyewe hao vijana maarufu bodaboda, familia zao, wananchi ambao Ni abiria, pamoja na serikali na taifa kwa ujumla.

Najaribu pia kuwaza ni bidhaa gani ya marekani ambayo imekua msaada kwa taifa letu nakosa, najaribu kufikiria Ni kampuni gani ya kiuwekezaji ya marekani imekua na maslahi ya moja kwa moja na taifa letu kwa Sasa nakosa!

Lakini kwa China tunaweza kuongea kinyume chake.

Kwa hio mtazamo wangu China Ina hoja.
China imechangia kushusha gharama za bidhaa kwa Afrika lakini hiyo si nchi pekee ambayo imefanya hivyo. Kuna nchi nyingine pia zimehusika hasa India bila kusahau Japan.

Ukizungumzia pikipiki za abiria hauwezi kusahau kampuni za uzalishaji wa bidhaa hizo kutoka India kama vile Bajaj. Hii ni kampuni ambayo imefanya biashara na Afrika kwa miaka mingi sana. Bila kusahau kampuni nyinginezo kama Tata na Eicher Motors.

Kampuni kama Honda, Suzuki na Toyota kutoka Japan pia zinachangia kwa kiasi kikubwa sana katika sekta ya usafirishaji barani Afrika. Sidhani kama kuna mtumiaji wa vyombo vya usafiri katika bara la Afrika asiyezifahamu hizo kampuni.

Marekani je?

Kuna mtu humu jukwaani asiyezifahamu kampuni kama vile Google, Microsoft pamoja na Facebook? Au kuna mtumiaji wa kompyuta asiyezifahamu brands kama Dell, HP pamoja na Apple? Kwa asiyefahamu, hizo ni kampuni za Kimarekani na zimefanya uwekezaji mkubwa tu barani Afrika.

Maswali mengine machache: kuna mwanamitindo ama mwanamichezo barani Afrika asiyezifahamu Nike, Converse pamoja na Calvin Klein? Unafahamu kuwa Nike inatajwa kama kampuni pendwa zaidi barani Afrika hivi sasa? Hizo zote ni za Kimarekani.

Usisahau kampuni kubwa za vinywaji duniani kama vile Coca-Cola, Pepsi na kampuni tanzu zao kama Mirinda, Fanta, 7 Up, Dasani, Mountain Dew n.k. Pepsi pekee ina assets ama brands zake zaidi ya 100 duniani kote ikiwemo Afrika. Wote huo ni uwekezaji wa Marekani ambao umekuwa na faida kwa uchumi wa Afrika.

Bado hatujazungumzia misaada kupitia mashirika ya Kimarekani kama vile USAID. Haya mashirika yamegusa sekta nyingi barani Afrika zikiwemo: afya, elimu, nishati, viwanda, usafirishaji na kadhalika.
 
baniani mbaya kiatu chake dawa,tuchukue mazuri yao,mabaya yao tuwaachie...
 
lazima na sisi tufikirie huu urafiki wa kinafiki kati ya china na africa. haiwezekani urafiki wa africa na china utazamwe katika nyanja za uchumi na miundo mbinu tuu lazima pia tutazame ongezeko la wachina africa nalo linatisha sana.
 
Back
Top Bottom