Wakati dunia inapigana na ukatili kwa watoto ikiwemo viboko mashuleni, Tanzania ukatili wa watu wazima unafanyika hadharani

Wakati dunia inapigana na ukatili kwa watoto ikiwemo viboko mashuleni, Tanzania ukatili wa watu wazima unafanyika hadharani

Sky Eclat

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2012
Posts
57,761
Reaction score
216,011
Hii tabia ya viongozi kuchapa raia viboko ni udhalikishaji na ukatili unaopaswa kukemewa kwa nguvu zote. Ki tendo cha kumpigia viboko mtu mzima hadharani ni kumshushia thamani na utu wake. Maafa ya kisaikolojia atakaa nayo mtu yule kwa muda mrefu na wengine hatutaelewa wameathirika kiasi gani.

Hivi tukifunga milango na kuwachapa bakora hawa viongozi. Kama wanategemea polisi mpaka polisi wafike tumesha walamba bakora za kutosha. Kutoka hapo tutaheshimiana.

Watoto wa masikini hao mnaowapa elimu bure mna wachapa vya kutosha. Na sasa mmeamua kuwachapa wazazi wao. Shule zinazo jielewa zimesha achana na adhabu za viboko leo mnapiga viboko watu wazima hadharani.

Tukifurahia maafa ya viongozi mnatuona wabaya wakati chuki mnaitengezeza wenyewe.
 
Sio kuwajibishwa tu ila na wao wachapwe hadharani, hii nchi inaendeshwa kwa sheria si mihemko ya watu.
Afu mm siwez kukubali nilale unichape hata unipige risasi lakin siwez kuchapwa hadharani.
Wale wanachapwa idadi yao kubwa ni wale wanyonge,
Sijaona mtu anayejitambua akipigwa,labda kwa msaada wa Polccm.
 
Sio kuwajibishwa tu ila na wao wachapwe hadharani, hii nchi inaendeshwa kwa sheria si mihemko ya watu.
Afu mm siwez kukubali nilale unichape hata unipige risasi lakin siwez kuchapwa hadharani.
Unarudi nyumbani unamwambia mke wako nimetoka kucharazwa bakora.
 
Wale wanachapwa idadi yao kubwa ni wale wanyonge,
Sijaona mtu anayejitambua akipigwa,labda kwa msaada wa Polccm.
Kabisa mm huwezi nichapa hadharani tena mbele ya vyombo vya habari athari zake ni kubwa sana asikwambie mtu.
 
Hapo raia nae akimchenjia kumchapa mangumi huyo kiongozi hadharani ita kuwaje na waziri washeria ilitakiwa atoe ufafanuzi wa hili la wananchi kuchapwa viboko hadharani
 
Hao viongozi wafukuzwe!! Kwangu nisingekubali eti mkuu wa wilaya au mkoa anipige viboko ,haitowezekana kama nimekosa anipeleke mahakamani na si kunipiga vibok otherwise yatatokea ya Kleruu na mwamwindi.
 
Wale wanachapwa idadi yao kubwa ni wale wanyonge,
Sijaona mtu anayejitambua akipigwa,labda kwa msaada wa Polccm.
Atapigwaje anayejitambua...... Wakati mwingine na Njaa na kukosa Utu nayo kunachangia
 
Unarudi nyumbani unamwambia mke wako nimetoka kucharazwa bakora.
Hahahahaaaa,... unajua jana nimeangalia ile clip nikajichukulia ndio mm asee yule mama ananichapa bakola aseee angekula RKO moja akashuka nayo ardhin akizinduka adabu atakuwa nayo.
 
Hahahahaaaa,... unajua jana nimeangalia ile clip nikajichukulia ndio mm asee yule mama ananichapa bakola aseee angekula RKO moja akashuka nayo ardhin akizinduka adabu atakuwa nayo.
Hata kama watakuweka mahabusu lakini utakua umefikisha ujumbe.
 
Hii ndiyo sheria inavyo sema? Tukiwachapa nyinyi viboko kwanza tutaanza kuheshimiana.
Nimekuzoea kwa maneno yako ya Hovyo..... Hivi kile walichofanya mpaka kupelekea kupigwa Viboko wewe Hamnazo Unaona ni sahihi?
 
Hapo raia nae akimchenjia kumchapa mangumi huyo kiongozi hadharani ita kuwaje na waziri washeria ilitakiwa atoe ufafanuzi wa hili la wananchi kuchapwa viboko hadharani
Huyo mwananchi atakae wekwa mahabusu kwa kumchapa mkuu wa Wilaya au Mkoa tutamtafutia msaada wa kisheria.
 
Atapigwaje anayejitambua...... Wakati mwingine na Njaa na kukosa Utu nayo kunachangia
Ni kweli Mkuu unajua sawa wanaweza kuwa wamekosea lakin adhabu iliyotumika si sawa.
Utu ni jambo la kwanza pia itambulike hata hao wanaowahukumu wenzao si kwamba ni wasafi bali mabaya yao hayakajulikana tu.
 
Siku watakosea watapata kilema cha kudumu na hapo ndio litakuwa fundisho.
Sielewi maana ya kuwa na mahakama au polisi
 
Back
Top Bottom