UHURU JR
JF-Expert Member
- Jul 24, 2014
- 16,543
- 7,880
Hebu weka sentensi iliyonyooka!! Yaani unadai wanasema unaweza ukachanja, na chanjko ikawa active na bado ukaweza kuwa infected?! Unaweza kutoa reliable source ya maelezo yako?! Na hapa kaa ukifahamu kwamba, hata huko ilikoonekana haisaidii kwa wazee sio kwamba chanjo kama chanjo haifanyi kazi bali side effects za chanjo zinakuwa hazihimiliki kwa watu wazee, especially wenye umri kuanzia miaka 80!!
Let's be reasonable! Kwenye screenshot ambayo niliweka awali inasema kwamba, South Africa yenye watu takribani 60M huku ikiwa imepima takribani watu 9M; watu 1.5M walipatikana na corona!!
Aidha, Italy ambayo na yenyewe ina watu takribani 60M sawa na SA lakini ikiwa imepima watu 41.3M, miongoni mwao takribani watu 3M wameonekana wana corona!!! Kwahiyo unataka kusema wakati nchi moja ya Afrika imepima watu 9M na kukuta 1.5M wana maambukizi; hii nchi maambukizi yake yapo chini kuliko nchi iliyopima watu 41.3M na kukuta ni 3M ndio wenye maambukizi?
Yaani unataka kujiaminisha Afrika haiathiriki kwa sababu tu cases zilizopatikana Ufaransa ni 3.8M huku Nigeria yenye idadi ya watu zaidi ya mara 3 ya Ufaransa ikiwa na cases 157,000 huku ukisahau Ufaransa imepima takribani watu 54M huku NIgeria ikiwa imepima less than 1.6M!!!!
Ina maana argument yako ndo ina-base hapo?!!
Anzeni kutamba kwamba Waafrika wana kinga endapo tu kutafanyika mass testing lakini sio hata kupima kwenyewe hatupimi halafu tunasema Afrika hatuathiriki sana!!! Kwa kutumia takwimu zipi?! Hata hiyo Marekani inayoonekana imeathirika zaidi ni kwa sababu US wanapima sana watu wao!! Wakati janga la corona linaanza, Urusi ilionekana ni miongoni mwa nchi ambazo hazikuwa zimeathirika sana! Walipokuja kufanya mass testing, total number of cases ikawa ina-shoot siku hadi siku!!
COVID-19 Vaccination
COVID-19 vaccines protect against COVID-19. Get safety info and more.
Naposema afrika haijathirika sana nina maana ya vifo na watu wengi kuuguwa hiyo corona ,kwa hali ya huduma zetu za afya basi hivyo vitu vingeonekana tu wazi na ndio maana watu hujaribu kuelezea kwanini hatujaathirika sana.