Wakati hadi Ethiopia wanafanikiwa kupanda miti bilion 20 kwa miaka 4 sie huku tunaendekeza tu wafugaji kukata miti

Wakati hadi Ethiopia wanafanikiwa kupanda miti bilion 20 kwa miaka 4 sie huku tunaendekeza tu wafugaji kukata miti

Lord denning

JF-Expert Member
Joined
Jun 3, 2015
Posts
15,819
Reaction score
33,255
Maisha ni mipango. Na kila aliyefanikiwa leo ujue alipanga na kutekeleza mipango yake vizuri siku nyingi nyuma

Leo Ethiopia wametangaza kutimiza malengo yao waliyojiwekea mwaka 2019 kupanda miti billion 20 ifikapo mwaka 2022

Kati ya nchi ambazo sasa zimekuwa na hali nzuri ya hewa iliyoanza kuwapa mvua nyingi na mazao ya kutosha ni Ethiopia.

Sasa Ethiopia sio tegemezi wa chakula tena kama ilivyokuwa miaka ya 1980 na 1990 kutokana na mipango yao ya kuamua kwa dhati kupanda miti iliyoanza kuwapa mvua nyingi na za kutosha kuwezesha kuzalisha chakula cha kutosha na kufanya kilimo vizuri

Kwa huku Tanzania tuna Wizara ya Mazingira ambayo viongozi wake hawajulikani kama wapo kazini kweli au wapo kupata hela tu maana hatuoni hata mkazo wa kuondoa Jamii za kifugaji kwenye misitu yetu ambayo sasa inateketea kila kukicha

Hatuoni hata jitihada zenye userious katika kuhamasisha upandaji wa miti kwenye maeneo yetu zaidi watu kila siku kuharibu miti na misitu tu

Kwa sasa Tanzania tumeanza kupata mgao wa umeme kutokana na ukosefu wa mvua ambao unasababishwa kwa kiasi kikubwa na uharibifu wa mazingira ila kwa upoyoyo wetu kuendekeza ujinga itafika kipindi tutakosa vote chakula na umeme kwa kutokuwa serious kuyatunza na kuyalinda mazingira.
Screenshot_20221119-193326_Chrome.jpg
 
Kwa jinsi hii nchi ilivyoharibiwa akili na CCM, huenda miaka 10 ijayo tukawa ni nchi inayoongoza kwa jangwa hapa Afrika.
CCM ni wapuuzi sana.
Miaka 10 mingi sana. Mingi sana 7 tu Kama hatua hazihachukuliwa tumeumia vibaya sana
 
Huko kuna kitu kinaitwa FARM AFRICA watu wa Dareda na Babati wanajuwa hii kitu.....DISIPILINI ya Forest Conservation Ethiopia ni ya kiwango cha juu....
 
Siku uharibifu wa mazingira utakapo tishia kuiondoa ccma madarakani ndio watakua serious na ishu za mazingira..sasahivi wacha waendelee kupambana na wapinzani.

Ccm ni laana.

#MaendeleoHayanaChama
 
Tatizo la Tanzania ni siasa na wanasiasa

Wafugaji wakikabwa, kuna watao watetea.

Ukizuia Mkaa kuna wataolalamika

Yahitajika maamuzi magumu mno
 
Hakuna kampeni waliyoifanya ccm wakafanikiwa haipo, lazima wananchi kuamka na kuchukua hatua wao wenyewe kuwategemea ccm ni kupoteza muda,
 
Pesa wanazo waanzishe hata kampeni ya “ Panda mti kwa uhai wa Tanzania “ hapo itatafutwa spicie yakupandwa kulingana na mazingira na miti ya kutiliwa mkazo iwe ile ya rafiki kwa vyanzo vya maji, miti ya matunda na miti ya mbao
 
Nimeona wafungwa wanakata miti na askari magereza.
 
Kampeni hiyo itasimamiwa kuanzia ngazi ya mtaa hadi taifa yaani mtaa kiongozi wa mtaa ahakikishe kila kaya ina miti minne au mitano ya matunda kwanza, halafu kila mwenye shamba ahakikishe shambani kwake amepanda miti pendekezwa kumi na tano walau kuzunguka eneo na ikizidi ni sawa tu
 
Miti itakua na ukaguzi wa kila jumamosi yaani kuanzia mtaani na wakuu wa wilaya na mikoa wawekewe malengo ya miti bilionj moja kwa walau kila mkoa
 
Siku uharibifu wa mazingira utakapo tishia kuiondoa ccma madarakani ndio watakua serious na ishu za mazingira..sasahivi wacha waendelee kupambana na wapinzani.

Ccm ni laana.

#MaendeleoHayanaChama
🤣🤣
 
Wataalamu waelimishe wananchi umuhimu wa miti kwa mfano muda huu kwenye mvua ndio kipindi kizuri cha kupanda miti kwani maji ya mvua yapo mengi, lakini hakuna ubunifu mijamaa ipoipo tu hakuna kampeni ya kimaendeleo waliyofanikiwa wanawaza kupiga pesa tu basi
 
Maisha ni mipango. Na kila aliyefanikiwa leo ujue alipanga na kutekeleza mipango yake vizuri siku nyingi nyuma

Leo Ethiopia wanetangaza kutimiza malengo yao waliyojiwekea mwaka 2019 kupanda miti billion 20 ifikapo mwaka 2022

Kati ya nchi ambazo sasa zimekuwa na hali nzuri ya hewa iliyoanza kuwapa mvua nyingi na mazao ya kutosha ni Ethiopia.

Sasa Ethiopia sio tegemezi wa chakula tena kama ilivyokuwa miaka ya 1980 na 1990 kutokana na mipango yao ya kuamua kwa dhoti kupanda miti iliyoanza kuwapa mvua nyingi na za kutosha kuwezesha kuzalisha chakula cha kutosha na kufanya kilimo vizuri

Kwa huku Tanzania tuna Wizara ya Mazingira ambayo viongozi wake hawajulikani kama wapo kazini kweli au wapo kupata hela tu maana hatuoni hata mkazo wa kuondoa Jamie za kifugaji kwenye misitu yetu ambayo sasa inateketea kila kukicha

Hatuoni hata jitihada zenye userious katika kuhamasisha upandaji wa miti kwenye maeneo yetu zaidi watu kila siku kuharibu miti na misitu tu

Kwa sasa Tanzania tumeanza kupata mgao wa umeme kutokana na ukosefu wa mvua ambao unasababishwa kwa kiasi kikubwa na uharibifu wa mazingira ila kwa upoyoyo wetu kuendekeza ujinga itafika kipindi tutakosa vote chakula na umeme kwa kutokuwa serious kuyatunza na kuyalinda mazingira.View attachment 2421253
Mkuu unazungumzia Ethiopia ipi? Hii hii iliyopo Afrika au kuna Ethiopia nyingine kwenye Bara lililogunduliwa karibuni?
 
Tupige vita matumizi ya mkaa, yaani mkaa uonekane kama bangi, biashara haramu, hata kuni zipigwe marufuku kabisa.
Lakini waangalie upya bei ya gesi za majumbani, waondoe tozo katika hii nishati.
Nawasilisha.
 
Tupige vita matumizi ya mkaa, yaani mkaa uonekane kama bangi, biashara haramu, hata kuni zipigwe marufuku kabisa.
Lakini waangalie upya bei ya gesi za majumbani, waondoe tozo katika hii nishati.
Nawasilisha.

Tukiwaambia ccm mmerogwa mnakataa mkaa ni fursa kubwa namibia, kuna aina za miti kama kumi ya kupandwa ni miezi kumi na nane mnavuna na kuchoma mkaa, na miti hiyo hukubali maeneo mengi tu, serikali ikachukue hiyo miti ije itoe elimu kwa wachoma mkaa wapewe maeneo wapande miti yao wawekewe taratibu za uvunaji wapate pesa
 
Namibia amepata soko la mkaa ulaya na marekani na anaingiza mabilioni ya dola sisi tumekazana na gesigesi kwakua hatuna mipango
 
Back
Top Bottom