Wakati hadi Ethiopia wanafanikiwa kupanda miti bilion 20 kwa miaka 4 sie huku tunaendekeza tu wafugaji kukata miti

Wakati hadi Ethiopia wanafanikiwa kupanda miti bilion 20 kwa miaka 4 sie huku tunaendekeza tu wafugaji kukata miti

Nimeona wafungwa wanakata miti na askari magereza.
pale Dar es Salaam nimepita kipindi fulani masaki na oysterbay nimekuta miti ya zamani inakatwa vibaya sana. Ukienda kusini na magharibi mwa nchi hii ndo balaa hakuna mti mpya unaopandwa ila kuna miti inakatwa kwa kiwango cha kutisha sana
 
IMG_0943.jpg
 
Tupige vita matumizi ya mkaa, yaani mkaa uonekane kama bangi, biashara haramu, hata kuni zipigwe marufuku kabisa.
Lakini waangalie upya bei ya gesi za majumbani, waondoe tozo katika hii nishati.
Nawasilisha.
Wazo zuri halina budi kufanyiwa kazi
 
Huu ni uongo miti billion 20 sio jambo dogo kwa miaka 4.

Kwamba kwa siku wanapanda miche 13m kwa kipindi cha miaka 4. 😂😂😂😂😂

Hawa hata ma pyramid watajenga. Wapo juu😂
 
Pesa wanazo waanzishe hata kampeni ya “ Panda mti kwa uhai wa Tanzania “ hapo itatafutwa spicie yakupandwa kulingana na mazingira na miti ya kutiliwa mkazo iwe ile ya rafiki kwa vyanzo vya maji, miti ya matunda na miti ya mbao
Walitangaza kampeni moja this year,wakaweka link ya kutuma proposal,link yenyewe haifunguki.
 
Mkaa huo unaotokana na miti ya kupandwa hua packed hivo na kupelekwa ulaya na marekani na mwingine huuzwa afrika kusini, na kwenye sipermarket zao namibia utaukuta, hizo ndio hoja tunapaswa kujadili sio mambo na ujanjaujanja wa gesi ambayo kiuhalisia watanzania wanaomudu ni wachache mtu ashindie mlo mmoja ataweza kupata pesa ya gesi?
 
Miti ya kupandwa ya mkaa bora iletwe kutoka namibia na wataalamu wetu wakajifunze na tuwe na mashamba mengi ya miti hiyo ya mkaa kiwe kilimo rasmi cha kila mwaka, huku tukiwa na kampeni endelevu ya upandaji wa miti rafiki ya mazingira na kiasi kikubwa miti ya matunda hasa majumbani kwetu, porojo za gesi mimi sitaki kuzisikia watu wetu bado maskini wanahitaji ahueni sio gesi ambayo hata hawawezi kumudu,
 
Walitangaza kampeni moja this year,wakaweka link ya kutuma proposal,link yenyewe haifunguki.

Unatarajia wanaweza wakaja na kitu cha kushikika hao? Ngoja tuwe tunawapa mawazo hapa wakipenda watachukua wasipopenda waache tu, maana sijaona kiongozi mbunifu hapo na sijui wanazurura kila pembe ya dunia wanajifunza ujinga au inakuaje
 
Mkaa huo unaotokana na miti ya kupandwa hua packed hivo na kupelekwa ulaya na marekani na mwingine huuzwa afrika kusini, na kwenye sipermarket zao namibia utaukuta, hizo ndio hoja tunapaswa kujadili sio mambo na ujanjaujanja wa gesi ambayo kiuhalisia watanzania wanaomudu ni wachache mtu ashindie mlo mmoja ataweza kupata pesa ya gesi?
kujadili Gesi sio ujanja ujanja. Ni best solution kwa kweli kikubwa iwe utilised vizuri na kwa kutosha maana tuna Gesi nyingi ila hatujavutia uwekezaji wa kutosha kwenye kuiweka kwenye LPG ili itumike kwa shughuli za kupikia.

Serikali inachotakiwa kufanya ni kuvutia uwekezaji wa kutosha kwenye sekta hii na kuanzisha kampeni kubwa zaidi kuwai kutokea ya kupanda miti hapa nchini
 
Kulikuwa nq mpango wa kila wilaya ipande miti 1.5m. manaake ingepandwa karibu miti milioni mia nne. Ni miti mongi sana hiyo. Lakini wapumbavu wakala pesa za vikao na sikui workshop na kupotea.
 
Kulikuwa nq mpango wa kila wilaya ipande miti 1.5m. manaake ingepandwa karibu miti milioni mia nne. Ni miti mongi sana hiyo. Lakini wapumbavu wakala pesa za vikao na sikui workshop na kupotea.

Hao wakishapata perdiem zao, wakanywa na pombe wakapata na malaya basi sahau malengo yaliyowapeleka, malengo ya miti milioni 400 kila mwaka ni miaka mitano mnakua na miti bilioni mbili hapo utakua na hali ya hewa safi, matunda ya kutosha, mvua nyingi, ukipanda ile miti ya mkaa ndio kabisa unapata fedha za kigeni kutoka nchi kama Kenya, Rwanda, Burundi zambia hapo masoko ni mengi mno
 
Tatizo la Tanzania ni siasa na wanasiasa

Wafugaji wakikabwa, kuna watao watetea.

Ukizuia Mkaa kuna wataolalamika

Yahitajika maamuzi magumu mno
Ndio mana jpm alikuwa anawala vichwa tu..hii nchi bila maamuzi magumu hakuna litakalo fanikiwa.

#MaendeleoHayanaChama
 
Tupige vita matumizi ya mkaa, yaani mkaa uonekane kama bangi, biashara haramu, hata kuni zipigwe marufuku kabisa.
Lakini waangalie upya bei ya gesi za majumbani, waondoe tozo katika hii nishati.
Nawasilisha.
Bila kusahau umeme wa uhakika na wa bei nafuu.

#MaendeleoHayanaChama
 
Back
Top Bottom