Uchaguzi 2020 Wakati kampeni zikianza mwishoni mwa wiki hii, ni dhahiri kuwa mgombea wa CHADEMA, Tundu Lissu atakuwa na mvuto zaidi ya mgombea wa CCM John Magufuli

Pascal Mayalla
Ngoja nikuulize swali jepesi tu hivi unadhani "popularity" ya mtu haiwezi kuwa kigezo mojawapo cha kumpa mgombea ushindi?
Tena kwa kuongezea tuu, haya mambo ya makundi ya watu, mimi nimeshiriki chaguzi zote za vyama vingi toka ule uchaguzi wa kwanza wa jimbo la Kwahani Zanzibar 1993, ukaja uchaguzi Mkuu wa 1995, 2000, 2005, 2010, 2015, hakuna uchaguzi nilishuhudia makundi ya watu kama 2015
Elections 2015 - Hii 'Vox Populi' ni 'Vox Dei' Kuhusu 'Jiwe Walilolikataa Waashi'?

Kufuatia makundi hayo, niliamini, hakuja jinsi CCM inaweza kushinda!.
Kwa Hali Niliyoishuhudia Leo Old Bagamoyo Rd: There is No Way CCM Inaweza Kushinda!

Tena nikaamini
Kama kipimo cha ushindi ni idadi ya watu, Lowassa ndiye rais wetu

Lakini matokeo...
Pamoja na makundi hayo, mtu alibwagwa chini puu!.

P
 
Mbona unakuwa
Uchambuzi wa kitoto sana huwezi kuamini hata kama ni "mwanahabari"ki
 
Sio kwa hii bongo
Wewe jiaminishe hivyo hivyo tu..........

Tuombe Mungu atupe uhai hadi hiyo tarehe 28/10/2020 ili tushuhidie muujiza wa Mungu, kwa kumpa ushindi Tundu Lissu kwa kutumia sanduku la kura!
 
Mwaka 2020 mambo yamebadilika sasa ubaya wa CCM umefika mwisho, hakuna mabaya yasiyo na mwisho, ya Malawi, kenya, Gambia, Congo, Ghana, Zambia yanaenda kutokea Tanzania, malaika na mungu atawapiga Sipana NECCCM washindwe kuiba kura uchakachuaji utaduwazwa na nguvu za maombi ya watanzania wengi wanaotamani mabadiliko, Paskal mayala subiria uone maajabu ya mungu.
 

Pascal, you are a great thinker, you should know that in Tanzania what matters is who declares the winner and not how many votes the candidate gets.
 
Wewe jiaminishe hivyo hivyo tu..........

Tuombe Mungu atupe uhai hadi hiyo tarehe 28/10/2020 ili tushuhidie muujiza wa Mungu, kwa kumpa ushindi Tundu Lissu kwa kutumia sanduku la kura!
Ushetani wa CCM unaenda kufikia mwisho sasa hakuna mabaya yasiyo na mwisho
 
Paschal, wewe ulipaswa kuwa neutral ila tamaa ya ubunge ndio inakuponza, uandishi wako haupaswi kuwa na muegamo. Unaongeleaje kuhusu wagombea wote 18 wa kule Pemba kukatwa, na baadhi ya wa huku bara ambao ni wa vyama vya upinzani?

Halafu hicho amabcho unadhani hakiwezi kutokea, je kikitokea aina ya uandishi wako utakuwaje?, utabadilika tena?
 
Hata ungekuwa ni wewe utapenda kumsikiliza kwa sasai? aliyekuwa anaongea peke yake miaka 5 mfuluizo huku kawapiga pin wenzake ama Lissu mmoja wa wale ambao walikuwa wamepigwa pin?

Jibu lipo wazi.
 
Wewe jiaminishe hivyo hivyo tu..........

Tuombe Mungu atupe uhai hadi hiyo tarehe 28/10/2020 ili tushuhidie muujiza wa Mungu, kwa kumpa ushindi Tundu Lissu kwa kutumia sanduku la kura!
Apewe ushindi kwa tume ipi? Wenyewe mnajua mapema bila tume huru mtaishia kua wapinzani tu miaka nenda rudi + watu wakuliamsha hamna ,,,Kenya yenyewe watu wanatandikwaga mabom na virungu ila kila uchaguzi mtu wa system anashinda sembuse hapa bongo walipojaa ma keyboard warriors mtaishia tu kua na ndoto za mchana
 
JPM hana mtu sahihi wa kushindana naye kwa uchaguzi huu
 

Nilikuwa nikidhani mpaka uvue nguo ndio uitwe kicha,,, kumbe sio lazima tunaishi nao humu humu kila siku.
 
Wasiojulikana kuendelea kutojulikana kwa neno rahisi nikwawao kuendelea 'kudundazi'
 
Haiwezi kuwa Kigezo kabisa Unafikiri Leo Diamond Agombee Urais Nchii hii atapata kisaa no Poporal
Nimesema ni MOJAWAPO ya vigezo na sijasema ni kigezo kikuu
 
Watu wanapenda kusikiliza hotuba za Lissu kwakua zona mvuto, Lissu ana charisma, maneno yake yana fundisha, yana tia moyo, na yanaleta matumaini.
 
Tuombe Mungu, mimi ni mpiga kura wa Kawe, tutamrudisha mchunga Kondoo kwa Kondoo wake asubuhi na mapema.

Kila la kheri katika kumnadi Mchunga Kondoo!
 
Hongera sana kwa msimamo wako, next time hutaachwa hivi hivi. Keki ya Taifa sio ya Mchato pekee ni ya watu wote
 
Lowasa alishinda ila akutangazwa najua hata wewe unajua ila kwa kuwa ni kada unajitoa fahamu tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…