Simba imekuwa timu ya hovyo kuanzia kwenye management,CEO yeye anachojua ni kubana matumizi tu,amekosa mipango ya kudhibiti kambi ya timu,amevuruga utamaduni wa timu yetu,tunafungwa mechi zote kubwa kwa sababu ya ubishi wake.
Ameshauliwa mara nyingi kwenye mechi kubwa timu ikae kambini na ulinzi wa kambi uimalishwe,wachezaji wa timu wasipewe nafasi ya kurudi nyumbani muda wote wa kambi,na kambi iwe mafichoni ili kudhibiti hujuma,wachezaji wetu ni waswahili hawa hawajielewi wanaturubuniwa na wapinzani hata kwa ahadi ya kupewa pesa na vitu vingine, lakini CEO amekuwa mbishi na kujifanya yeye ni professional zaidi na pia amekuwa hataki wazee wetu na wataalamu wetu wa asili wapewe nafasi wafanye jambo lao maana mpira wa africa bila kujizatiti kwa mbinu zote utoboi!!
Matokeo ya ubishi wake ndio ameyaona sasa,mechi kubwa kuanzia ile ya utopolo, timu imekuwa inafanyia mazoezi bunju uwanja ambao hauna hata uzio,mashabiki wanajazana kuangalia mazoezi na mipango ya timu,na wachezaji wanakuwa huru tu,hawana udhibiti wowote matokeo yake tunagongwa tu kama walevi!!nakumbuka mechi ya simba na utopolo iliyofanyika kigoma baadhi ya viongozi wa bodi wakiongozwa na Simba wa yuda Mzee kaduguda,na Asha baraka walikataa kata kata mipango ya CEO wakagoma mpaka wakakabidhiwa timu waweke udhibiti wao kuanzia kambini na kweli isingekuwa wao uto walikuwa wanatuua tena.
Mechi ya ngao ya hisani CEO alishauliwa tena kuhusu kambi na udhibiti wake, akawa mbishi kweli kweli, matokeo yake tukayaona uto wakapenyeza mambo yao tukafa kimoja cha mapema,mpira una matokeo matatu ila mechi hii ya watswana Simba haikustaili kutolewa kwa namna yeyote ile,ubishi wa CEO na Magoli pamoja na mulam ng'ambi ndio umeleta aibu hii kwa taifa,tuliwashauli mapema tuingie kambini mafichoni maana kuna harufu ya hujuma,kuna kiongozi wa utopolo bwana senzo na watu wengine maadui wa Simba Said tuli, Mwenyekiti yule aliejiuzuru, na kiongozi mmoja wa benchi la ufundi,ambao wamekuwa na mawasiliano ya karibu na watu wa galaxy ambao walikuja hapa nchini siku moja baada ya Simba kutoka Botswana, kiongozi uyo wa benchi la ufundi akishirikiana na watu wa uto hasa senzo na mwanachama maslahi wa simba said Tully,kupiga simu kwa watu wa galaxy wakitaka wapewe kiasi fulani cha pesa ili kufanya hujuma,taarifa zote magoli na CEO walipewa ila wakazipuuzia kwa kusema tumeshapita kwakua tulishinda mechi ya uko kwao,ukweli hujuma zipo Simba.
Hata baada ya MO kutia mgomo kusaini mkataba na Azam TV baadhi ya wakurugenzi wa Azam wakishirikiana na kiongozi mmoja wa bodi ya ligi,walikutana mara kadhaa kupanga kuhujumu timu ya Simba ili ionekane timu ya kawaida tofauti na MO anavyojinasibu ili kumkomoa, mambo ni mengi mno na mara zote CEO amekuwa akishauliwa na wadau wafia timu ila amekuwa akipuuzia kwa kiburi chake tu.
Nafikili sasa akili itamkaa sawa,ataelewa soka la bongo limejaa utapeli na watu wapigaji tupu,wazee wa kuchukua muhamala,MO bahati nzuri ABC zote ameshazijua ndio maana aliona ni upuuzi kuwekeza kwa timu ambayo baadhi ya wanachama wakiongozwa na Tully Said,wakishirikiana na watu wa uto na kiongozi mmoja wa bodi ya ligi,kutengeneza mtandao wa hujuma ili timu ikwame kwa maslahi yao,mfadhili wa mpango huo ni mkwepa kodi maarufu nchini mwenye asili ya Yemen mwenye ushirikiano na mstaafu mmoja aliewahi kuwa namba moja nchini.