Wakati Serikali inaendelea kununua ndege kwa taslimu tena ndani ya muda mfupi,hali halisi ya wananchi wako ndio hii huko vijijini

Wakati Serikali inaendelea kununua ndege kwa taslimu tena ndani ya muda mfupi,hali halisi ya wananchi wako ndio hii huko vijijini

Wote tukiwa washangiliaji na wapiga makofi,Bwana mkubwa utakosa watu wa kukumbusha mambo kama haya, na wewe kama binadamu,unaweza ukajisahau.

Wananchi hao wamefikia hatu hata ya kukosa maji ya kuoshea maiti kama wenyewe wanavyoongea katika hii clip.

Ndege tununue na mambo mengine tufanye,lakini tujaribu ku-balance ili na huduma za kijamii kama hizi ziweza kushughulikiwa.

Ununuzi huu wa ndege hizi nyingi tena kwa cash, unafaidisha zaidi mnaowaita mabeberu kuliko wananchi wanaokabaliwa na matatizo mengi yakiwemo ukosefu wa huduma za kijamii, hivyo tujitahidi kuwaangalia sambamba na kununua hizo ndege na kufanya mambo mengine yanayotumia fedha nyingi lakini iwakati huo huo na wananchi wasikose huduma za msingi za kijamii kama maj,afya,n.k...
 
Jamani kwanini tulazimishane ndoto? Huyu anapenda ndege ziwepo hayo mengine si ya muhimu.
Hata sisi tunaompinga hizi ndege twazipanda sana.
Huyo Fatma anazipanda hizi ndege. Mbowe anazipanda.
Kwanini tupinge ili tuonekane tu tunapinga?
Mtu keshatuonesha yeye anapenda ndege hatuwezi mzuia ndio kwanza anatukomoa.
Hao wenye shida ya maji ndio waliompa kura wacha kila mbuzi ale kwa urefu wa kamba yake.
Hata chadema ingeshinda isingepeleka maji kila sehemu.
Mambo mengine kila mtu ajiongeze
 
Aliyeiloga hii nchi alishakufa, yaani utadhania hicho Kijiji siyo sehemu ya hii hii Tanzania tuyoyo jimwambafy kwamba ni dona kantri.
 
Chadema na nyinyi zile bilioni tatu za ruzuku mnazopata kila mwaka kwa nini msiwapelekee wananchi wa hali ya chini vijijini badala yake mnanunulia magari na kujilipa posho kila mnapokaa kwenye vikao vyenu.
Dhiki hiyo hao wananchi wametiwa na ccm,chadema inahusika vp hapo mataga
 
Watanzania walioko huko vijijini wanatabu sana na serikali yao wala haijui na haitaki kujua.
Aliyeiloga hii nchi alishakufa, yaani utadhania hicho Kijiji siyo sehemu ya hii hii Tanzania tuyoyo jimwambafy kwamba ni dona kantri.
 
Wote tukiwa washangiliaji na wapiga makofi,utakosa watu wa kukumbusha mambo kama haya, na wewe kama binadamu,unaweza ukajisahau.

Wananchi hao wamefikia hatu hata ya kukosa maji ya kuoshea maiti kama wenyewe wanavyoongea katika hii clip.

Ndege tununue,lakini tujaribu ku-balance ili na huduma za kijamii kama hizi ziweza kushughulikiwa.

Ununuzi huu wa ndege hizi nyingi tena kwa cash unafaidisha zaidi mnaowaita mabeberu kuliko wananchi wako.
Hovyo kabisa ,kazi kulaumu tu pumbavu nyie
 
Naomba mnijuze, Toka lini Magufuli kaanza kuwa mtetezi wa Wanyonge?

Miaka yote 22 akiwa mbunge wa Birahamulo na baadae Chato, Akawa waziri wa Ujenzi, Mifugo na uvuvi, pia waziri wa Kazi kama sikosei, Sikuwahi kuona utetezi wake kwa wanyonge!

Labda kazaliwa upya sasa.
 
Hopeless! Kama hujui maswala ya uchumi funga domo lako! Hujui hata vichochea maendeleo ya nchi.
Hebu mpinge kwa hoja sio vihoja muelekeze faida ya hayo mandege yanayozunguka kupeleka watu katavi jinsi yanvyobust uchumi. Faida yake wa wananchi maskini wasio na Maji huko vijijini wafanyakazi ambao hawajapandishiwa mishahara. Na mafaida mengine ili aweze kuunga juhudi
 
Huko vijijini huwaambii kitu kuhusu chichiemu.Wacha waisome namba CCM mbele kwa mbele.
 
Chadema na nyinyi zile bilioni tatu za ruzuku mnazopata kila mwaka kwa nini msiwapelekee wananchi wa hali ya chini vijijini badala yake mnanunulia magari na kujilipa posho kila mnapokaa kwenye vikao vyenu.

Hilo ni jimbo la yule aliyepiga bao la mkono!
Alifanikisha meko akapita kwa bao la mkono, then ni kwa nini wananchi wake waachwe wataabike hivyo?
...baada ya kutumbuliwa na kwenda kupiga magoti kwa meko inabidi arudi kwa hao wananchi akawapigie magoti pia!
...ccm imewapumbaza sana!
 
Back
Top Bottom