Wakati Serikali ya Samia ikijitetea huko Geneva, Maovu yake yazidi kuanikwa na vyombo vya habari vya Kimataifa

Hii ni siku chache tu baada ya Serikali ya Samia kupeleka Utetezi feki kwenye kikao cha Umoja wa Mataifa kinachohusu masuala ya Haki za Binadamu huko Geneva, Uswizi.
 
Mjue tunaweza mlaumu yeye sana kumbe haya anaelekezwa na msoga. Halafu msoga anajifanya nayeye ni muangaliaji kama sisi, duniani mtu mnafiki, anakuuwa huku anakuchekea...✍️
Hapana. The buck stops with her. Yeye hana akili mpaka aelekezwe na Msoga? Historia na Legacy itakuwa ni yake na haitakuwa ya Msoga maana Msoga yeye alishapoteza nafasi nzuri sana ya kujijengea legacy iliyotukuka baada ya kushindwa kupitisha ile katiba ya Warioba. Viongozi wa Afrika huwa hawajali mambo ya legacy wala nini isipokuwa tu kujitajirisha wao, familia zao na marafiki/machawa.

Msoga anaweza kuwa anamharibia makusudi lakini when everything is said and done, maovu yote na mazuri yote atabebeshwa yeye na siyo Msoga...
 
Wewe uko kama mimi sikujua kuwa Kikwete ni mbaya ila leo nimeamini shetani wa Tanzania ni Kikwete na Mwigulu Nchemba.
Nilikuwa nagombana sana na Sukuma gang kipindi kile wanampa makavu Mzee wa Msoga. Ila saivi nawaelewa sana Suguma Gang. Yule mzee wa Msoga do chanzo cha mkwamo wa hili Taifa kutokana na kuendekeza kwake maslahi binafsi.
 
Hapakua na sababu ya kufika huku tulipo, ila ndo hivyo ,acha tufike ili tutie adabu.

Kuna watu wakaacha Jitengenezea ufalme wa mbingu wakataka jitengenezea ufalme wa kidunia kisa vyeo vya kidunia.twende tu mda mwalimu, Mungu yupo kazini
 
Huyu mtu tuombe Mungu afanye vinginevyo, utaona mabadiliko makubwa sana. Ila akiwa bado yupo mambo yatakuwa hayahaya. Watu wanasahau utekaji ulianzia kwake, haya ni muendelezo tu. Mtu mzima unasimama na kuuliza eti hivi tuna sheria mbaya kiasi kwamba watu wanakataa kushiriki uchaguzi? Ni matusi makubwa sana kwa Watanzania.

Hajali hana uchungu na Watanzania. Yeye kama mstaafu pekee aliyebaki kwa hapa, ndiye angekuwa msuluhishi mzuri na kusaidia kufanya reforms. Kwa makusudi kabisa anajua kufanya reforms zozote mali zake ziko matatani. Kila leo anaongeza umiliki wa vitu, inaweza fika nusu ya nchi vitu ni vyake juzi kuna kampuni ya simu yumo, mimi huyo mtu alishanitoka kabisa.
 
Japo mwenzake alisema kuwa wazuri hawafi...labda ipo siku nao watakufa maana you never know!😡
 
Nakubaliana na wewe. Huyu mzee na ubinafsi wake na tamaa zake za kutaka kuneemeka yeye na kizazi chake tu ndo wanasababisha mkwamo mkubwa sana kwa hili Taifa.
 
Kama wanatutetea tusitekwe na kuuliwa na viongozi tuliowapa madaraka wenyewe hao ndiyo marafiki wa kweli, adui mkubwa wa watanzania kwa sasa ni serikali yao wenyewe.
 
Hana muda mrefu watamfix na yeye
 
Nimeota kuwa hata ule u rais wa bunge la dunia uko matatani kwa ukiukaji wa haki za binadamu nchini.
Mungu hachelewi kuonya penye hata dalili ya uovu na huangamiza uovu unapozidi.Ifike mahali uchawa na chawa waharamishwe kwenye taifa letu.Tena kibidi kwa mswaada wa hati ya dharura.Binafsi nawabebesha hili zigo.
 
Dola ikiogopa social media, hasa Twitter au X, YouTube etc etc..
Ikiwapiga mikwara magazeti yanayokosoa maovu na ufisadi.
Viongozi wa kila sehemu wakiamriwa kila sentensi kumsifia na kulitaja jina la kiongozi mkubwa.
Ikulu ikiingiliwa na matapeli wasio na hili wala lile...
Ujuwe hapo Dola ni banana republic!
Ni uonevu, unyanyasaji, utekaji, uuwaji na udikteta!
Hakuna uongozi wa kidemokrasia, mwisho wake wawa mbaya sana kwa walio madarakani! Hata wafanye nini, lazima wataangukia pua tu!
 
Aisee
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…