Wakati Tanzania watawala wanatishia kufungia X, Ruto asema ataendelea kuingia space X, ndio safari imeanza

Gen z wanapigania maisha sawa kwa wakenya wote, Kenya ni ya wote na sio wachache. Kila mwaka Wakenya wanao kufa kwa kukosa huduma za afya ni maelfu kwa maelfu.


Tanzania Serikali yake haina tofauti na ile ya Makaburu wa South Africa tena bora hata wale.

Kuna raia wangapi Tanzania wanakufa kwa kukosa huduma za afya? Sio jana tu Morogoro kijana wa SUA kafa kwa sababu ya huduma za kihuni za afya? vipi na yeye kafa akiwa anaandamana?

Hapa Bongo report za CAG huwa ni za kwenda kujitawazia chooni make hazifanyiwi kazi na hata report ya mwaka huu labda isha ishilia chooni.Haya ndio oia Gen z walikuwa wanapigania vitu kama hivyo.
 
Nitajie wewe hao raia wanaokufa Kwa kukosa Huduma ya Afya maana Huwa mnaropoka bila kujua mnachoongea.

Una uhakika ripoti za CAG hazifanyiwi kazi?

Mwisho Kenya na Tanzania wapi wanatawaliwa kama makaburu? Umewahi sikia mauaji ya raia kienyeji hapa Tanzania?

Hivi Kwa nini Huwa unaropokatuu hovyo mambo ambayo huwezi thibitisha?
 
Wako chini ya 200
wilaya 184 weka na Wakurugenzi ni wengi zaidi ya hizo wilaya. Njoo kwa wakuu wa mikoa na RAS mikoani tu Offisi ya mkuu wa mkoa hukosi V8 zaidi ya 7

Hao wakuu wa wilaya 184 bado gharama za matengenezo bado mafuta unazamia ni pesa ndogo?
 
Anatukiza mvutano wa Kisiasa.

Nataka kujua Hadi Sasa hao Gen Z wamepata nini baada ya kuuwawa na kujeruhiwa?
Maisha ni hadithi... kufa au kujerehuliwa ni suala la muda na mazingira.
Muhimu usife kizembe bila kuwa chachu ya mabadiliko kwenye mifumo ya utawala!
Kubwa walichopata ni kuiambia dunia yaliyojikita kwenye mioyo ya viongozi wao!
Ni ushindi mkubwa sana maishani!
 
Hao wamekufa na kujeruhiwa kizembe
 
Kama wakifungia x tutawakuta kwao
 
Kuna mjinga humu ameng'ang'ania kuuliza Gen Z walifaidi kivipi, bado amekwama kwenye akili za kijinga zenye ubinafsi.
Hawa vijana walichofanikisha haitokaa tukisahau, wameshangaza taifa lote, leo hii hata wabunge wameogopa sana kwamba hatuishi kwa mazoea tena, kwamba vijana wana uwezo wa kufanikisha maandamano bila kuongozwa na kiongozi yeyote, wao kwa wao wanahamasishana kwenye mitandao na kumfanya rais na uongozi wote wakose amani.
Miswada kwa sasa itaangaliwa kwa makini sana, maana huo ulipigwa chini na kuondolewa na bado rais anaendelea kubanwa.
 
Kwenye sheria kuna kitu kinaitwa " Capacity to contract" haoa ruto anaonesha ana capacity ya kusikiliza machungu ya wakenya kupitia x. Sasa hapa kwetu nadhani hiyo capacity haipo. Watu hawataki kusikia machungu wanataka kusifiwa tuu
 
Unabishana na wajinga wa hili Taifa, amini nakuambia hii nchi ina wajinga wengi sana
 
Huku kuna watetezi wa Wanaolawiti wanafunzi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…