Mfiaukweli
JF-Expert Member
- Aug 30, 2018
- 5,636
- 8,777
Mkakati - kama mtu anaweza kuuita hivyo- wa serikali ya awamu ya tano kupambana na COVID-19 kuwaambia watu "waendelee kuchapa kazi huku wakichukua tahadhari". Binafsi ninachokiona ni kuwa serikali hii imeamua kufuata falsafa ya "do-nothing-and-the-problem-will-go-away". Kwa nini?
1. Naomba mtu anieleweshe kazi watakaoichapa waajiriwa kwenye makampuni yaliyofungwa (na yanaendelea kufungwa) kwa mfano mahoteli, shule, kampuni za utalii, mashamba ya maua, kampuni za ndege za kukodi, tour guides etc, etc,etc. Sioni (na sijasikia) serikali ikianzisha jitihada zozote kuwezesha biashara hizi ziendelee kuendeshwa ili watu wachape kazi.
2. "Chukua tahadhari" ina maana gani in practice? Ni kunawa mikono na kuvaa barakoa pekee? Senegal wametangaza kutengeneza kifaa cha kupima uwepo au la maambukizi ya coronavirus ambacho gharama yake ni sawa na Dola moja ya Kimarekani, kwa nini tusivitumie ili tuweze kupima watu wengi zaidi ili kuepusha maambukizi mengine mapya?
Hatuwezi kuishi kama kisiwa na tukafanikiwa. Lazima tushirikiane na mataifa mengine kukabiliana na janga hili, vinginevyo tutazidi kutengwa.