Ni propaganda kutumia usemi huu bila kutazama kwa mapana yake.
UKIMWI tunaishi nao ni kweli, ila jitihada zilizofanyika kuzuia maambukizi yake kwa kasi na madhara yaatokanayo na ugonjwa huu kwa mida wa zaidi ya miongo 3 ni kubwa mno.
Tulipoteza nguvu kazi kubwa sana Kama taifa kabla ya
Kupekeka elimu ya UKIMWI kwa watu wengi na makundi maalumu
Kupunguza unyanyapaa
Kuandaa sera na miongozo ya tiba za wagonjwa wenye UKIMWI
Kupatikana kwa dawa za kufubadha UKIMWI
Kupatikana kwa condoms
Kuandaa kwa sheria za usimamizi wa janga hili na mambo mbalimbali mtambuka .
Kwa upande wa covid-19 bado tuko mahala pagumu. Hadi Sasa
Hatuna chanjo dhidi ya COVID-19
Hatuna tiba mahususi
Hatuna huduma nzuri kwa wagonjwa critical wa Covid-19
Hatujawa na mfumo wa kisera wa kukabiliana na kuzuia maambukizi
Elimu na ushirika wa jamii ili kupambana na janga hili bado upo chini na jamii Bado haijahamua kubadilika
Ukweli ni kwamba kujifariji kwa misemo ya kuwa tujifunze kuishi na COVID-19 Kama magonjwa mengine ni sehemu ya propaganda ili kukwepa uwajibikaji
Sent using
Jamii Forums mobile app