Wakati tunafurahia kichekesho cha TRAB na TRAT tukumbuke trilioni 360 ni pesa nyingi sana

Maprof. walimwongopea Magufuli, hakuna pesa za hivyo. Lisu aliposema zile report ni za kupika na hazina ukweli wowote, nusura wamtoe roho.
 
Serikali inapaswa kumwita Prof Osoro na waongozane kwenda Ofisi za Barrick ili Osoro akafafanue vizuri yale mambo aliyoyaandika kwenye report yake.
 
Magufuli alikua fiksi yule mzee..japo kuna maeneo alifanya poa nampa 1/10

Sent using Jamii Forums mobile app
 
JPM alitumia hisia zaidi ya kutazama suala husika kiuhalisia. Ndiyo! Alikuwa na tamaa kubwa sana ya maendeleo, lakini alijikuta akiishi ndani ya matamanio ya kufikirika kutokana na ndoto zake za alinacha.
Kwahio reality ni sasa mgao wa umeme kurudi kutafuta crane ya Bwawa kama needle in the haystack na mkuu wa nchi kuzurura hovyo hadi kupelekea kukaa ugenini zaidi ya wiki kwa kufanya kazi za akina Diamond, bila kusahau kuwazima wanaoongea kwa kuwatafutie vikazi vya ajabu ajabu...?

Kama huo ndio U-Alinacha Had rather live kwenye ndoto yenye ahueni kitaa kuliko uhalisia wenye faida ya wachache wakati majority ndio tuna-facilitate their extravagant lifestyles
 
Hizi Tirilion 360 ndiyo tumezikosa kwa sababu serikali legevu.Kwa sasa hakuna mwenye uwezo wa kuzidai
 
Hizo trilioni we umeziona wapi achana na mambo ya kusadikika. Huo ni utopolo wa genge la wasukuma likiongozwa na kina Luhaga Mpina. Alikuwa wapi mpk asubiri kutemwa uwaziri? Msikubali kutimika kwa maslahi ya wajanja wachache pambana na mambo yako
 
Tunao vijana wajinga sana nchi hii. Wale wenye influence na kuweza kupata wa kuwasikiliza wamejawa na mambo ya kipuuzi.
*****

Sent from my SM-A125F using JamiiForums mobile app
Kwann unashutumu vijana tu wakati nafasi nyeti zote zimeshikiliwa na wazee? Kuanzia jpm, kabudi, maprofesa waliotoa ile ripoti, mpaka walio-negotiate kutoka trilioni 300+ mpaka bilioni 700 kuna kijana hata mmoja?. Vijana maisha yanatupiga sana huku mtaani tupumzisheni kidogo na masimango basi
 
Hayo madai yalikua halali au zilikua siasa? Tuanzie hapo kwanza
 
Badala ya kupambania maovu yanayofanywa na kuangamiza vijana wenzso, wao wanajikita kwenye mizaha
 
Aisee kweli sisi ni wajukuu wa Chief Mangungo.

Tunauza haki yetu hivi hivi na kuwakejeli wanaoipigania.
 
Serikali inapaswa kumwita Prof Osoro na waongozane kwenda Ofisi za Barrick ili Osoro akafafanue vizuri yale mambo aliyoyaandika kwenye report yake.
Hakika
 
Hizo trilioni we umeziona wapi achana na mambo ya kusadikika. Huo ni utopolo wa genge la wasukuma likiongozwa na kina Luhaga Mpina. Alikuwa wapi mpk asubiri kutemwa uwaziri? Msikubali kutimika kwa maslahi ya wajanja wachache pambana na mambo yako
mkuu na 700billioni vp ?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…